Lipumba Slams IMF's Stance On EPA Scam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba Slams IMF's Stance On EPA Scam

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ochu, Sep 2, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Lipumba aishangaa IMF
  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishangaa Shirika la Fedha Duniani (IMF), kummwagia sifa, Rais Jakaya Kikwete, kwa jinsi anavyoshughulikia suala la wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA).

  Lipumba ameonyesha hali hiyo, ikiwa ni siku moja tu imepita, baada ya Mkurugenzi wa IFM, Dominique Strauss-Khan, kutoka Washington, Marekani, kummiminia sifa Rais Kikwete kwa jinsi uongozi wake ulivyosimamia urejeshwaji wa fedha za EPA, zilizoibwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, mwenyekiti huyo, alisema kitendo cha Rais Kikwete kutotumia ipasavyo madaraka yake kukabiliana na wezi na wahujumu uchumi wa nchi, hakipaswi kupongezwa kwani ni ukiukwaji wa utawala wa sheria.

  Profesa Lipumba ambaye ni mtaalamu wa mambo ya uchumi, alisema kashfa ya EPA, haijawahi kutokea katika benki yoyote duniani.

  “Tukio kama hilo halijawahi kutokea katika benki yoyote ile duniani, lakini IFM wanapongeza hatua za rais za kutowachukulia hatua wezi hao, hili kwa kweli linanishangaza,” alisema Lipumba.

  Akikaririwa na vyombo vya habari juzi, Mkurugenzi wa IMF, alisema tukio kama la wizi uliofanyika BoT, linaweza kutokea popote duniani, jambo ambalo Profesa Lipumba alipingana nalo.

  Mapema mwezi uliopita, CUF iliandaa mkutano na waandishi wa habari ambapo Lipumba aliwalaumu wahisani wakubwa wa Tanzania kama Benki ya Dunia (WB) na IMF, kwamba wamekuwa nyuma kuisaidia serikali katika vita dhidi ya ufisadi na badala yake wamekuwa wakiisifia kwa kila jambo, hali inayochochea kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi.

  Akilihutubia Bunge mjini Dodoma Agosti 21 mwaka huu, Rais Kikwete alisema serikali imekamata mali za wamiliki wa kampuni 13 kati ya 22, waliothibitika kuhusika na uchotaji wa sh bilioni 133 kwenye Akaunti ya EPA, ambapo kiasi cha sh bilioni 53.7 zimekusanywa, huku hati zao za kusafiria zikishikiliwa.

  Rais Kikwete alisema watuhumiwa hao wameongezewa siku 72 kuanzia Agosti 21 ili wawe wamerejesha sh bilioni 74, baada ya muda huo kupita watachukuliwa hatua za kisheria.

  Kutokana na hatua hiyo, viongozi wa kambi ya upinzani na makundi kadhaa ya wanaharakati, walipinga, na kuitafsiri kuwa ni sawa na kutangaza msamaha kwa wezi hao.


  source: Tanzania Daima
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  The best President Tanzanians will never have....
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  .......Mercy/parole to thieves!
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Sep 3, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lipumba,
  At last, unaongea vitu.....
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Date::10/6/2008
  Profesa Lipumba adai IMF inachochea ufisadi
  Na Kizitto Noya
  Mwananchi

  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amelituhumu Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwamba linachochea na kuendekeza rushwa na ufisadi nchini.

  Profesa Lipumba alitoa shutuma hizo nzito upitia barua yake aliyomwandikia Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Dominique Strauss-Khan.

  Katika barua hiyo ambayo jana aliamua kuigawa kwa vyombo vya habari, Profesa Lipumba alidai amebaini kwmba IMF ambayo imekuwa ikiheshimika kwa miaka mingi, ina mkono katika matukio ya ufisadi yanayoendelea hapa nchini.

  Alisema amebaini hilo kutokana na shirika hilo kufumbia macho matukio kadhaa ya ufisadi nchini na kitendo chake cha kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa hatua ya kuwapa muda wa kurejesha fedha mafisadi wa EPA badala ya kumponda.

  “Sikusoma popote zaidi kujiridhisha kwamba ulisema, niliamini kwamba taarifa iliyotolewa na gazeti la serikali hapa nchini, The Daily News kuhusu mazungumzo yako na Rais Kikwete ni sahihi. Kauli yako inachochea rushwa na kuendekeza ufisadi Tanzania,” alisema Profesa Lipumba katika barua hiyo ya Septemba 26, mwaka huu yenye kumbukumbu namba CUF/AK/ DSM/MKT/001/IMF/2008.

  Septemba mosi mwaka huu, gazeti la Daily News lilimkariri Mkurugenzi Mtendaji wa IMF akimsifia rais Jakaya Kikwete kwa hatua alizochukua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi wa EPA.

