Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Kitila,
Is it due to skepticism that Watanzania have with CUF and Maalim Sefu? is he in the right opposition party?
Naona CCM itatawala daima. Katika hali ya mazingira ya Tanzania, Lipumba tayari anaonekana alijaribu na kushindwa.
Hivi ni uchaguzi wa gani uliotoa nafasi kwa vyama vya upinzani kushinda?
Kama vyama vya upinzani havipewi nafasi za kikatiba kushinda uchaguzi basi Lipumba, Mrema, Mbowe na wengine wanaweza kuendelea kugombea na wala nafasi zao zisifananishwe na vyama vya upinzani vya Korea au Marekani ambavyo vinapigania katika mazingira ya kidemokrasia.
Please yaaani nimechoka mweeee! lets do away with all, I mean ondoa wotee kuanzia upinzani mpaka CCM toa wotee tuanze upya, I am sick, ishu ya wazee na vijana is dead, tumegundua wote ni bure, eti kina mama ndio even worse hawawezi kutusaidia, sasa tumebakia kujaribu only one idea nayo ni to do away na wote tuazne upya!
Masatu now is good that you back your sense . Mfumo wa demokrasia ni mbovu una unawapa CCM kushinda kila mara na kama utabadilishwa kama CCM hawatakataa basi ujue CCM yako inapigwa bao kweupee. Wizi na matumizi mabaya ya State security , forces etc
Kwa namna unavyoeleza inaonekana una siasa za ubaguzi,kama Jakaya akianza kujenga kwao na kuimarisha huko alikotoka ,tayari watu dizaini zenu mtazuka na kumvalia njuga,hivi tunapoandika kuna hisia za kuigawa Nchi kwa mfumo wa Mawaziri jambo ambalo si jema ni katika harufu ya ubaguzi kwa madai kwa nini mawaziri wengi wanatoka mkoa fulani,hivi Tanzania ina mikoa mingapi sasa Raisi wa Nchi akiamua kila mkoa utoe waziri huoni kama mtakuja na msemo wa Baraza lake ni kubwa na linafisdi fedha za walala hoi.ameshindwa kuwasaidia CUF kushinda hata kiti kimoja kule anakotoka (Tabora).
ameshindwa kuzifanya baadhi ya hizo sera zifanye kazi kwenye kijiji chake au wilaya yake.
Kuna watu hawawi na nafasi ya kufanya hayo wanayokusudia kufanya lakini kuna watu wengine wako kwenye positions za kupeleka changes wanakotoka lakini miaka na miaka hakuna walichofanya na sasa wanajifanya wanaweza kuongoza nchi?
Kwa CUF kushindwa kupata hata jimbo moja Tabora na failure kubwa sana kwa Lipumba.
Kwa namna unavyoeleza inaonekana una siasa za ubaguzi,kama Jakaya akianza kujenga kwao na kuimarisha huko alikotoka ,tayari watu dizaini zenu mtazuka na kumvalia njuga,hivi tunapoandika kuna hisia za kuigawa Nchi kwa mfumo wa Mawaziri jambo ambalo si jema ni katika harufu ya ubaguzi kwa madai kwa nini mawaziri wengi wanatoka mkoa fulani,hivi Tanzania ina mikoa mingapi sasa Raisi wa Nchi akiamua kila mkoa utoe waziri huoni kama mtakuja na msemo wa Baraza lake ni kubwa na linafisdi fedha za walala hoi.
Kama nilivyosema kwa siasa zilizopo chini ya Chaguzi zinazosimamiwa na CCM ambapo wagombea wengi wamesikika wakisema hata kura yao na ya mke wake hawakuziona ,hapo ujue kuna tatizo kubwa katika uchaguzi mzima,sioni ajabu kwa Lipumba au mgombea mwengine yeyote kukosa jimbo ,hizi ni tactic za kumdidimiza mgombea kwamba hata kule atokako hakubaliki ni major crime ambayo inafanywa na Utawala wa CCM.
