SoC01 Lishe bora ndio msingi wa maendeleo ya jamaii na Taifa kwa ujumla

Stories of Change - 2021 Competition

Salimu Kajembe

New Member
Nov 5, 2018
4
4
Kiuhalisia kabisa jamii nyingi za kitanzania kuanzia wananchi wa kawaida mpaka viongozi wa maeneo husika wakiserikali na hata wale wasio wa kiserikali imekuwa ni kawaida sana kutumia muda mwingi na nguvu kubwa sana kupambana na changamoto zilizozoeleka ambazo ndio zinaonekana kwamba ndio viini vikubwa vya matatizo katika jamii,changamoto hizo ni kama vile Uhaba wa Maji,Ukosefu wa Umeme,Upungufu wa Huduma za afya,ubovu wa miundombinu ya bara bara na kadhalika.

Nikweli sehemu kubwa ya jamii za kitanzania ikihusisha vijiji mbali mbali,mitaa na maeneo mengine yaliyo na makazi ya watu yanakabiliwa na changamoto nyingi sana,changamoto za kimiundominu,kimaadili,kijamii,kimazingira ,changamoto za kituwala na kadhalika.

Pamoja na changamoto zote hizo,lakini watanzania tunasahau changamoto muhimu sana na kubwa sana ambayo binafsi mimi naona ndio mzizi wa matatizo mengi sana katika jamii zetu na nchi yetu kwa ujumla japokuwa changamoto
hiyo haipewi uzito unaostahili.

Changamoto hiyo ambayo kwa namna moja au nyingine naweza kusema imesahaulika ni Lishe duni au ukosefu wa lishe bora ambao hutokana na mlo kamili kwa watanzania walio wengi sana.
Labda naomba kutoa kidogo maanaa ya Lishe ili jamii ipate kunielewa kwa upana wake,dhamira kuu ya andiko hili ni kuweza kujenga mitazamo chanya itakayoweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye afya za watanzania kinyume na ilivyo sasa.
Lishe ni mchakato mzima kuanzia chakula kinapoliwa,kinapomeng'enywa/kuyeyushwa,kufyonzwa virutubishi na kutumiwa mwilini kwa ajili ya ukuaji,uzazi,kinga ya mwili,kupumua,kufanya kazi mbali mbali,kujenga afya na uhifadhi wa virutubishi na nishati katika sehemu sahihi ndani ya mwili.Hiyo ni maana ya Lishe kama ambavyo nimejaribu kuilezea.Baada ya kuelezea maana ya Lishe sasa naomba nielezee maana ya neno mlo kamili ili jamii iweze kunielewa vizuri kusudi la kuandaa andiko hili.

Mlo kamili ni ule ambao hutokana na makundi mbali mbali ya vyakula ambao una virutubishi vyote muhimu kwa ajili ya lishe na afya bora kwa ukuaji na ustawi wa afya ya mwanadamu.

Yafuatayo ni makundi Matano ya chakula.

1: Matunda
Aina mbalimbali za matunda hulimwa na hupatikana katika nchi za Afrika mashariki na Duniani kwa ujumla na matunda hayo ya aina tofauti tofauti yanapatikana karibia mwaka mzima. Kuchagua matunda kutokana na msimu huleta thamani na ubora zaidi. Kula matunda kutokana na msimu wa matunda kunaongeza matumizi ya matunda aina nyingi zaidi kwa mlo wako katika mwaka mzima kwa bei nafuu. Na kama na vile matumizi ya mboga za majani, kula matunda kama vile pome apple(tufaa) na peasi,machungwa kama vile Mandarins na Zabibu,matunda jiwe kama vile mapera, cherries, persikor, nektariner na squash,matunda hari kama vile ndizi, papai, maembe, mananasi na tikiti ,Matunda mengine kama vile matunda ya pasheni yote hayo huchangia kupata aina tofauti ya madini na virutubisho kwa ajili ya afya binadamu.

2: Mboga mboga
Kundi hili la mboga limegawanyika katika makundi madogomadogo yenye virutubisho sawa,ikiwa ni pamoja na mboga za majani kijani, nyekundu na rangi ya machungwa, mboga zenye wanga, mboga za maharage na mbaazi. Madhumuni ya makundi haya madogo ni kukuongezea kula aina mbalimbali za mboga kutokana na virutubisho vyake.

