Lipumba na Tanzania

japokuwa pia msimamo wangu hakuna chama cha upinzani nnachokiona imara kwa sasa zaidi ya CCM

Sawa, inawezekana ni kweli. Lakini je kwa nini na wewe usishiriki kuimarisha huo upinzani? Au wewe unataka kufaidi matunda tu? Vipi ukiwa part of both a struggle and a success?
 
Naungana na wewe Kitila,watz ni waoga na wanafiki wengi wakigombea wanajipendekeza kwa ccm hata kama hisia zao ziko tofauti.Halafu kingine wanapenda kubeza watu ambao wamejitoa mhanga badala ya kuwapa support.
 
Hiyo ni kutafuta mchawi wa kushindwa kwa upinzani.

Lakima ukubali, Malawi upinzani walikuwa na matatizo hayo hayo, Zambia walikuwa nayo, Kenya walikuwa nayo nk.

You are right. Tunapaswa kupambana kwenye mfumo huu huu uliopo. Tukisubiri ubadilishwe, tutasubiri sana. CCM hawataubadilisha mfumo uliopo kwa sababu unawasaidia. Moi, Kamuzu Banda, Kaunda n.k. walishindwa kwa mifumo yao hiyohiyo. Tena mazingira ya upinzani TZ sio magumu kama yalivyowahi kuwa katika nchi zingine kama Kenya, Zambia na Malawi. Mfano mwingine, hakuna mazingira magumu ya upinzania kama Zimbabwe, lakini tazama MDC wanasonga mbele na wana viti vingi bungeni pengine mara 20 yetu. Kinachokosekana TZ ni watu jasiri. Watu wengi Tanzania wenye sifa za kuingia siasa wana hofu na woga wa ajabu sana na hawataki kuchukua risk hata kidogo; wanataka kushiriki mafanikio lakini sio mapambano. Hawa ndio maadui wakubwa wa maendeleo ya demokrasia yetu. Hawa ni pamoja na sisi tuliosoma soma kidogo na viongozi wa dini. Matokeo yake kuna wanasiasa wachache ndani ya upinzani wenye uwezo na ambao unaweza kushawishika kuwapa serikali. Ukihesabu watu mahiri ambao wanastahili kuunda seikali katika chama chochote cha upinzani hawatafika 10. Hivyo watu wakiangalia hivi hawa jamaa tukiwapa nchi kesho nani atakuwa waziri mkuu, nani atakuwa waziri wa fedha, hawaoni! Kwa maneno mengine sisi wapinzani hatujaanza kutabirika, na hulka ya binadamu hataki kubahatisha, anataka awe na uhakika kwa kiwango fulani kwamba kesho mambo yatakuwa hivi. This is our biggest weakness more so than ideological and policy issues.

Lakini sasa tufanyeje, kwa sababu watanzania walio makini ndio hao wamejawa na woga na hofu, hawataki ku-risk, wanataka tu kuvuna lakini hawataki kushiriki kupanda. Tena wengi tu wapo hapa ndani ya JF. Watu wengi wanaongea hapa kama vile kuna watu fulani wenye wajibu wa kuimarisha upinzani na wao kazi yao ni kuangalia tu. Sasa kama watu mnajifanya nyie ni washangiliaji na wakosoaji tu mmekaa pembeni kama vile mna-watch football macth hamtaki kuwa wachezaji na mmewaachia hao wachezaji ambao mnawaona hawafai, kama sio undamila kuwili ni nini hasa? Lazima tubadilike kama tunataka kuona ushindani wa kisiasa unashamiri nchini, hii ni pamoja na kushiriki katika hivyo vyama. CHADEMA wameshatoa ratiba ya uchaguzi, ni wakati sasa wa nyie kuchangamka na kuhakikisha mnaingia katika nafasi muhimu za kufanya maamuzi ndani ya CHADEMA. Kama hamtashiriki na mkawaachia wengine walioamua kujitoa, ifikapo 2009 tufunge midomo, tusije sema oohh, chadema chama cha wachaga au cha kigoma kwa akina Zitto. Kumbe wafenyeje kama wao pekee ndio wamejitokeza?