  Kwa mujibu wa gazeti hilo, katika mkutano wao uliofanyika kwenye hoteli ya Omni Shoreham, nchini Marekani, Mkurugenzi huyo wa IMF alisema “Tumeridhirika sana na kukupongeza jinsi ulivyoshughulikia suala la EPA. Suala hilo linaweza kutokea popote duniani lakini cha msingi ni jinsi ulivyolishughulikia. Na umelishughulikia vizuri kwa umahiri na utalaam wa hali ya juu. IMF sasa imefunga suala la EPA,”

  Profesa Lipumba alisema kauli hiyo ya IMF, inachochea rushwa kwani ni ukweli usiofichika kwamba serikali imeshindwa kushughulikia suala hilo kwa umahiri wala utaalam wa hali ya juu kama mkurugenzi huyo anavyodai.

  Akifafanua alisema: “Serikali haikuwa wazi kuueleza umma jinsi fedha hizo zilivyochotwa, watuhumiwa bado hawajulikani kwa majina na makampuni hayajafikishwa mahakamani,”

  Kwa mujibu wa Profesa Lipumba kitendo cha Rais Kikwete kutaka watuhumiwa wa ufisadi wa EPA warejeshe fedha, kinaleta shaka kuwa hatawafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili, kitendo ambacho ni kinyume na utawala bora na sheria.

  Alisema rais Kikwete amewasamehe watuhumiwa wa EPA na kauli yake haionyeshi nia thabiti ya serikali kuwafikisha mahakamani hivyo kumsifu kwamba amelishughulikia suala hilo kwa umahiri sio sahihi.

  Aliitaka IMF kuongeza umakini katika kupitia hali ya uchumi wa Tanzania katika vikao vyake vijavyo na kuishikiza serikali kusimamia mapendekezo ya ripoti ya awali iliyokagua akaunti ya EPA mwaka 2006 iliyotaka nchi iache kuendelea kulipa madeni hayo kwa kuwa yamepitwa na wakati.

  Katika hatua nyingine Profesa Lipumba jana ameeleza kuwa msimamo wa chama chake kuandamana kwa lengo la kuishinikiza serikali itaje majina ya watuhumiwa wa EPA na kuwafikisha mahakamani, uko palepale.

  Aliwaambia waandishi wa habari kuwa maandamano hayo yamepangwa kufanyika Oktoba 6 mwaka huu kuanzia Buguruni kupitia barabara ya Uhuru hadi viwanja vya Mnazi Mmoja ambako viongozi wakuu wa CUF watahutubia.

  Profesa Lipumba alibainisha kuwa ingawa polisi wameshajulishwa kuhusu maandamano hayo, baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wameanza kuyawekea mizengwe kwa kuzuia viwanja hivyo.

  Alisema baada ya CUF kumwandikia barua mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumjulisha juu ya maandamano hayo kuishi katika viwanja vya Mnazi Mmoja, aliwajibu kwa barua kwamba viwanja hivyo haviruhusiwi kwa shughuli za kisiasa.
   
 6. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180

  Hao ndio watanzani. Wanaona matatizo na wana-react kutokana na wakati uliopo. Sio wengine wakiona matatizo wanataka kurudi kwenye Ujima.
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Huyu naye keshaishiwa
  angeanza na bilateral agreements kama tulizo nazo na waingereza kupitia DFID ambao wana chochea ufisadi zaidi Tanzania kuliko hao IMF

  mchumi mzima anaboa
   
 8. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280

  really?????
   
 9. C

  Chief JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2008
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  GT.
  Nadhani ingekuwa bora zaidi kama ungetufahamisha kuhusu hizo bilateral agreements tulizonazo hasa ya DFID tuweze kujua jinsi gani ufisadi umejikita.
   
 10. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #10
  Oct 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  By Beatus Kagashe
  [​IMG]
   
 11. M

  Masatu JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyu poor profesa amechoka kufikiri..
   
 12. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kikwete ameamua kutokuwachukulia hatua za kisheria watu waliohusika na EPA, skandali ambalo yeye alionyesha bungeni kwamba lilikuwa ni ufisadi. Kwa maneno mengine amewasamehe.

  IMF imesema Kikwete ame handle vizuri scandle la EPA.

  Profesa Lipumba akasema IMF wanachochea ufisadi kwa kumpongeza Kikwete kwa sababu hizo hatua za Kikwete hazitoshi.

  Sasa huyu "poor profesa" amechoka vipi kufikiri hapo ?
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  unajua kuna mtu aliwahi kuniuliza idadi ya marais duniani wanaoitwa ma professa nikashindwa kuwataja hata mmoja labda OBAMA akiwa rais maana university of Chicago wamesema alikuwa ni professor
  [​IMG]
  Huyu Lipumba kusema ukweli ni disgrace na alizidi kuwa disgrace pale alipokuwa akikampeni nchi za Scandinavia zitukatie misaada in the 90's

  saya alot about where his priorities are

  ngja tukishamaliza na Mbowe itabidi tuhamie kwa hili kubwa jinga
   
 14. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  You are missing the point
  kagombea urais 1995 kashindwa

  kagombea tena 2005 kashindwa

  sasa bado anataka kugomea urais

  sasa kama kweli angekuwa na akili na alitaka awe taken serious then ilitakiwa akae pembeni awapishe wenzie.