3: Vyakula vyenye protini
Vyakula hivyo ni kama Nyama ya kuku, samaki, dagaa, mayai, karanga, mbegu, bidhaa za soya na maharage, mbaazi huunda kundi la chakula chenye protini .
Ingawa kunde na maharage zipo katika kundi la vyakula vyenye nyuzinyuzi vyakula hivi huwa ni chanzo cha vyakula vyenye protini. Inashauriwa kula nyama ya kuku na nyama kutoka kwenye samaki na vyakula vingine kama vinavyopatikana kwenye mimea ili kuongeza afya ya mwili wako kwa kutokula nyama nyekundu kama za wanyama wa kufugwa au wa polini.

4: Vyakula vya wanga (Nafaka)
Vyakula vya nafaka ni vingi vilivyotengenezwa kutokana na ngano, shayiri, mchele, mtama na mahindi. Nafaka mbalimbali zinaweza kupikwa na kuliwa nzima, kusagwa kuwa mfumo wa unga na kupika aina mbalimbali ya vyakula kama mkate, ugali, uji, vitumbua, ama maandazi kwa ajili ya kifungua kinywa. Vyakula vya nafaka huupatia mwili wanga. vya wanga kwa kubonyeza.

5: Maziwa
Kundi la maziwa ni kundi lenye vyakula na mazao yake zikiwemo bidhaa za maziwa na huwa na kiwango kikubwa cha madini ya kalsiamu. Maziwa ya mgando, jibini zaidi na bidhaa zote zenye maziwa ni sehemu ya kundi la chakula cha maziwa. hata hivyo maziwa ya soya pia huwa ni sehemu ya kundi la maziwa licha ya kukosa madini ya sodiamu kwa wingi, pamoja na maziwa ya soya siagi ya maziwa huhesabika pia katika kundi la maziwa, Maziwa huwa muhimu na ni chanzo kizuri cha madini kalsiamu.

Hizo ni maana ya Lishe na Mlo kamili,nimejaribu kueleza maana ya hayo maneno ili jamii iweze kuelewa ninapozungumzia Lishe kuwa namaanisha nini,na pia ninapozungumzia Mlo kamili pia jamii iweze kunielewa namaanisha nini.Ukosefu wa Lishe bora inayotakana na Mlo kamili ni changamoto kubwaa sana kwa watanzania vizazi na vizazi,chamoto hii ni kubwa sana tofauti na hata uhalisia wa takwimu zilizopo sasa zinozotambulika na serikali pamoja na mashirika kadhaa yanayoshughulika na masuala ya Lishe na udhibiti wa utapiamlo na udumavu katika jamii zetu.

Mimi binafsi mwaka 2017 nilishawahi kufanya kazi na shirika flani ambalo siwezi kulitaja hapa,kazi hiyo ilikuwa ni kufanya tathimini kutambua uelewa wa wananchi juu ya masuala ya Lishe na Utapiamlo,lakini pia tathmini hiyo ilihusu kutambua watoto waliopata matatizo ya utapiamlo katika wilaya za Chamwino na Kongwa mkoani Dodoma.

Kitu ambacho kilinishangaza ni kwamba kuna vijiji vingi sana ambavyo viko ndani ndani ambapo kuna changamoto kubwa sana ya watoto wengi kuzaliwa wakiwa na Utapiamlo mkali sana na baadhi yao kuwa na utapiamo wa wastani,hao ni kwa upande wa wale waliozaliwa ambao kimsingi tunasema tatizo la Lishe duni hapo lilianzia kwa wazazi wao kipindi ambacho ni wajawazito,lakini pia kuna wale ambao ni watoto wa miaka mitano kushuka chini mpaka miwili,wao nao ni wengi sana wenye matatizo ya utaliamlo,na wengi wao tayari wameshapata tatizo baya zaidi la udumavu kwasababu mtoto wa miaka mitano ukimuangalia unaweza hisi ana miaka miwili au mitatu.

Wakati nafanya tathmini hiyo moja ya mambo niliyokuwa nimeyabaini ni kwamba jamii zetu nyingi hazina elimu au uelewa wa kutosha kuhusu maana ya Lishe na Mlo kamili,na umuhimu wake kwa ukuaji kwa watoto katika kuimarisha afya ya mwili wa mtoto na afya ya akili.

Hiyo ni kwa upande wa baadhi ya vijiji vya Kongwa na Chamwino Mkoani Dodoma pekee,tena ni kwa wakati huo mwaka 2017 tu ,na hapo tulitumia nguvu kubwa sana kuweza kuwatambua watoto wa aina hiyo,je tujiulieze Tanzania ina mikoa mingapi? Wilaya ngapi,Tarafa ngapi? Kata ngapi na vijiji vingapi vyenye jamii zenye watoto wa aina hiyo?
Naomba tutambue kwamba utapiamlo huwa Una madhara makubwa Sana ,kuna mamdhara ya muda mrefu na madhara ya muda mfupi kama vile
Udumavu wa mwili ambao husababisha mtu kuwa na umbile dogo ambalo halilingani na umri wake.