Na hata kufanya mabadiliko kwa ile sehemu inayowahusu upinzani pia nayo hufanyiwa njama kuna mifano mingi ambayo upinzani umekosa kibali kufanya kama kujenga zahanati na pia kuna vituo vya polisi ambavyo vilijengwa na bada ya kumaliza havikupewa wanausalama hao kuvitumia ,sababu tu vipo katika maeneo waliyoyadhibiti wapinzani ,bado hiyo haijawa hoja ya kuwapima viongozi kutoka katika kambi ya upinzani,natumai ulisikia kisa cha Lwakatale kilicho tokea uwanja wa ndege cha kuvuliwa nguo na polisi ili kumdhalilisha na yako mambo mengi.Kesi za Mrema ambazo hazishi,kwa kweli mimi naamini Lipumba ni tishio kwa uongozi wa CCM ,hivyo kumzima asionekane ni jambo la lazima,hapa inatakiwa mtu ambae yupo tayari kuiona Tanzania ikiingia katika vita vya wananchi na vyombo vya serikali lakini Lipumba naona hakuwa tayari kwa maana yeye ni msomi anaefahamu hasara ya uamuzi wa mapambano.Kumbukumbu zinaonyesha watu wapo tayari ila wanafuata na kusikiliza maneno ya busara kutoka kwa viongozi walio makini.Zanzibar walijaribu na hadi hii leo hawajulikani wangapi walikufa na wangapi walikuwa raped mbali ya waliovunjika na kubaki na masalio ya risasi ndani ya miili yao.
Mwiba,
Nafikiri unakurupuka na kushindwa kuelewa hoja yangu. Charity starts at home haina maana mtu atumie madaraka yake vibaya na kutengeneza sehemu moja kwa gharama ya sehemu nyingine.
Kiongozi bora haanguki toka angani na badala yake matendo yake kwenye jamii anayotoka huwa kielelezo tosha. JK alikuwa mbunge wa Bagamoyo, je kuna maendeleo gani aliyaleta kwenye hilo jimbo lake? Kama kwa miaka 15 hakuna cha maana alichofanya, unategemea kwenye taifa atafanya nini?
Hivyo hivyo kwa Prof. Lipumba, nilikuwa nategema kati ya sehemu ambako ingelikuwa rahisi mafanikio yake kuonekana ni kule Tabora lakini bahati mbaya inaelekea hayo mafaniko hayapo.
Tumeona jinsi Mrema alivyoandamwa na serikali ya CCM, lakini kazi alizowahi kufanya huko nyuma zinajulikana na ndio maana aliweza kushinda wilaya ya Temeke na pia kule Kilimanjaro aliweza kuwawezesha NCCR na TLP kushinda viti. Pia tunamwona Hamad, pamoja na mikiki miki ya serikali lakini kule Pemba hata wafanye nini, CUF watashinda tu.
.Sina ubaguzi wowote na wale wote wanaonijua wanajua hilo fika ila ni mtetezi wa dhana ya watu kujaribu kurudi kwao kuendeleza wilaya zao wapatapo nafasi. Kule wilayani kunahitahi role models
ambao wanaweza kuamsha ari ya maendeleo kwa vijana. Ni mpinzani wa hii dhana mpya ya wasomi kujichimbia Dar Es Salaam na kusahau walikotoka. Kama huo ni ubaguzi, basi una haki ya kuniita mbaguzi
kumlinganisha profesa Lipumba na Mrema ni comparison isiyo sawa kabisa, Mrema ashakaa katika nafasi ya kutoa maamuzi na kuyasimamia, keshakuwa naibu waziri Mkuu na pia waziri wa mambo ya ndani, kwa hiyo kwa nafasi zake ni rahisi kufanya kazi za kuwaletea watu wengi maendeleo kwa sababu yupo katika position ya kutekeleza vipaumbele vyake.
Au ukichukulia maalim seif ,yeye ameshakuwa waziri kiongozi, nafasi inayompa nafasi ya kudictate sera kwa mujibu wa cheo chake.
Sasa kwa mtu kama profesa Lipumba, unategemea yeye kama Mwenyekiti tu wa CUF atafanya nini kubwa kwa wananchi hao unaowasema wa Tabora, wakati mtu hayuko katika nafasi ya kufanya maamuzi ya kisera?(bimaana hana rungu).
au kwa kuwa ni profesa basi aende kuitisha mikutano ya hadhara atoe lecture juu ya uchumi na umasikini?.laiti huko tabora kungekuwa hata na chuo kikuu basi ungesema profesa akafundishe huko chuoni ili kusaidia mkoa wake, lakini otherwise unataka profesa akafanye nini haswaaa huko tabora.
kikubwa anachoweza kukifanya profesa Lipumba ni kuikosoa serikali,kwa hiyo ukitaka kumpima profesa kipimo kizuri ni je ana/ameikosoa /ameishauri serikali barabara?