  Nimesema angetuletea info jinsi DFID TANZANIA wanavyochochoea ubadhirifu na ufisadi ningemwona wa maana lakini Lupumba comes across as another useless professors tulionao ambaye at most he is good for nothing really
   
 15. M

  Masatu JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kumbe hili lijamaa ni mashoto...
   
 16. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  kama CLINON...ckwani clinon naye mashoto au?
   
 17. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Anhaa, kumbe mlikuwa mnaongelea criticisms za jumla jumla mlizonazo dhidi ya Lipumba. Oh yeah, hata mimi nina misgivings zangu dhidi yake, haswa hilo la kuwa mgombea wa kudumu wa CUF. Nilifikiri mnaongelea hili lililoletwa kwenye mada hapa, ambalo naona Lipumba yuko picture perfectly correct:

  Kikwete kasamehe wahusika wa alicholionyesha Bunge kuwa ni ufisadi. IMF ikampongeza Kikwete kwa jinsi alivyo handle skandali la EPA. Profesa Lipumba akasema IMF wanachochea ufisadi kwa kupigia debe hatua ambazo hazitoshi. Exquisite point.

  Nyinyi mnasema Profesa kachoka kufikiri. Kumbe mnaongelea yenu mengine. Yes, to the extent that you were just venting unrelated frustrations then I missed the point, you are right.
   
  Last edited: Oct 7, 2008
 18. M

  Masatu JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  U have no clue on what ur talking abt.. yes! its shows clearly ur unrelated frustrations!
   
 19. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Ukiona mzungu anakusifia usifikiri wewe ni mahiri sana bali ndondocha lake, usishangae imf kumsifia kikwete kuchukua hatua dhidi ya epa, huu ndo undondocha wenyewe,ingekuwa ulaya au marekani watuhumiwa wa epa wangepewa muda kurudisha pesa walizoiba?
   
 20. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Benki ya Dunia yataka mafisadi wabanwe
  Na Ramadhan Semtawa

  BENKI ya Dunia (WB), imesema inatarajia kuona serikali inachukua hatua zaidi za kupambana na ufisadi, ili kujijengea imani zaidi kwa wahisani.

  Kauli hiyo ya WB imekuja wakati wananchi wakitaka hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi, wakiwamo watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT).

  Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi wakati wa maswali kwa waandishi, Mchumi Mkuu wa benki hiyo nchini, Paulo Zacchia, alisema Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika mapambano dhidi ya ufisadi.

  Zacchia alisema BoT na serikali zimekuwa zikichukua hatua za makusudi katika kupambana na ufisadi, lakini mategemeo ni kuona hatua hizo zinaendelea.

  "Tunaridhishwa na hatua kubwa zinazochukuliwa na Benki Kuu na serikali katika kupambana na rushwa, jambo la msingi ni kuendeleza zaidi hatua hizo," alisema Zacchia.

  Akifafanua kuwa hakuna nchi duniani ambayo haina rushwa au ina rushwa kwa kiwango cha asilimia sifuri ndiyo maana benki yao na hata Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) imekuwa zikijikita katika kusaidia mapambano hayo.

  "Hakuna nchi unaweza kusema ina kiwango cha rushwa asilimia sifuri, kila nchi rushwa ipo, kitu kikubwa ni kuzidi kuongeza rasilimali kupambana nayo," alisisitiza.

  Alisema hata Marekani na nchi nyingine duniani bado rushwa ipo, ila jambo la msingi ni kuongeza nguvu katika kupambana na tatizo hilo.

  Alisema kwa kufahamu hilo, ndiyo maana benki ya dunia na washirika wengine wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa kuimarisha utawala bora.

  Mkuu huyo wa Uchumi wa WB, alisema katika kusimamia hilo nchi 14 wafadhili zinazochangia katika Mfuko Mkuu wa Bajeti (GBS), zilikuwa zimesitisha kwa muda misaada yao kwa Tanzania lakini baadaye zikatoa.

  Alisema hatua hiyo inatokana na kuridhishwa na hatua kubwa zinazochukuliwa na serikali katika kupambana na rushwa.

  "Mtaona kwamba wahisani 14 wanaochangia katika GBS walikuwa wamesitisha kwa muda michango yao katika bajeti, lakini waliamua kutoa baada ya kuridhishwa na hatua aza serikali katika kupambana na rushwa," alisisitiza.

  Katika siku za karibuni, Tanzania ilijikuta katika wakati mgumu kuweza kupata misaada ya bajeti kutoka wahisani 14 wanaochangia katika GBS, kutokana na kutakiwa ichukue hatua zaidi dhidi ya mafisadi.

  Hata hivyo, kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali chini ya Rais Jakaya Kikwete, wahisani hao wameanza kumimina misaada yao baada ya kuridhishwa.
   
Loading...