Udumavu wa akili ambao hupelekea mtu kuwa na uelewa hafifu wa mambo,mfano uelewa duni darasani na hata kwenye masuala mambo mengine ya maisha!
Pia utapiamlo huweza kupelekea magonjwa ya mara kwa mara mwisho wa siku kifo.

Kwa ujumla tatizo la utapiamlo Tanzania ni Jambo mtambuka ambalo linapaswa kupewa kipaumbele Sana kutokana na ukubwa wa madhara yake ya moja kwa moja katika jamii zetu.

Ukiangalia watengaji na watumishi wote katika nchi hii hutoka katika jamii hizi za kawaida(Masikini),wanasiasa na viongozi wengine wengi,wakiamo viongozi wa dini na wakiroho wote hutoka katika jamii hizi hizi za kimasikini,kutokana na hivyo tunaweza kujikuta tunalaumu kuwa na watendaji WA serikali wasio na uwezo au viongozi na wanasiasa wasio na uwezo wa kutosha kiuongozi kutokana kwamba nao walipitia changamoto za kupata tatizo la utapiamlo wakati wakiwa watoto hivyo kupelekea kuathiri utengaji kazi wao na utekelezaji wao wa majukumu kama viongozi kivyo kupelekea taifa kuwa na viongozi wasiofaa ambao hwataweza kutufikisha katika nchi ya ahadi kama tulivyojipangia.

Dhumuni kuu la andiko hili ni kufumbu akili jamii na serikali kulipa umuhimu na kipaumbele tatizo la utapiamlo katika jamii zetu kwasababu madhara yake ni makubwa Sana Kwa mtu mmoja mmoja,jamii na nchi kwa ujumla tofauti na watu wengi wanavyolichukulia kwa sasa.

Kama tuna ndoto za kuzalisha viongozi na watumishi bora,hodari na wenye weledi tunapaswa kuweka mkazo zaidi kwenye mzizi wa tatizo ambalo ni utapiamlo uliokithiri katika jamii zetu nyingi.

Kama inavyofahamika viongozi wazuri huandaliwa tokea wakiwa tumboni Kwa Mama zao,hivyo serikali na wadau wote wanapaswa kuwekeza nguvu kwenye afya za watoto tokea wakiwa tumboni kwa mama zao,baada ya kuzaliwa na muda wote wa ukuaji wao.

Tusitumie nguvu nyingi tu kutumia mamilioni ya Pesa kupeleka watoto kusoma shule za gharama wakati mzizi wa tatizo tunakuwa tumeuacha,ni rahisi Sana mtoto akasoma shule nzuri na akafaulu vizuri tu lakini kama huyo mtu aliwahi kuwa na tatizo la utapiamlo ni dhahiri kwamba atakosa ule weledi na ufanisi wa ufanyaji kazi zake,tumeona wanasiasa wengi wakikosa misimamo,unakuta mwanasiasa Leo anasema hivi Kesho anasema vile,au kiongozi mkubwa tu anakosa msimamo wa dhati kama kiongozi,huko ni kukoza weledi,na ukiangalia mbali unaweza kuta ni matokeo ya kukosa lishe bora na mlo kamili ambao umemfanya kuimarika kiafya ya akili na kuongeza weledi na kujitambua katika kutimiza majukumu Yake kwa manufaa ya anaowaongoza.

Ningependa ifahamike kamba ukosefu wa lishe bora haiko Kwa familia masikini pekee,hapana,ukosefu wa lishe bora unaweza kuwepo kwenye familia za kimasikini na hata familia za kitajiri,kwasababu lishe bora itaokanayo na mlo Kamil ni suala la elimu tu juu ya namna ya kutambua na si Hali zaaisha,kwasababu ziko familia za kimasikini lakini zinazingatia mlo kamili na ziko familia za kitajiri lakini ndio zinaongoza kuwa na tatizo la utapiamo kwasababu hazina elimu juu ya lishe Bora na mlo kamili,zinakula vyakula bila mpangulio.

Ni Imani Yangu kubwa Sana,jamii husika,serikali na wadau wote kwakupitia andiko hili kutakuwa na mabadiriko chanya Sana katika jamii zetu hivyo kuweza kuzalisha wataalamu bora na viongozi wenye weledi wwtakatufikisha kule tunapotaka kwenda kama taifa.

Andiko hili limeandaliwa na kuandikwa na Salimu Juma Kajembe.

P O BOX 11077,DODOMA.

SIMU +255 657 752 155

Email: kajembesj@gmail.com

Ahsante Sana..!
 
Back
Top Bottom