.
Mtu kama profesa Lipumba au ambao wapo katika upinzani kwa sasa kazi kubwa wanayoweza kuifanya katika Tanzania ni kufanya kila namna kuleta mabadiliko ya uongozi katika Tanzania, na wala si kurudi walipozaliwa wakajichimbie huko ama sijui wakasaidie walipotoka, isitoshe watasaidiaje? wakati hawapo katika nafasi ya kufanya maamuzi ya kisera?
Tz ninavyofikiri ina matatiozo-
watanzania wenyewe -yani watanzania hawapendi maendeleo kwanini
moja hakuna mtanzania hata mmoja aliye tayari kuchangia mtoto wa mtanzania mwenzie aende shule wapo tayari kumchangia akapige ulabu au kufanya bongee la harusiiiiii yani TUPOWANAFIKI ILE MBAYA.
Na bado mzazi akijinyima akakusomesha wao bado inawakela watatafuta kila njia ujambazi ama vibuyu ili wakuangamize na hii utakuta watu wengi wenye fedha ama viongozi kwao ni choka mbaya wanaogopa kurudi kwani ni siri.
Ukizamia mjini na wa huko hawachelewi kuanza kuhoji amepata wapi fedha mshahara wake elfu sitini INDEED TANZANIANS LIKE POVERTY .
ukiwa masikini unakula mlo mmoja wa kulumangia they have good news to publish and sometimes they used to go deep down kwa kuombea ukose hata huo mlo mmoja.
If u have something it is owful news for them going here and there barking obvious ur Fisadi whereby the best soln for them is to drop u down and zap all of urs so that they can gather good news.
Na zaidi watanzania hatukubali makosa ila nikutafuta mchawi ambaye ndiye unafikiri ni source of ur problem kumbe source of ur problem ni wewe mwenyewe.Watanzania hawafanyi kazi ila tunategemea santa clous afanye mambo yake.
Watu wa ugaibuni hebu niambieni mnalala masaa mangapi??nje huwa kunakuchagua kazi?? matako ya vijibibi si tunaviosha?? kuosha vyobo je? na kuchuma stawbell mgongo vipi unaupindisha karibu ukatike au vipi? lakini mtu huyohuyo akija bongo hataki kwenda kigoma .
Matatizo yetu si Lipumba wala Mbowe wala JK ila atakayeweza kubadili mentality yetu ndiye atakuwa mshindi
tuna matatizo amabyo yameanzia chini kiasi kwamba yanaharibu mfumo mzima na inafika mahala fulani mtanzania akikuhangaisha anajiona yeye ndi yeye ->njoo kesho njoo kesho njoo kesho sio ofisini tu hadi kwa mtu binafsi umeenda kukopa fedha upeleke mgonjwa hospitali hadi mgonjwa ISRAEL anamwita ,huyo huyo ndiye wakwanza kuangua bonge la kilio na kutoa rambi rambi fedha ambayo ni zaidi mara nyingi ya ile uliyotaka kukopa.
UNAFIKI UNAFIKI UNAFIKI UNAFIKI UNAFIKI KWENDA MBELE
Tuna matatizo makubwa mno
tujiangilieni kwanza harafu tukimaliza ndiyo tumfuate JK
Aminia mkuu
Wachilia Lipumba, Mrema na wengine wengi, hata ashuke malaika upinzani hashindi Tz. Wasimamizi wa uchaguzi wanaamini kuwa wapo pale kwa kujuana na sio uwezo (elimu na ufanisi) wao katika kazi, so ni lazima walipe fadhila kwa aliyewachagua ili wakae hapo milele. Ikiwa kama wataamini wapo pale kwa uwezo wao na sio kujuana amini mabadiliko yatakuja tu Tz.
Tuangalie Kenya mazee, kwanini Tz isiwezekane?
A day will come