Huko tunakokutamani Kenya na kwingeneko-watu wamejitoa hasa sio mchezo; wamejitoa ili kuhakikisha wanashimirisha siasa za ushindani. Watu wameacha kazi za maana sana ili kufanya kazi ya upinzani. Manung'uniko, malalamiko na kejeli pekee kwa upinzani hazitabadilisha hali iliyopo; kinachotakiwa ni sisi kuchukua hatua. Kama tumeshaiona CHADEMA ndicho chama chenye mwelekeo, badi twendeni tujiunge huku na tugombee nafasi za uongozi. Watu tunasema wangekuwepo akina Zitto 10, sasa watatoka wapi kama sisi hatujiungi nao? Wishful thinking itabaki hivyo siku zote, it is actions that will make a difference!
 
Duu,
Kitila hapa naona umeamua umkome nyani humu humu humu JF,
Tumekusikia mkuu!, hii ndo wenzetu wa Japani husema ''I tell you ze trusi only''
 
nasubiri watu waje wamsakame Prof.Lipumba manake na yeye ameoa mwanamke wa Kichaga.
 
nasubiri watu waje wamsakame Prof.Lipumba manake na yeye ameoa mwanamke wa Kichaga.

inasemwa mkapa kaharibiwa na mkewe wa kichaga na kuifanya ikulu genge la wezi sasa unataka kutoa ujumbe kuwa lipumba na yy ana mchaga tuwe na hadhari au?
 
Mtu wa Pwani said:
inasemwa mkapa kaharibiwa na mkewe wa kichaga na kuifanya ikulu genge la wezi sasa unataka kutoa ujumbe kuwa lipumba na yy ana mchaga tuwe na hadhari au?

Mtu-wa-Pwani,

..nilikuwa nawatumia ujumbe nungwi na samvulachole.

Masatu,

..mbona hii habari ya Prof.Lipumba kuoa iko muda mrefu tu. mwaka 1995 kuna jamaa alikuwa akimlalamikia Lipumba kwa kumvunjia ndoa yake. nadhani CCM walikuwa wanamtumia.

..mzozo wa ndoa ya Prof.Lipumba ilikua na utata wa Udini kwasababu huyo mwanamke wa Kichaga ni Mkristo.
 
Kitila,Rev.Kishoka,Mtanzania,Bin Maryam,SiDE

Dr.Festus Limbu aliwahi kugombea kupitia NCCR akashindwa. Uchaguzi uliofuata akahamia CCM na kushinda uchaguzi. Baada ya hapo "akaukwaa" unaibu waziri wa fedha.

kwa kweli sijui tatizo ni nini hapa Tanzania. Lakini nilitegemea chama kilichovuruga nchi kama walivyofanya CCM, kingekuwa na wakati mgumu sana wakati wa Uchaguzi.

Na hicho ndicho tunachopaswa kujadili kama watu wazima. Kwanini anayevulunda-vulunda anashinda tena kwa asilimia zaidi ya 70.

Ukiweka debate hapa ya masuala ya nchi kati ya JK na Lipumba, Lipumba anampiga shule JK. Ukiweka debate ya masuala ya nchi kati ya Mbowe na JK, Mbowe anashinda. Lakini ukiweka Ballot box JK anashinda kwa kuvaa jezi ya YANGA tu.

Wanasema Lipumba yuko CUF na CUF kina-udini. Lakini kwenye uchaguzi kulikuwa na vyama vingi tu. Kama hutaki CUF chagua CHADEMA.

Kama sio tatizo la mazingira ya kikatiba kuwa mabaya basi tulipata uhuru mapema. Na sioni sababu ya kumlaumu Lipumba wakati kasoro zinaonekana katika uchaguzi wa wabunge na madiwani.
 
Ninachojaribu kusema hapa tuna matatizo makubwa ktk mfumo mzima wa demokrasia Tanzania unaopelekea matokeo ya uchaguzi kuto reflect matakwa ya walio wananchi

Masatu,

That is why I m championing for Chadema to be a first party to make reformations and become party of people(Chadema must reform), where the Chadema members from bottom (Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa) will have powers to elect their own candidates and not CC or NEC!

Once this is in place and people see the empowernment they have been trusted by a party, trust me changes will come faster than you can imagine.

Ila, kama vyama vitaendelea kujiendeshana kujiongoza kwa mfumo wa ki-CCM, thee will never be a change!
 
Bin Maryam,

kuna wanaodai Kikwete alikuwa tayari kuhamia upinzani kama CCM wangemuwekea mzengwe. je, alikuwa na imani kwamba atashinda? je, angehamia NCCR au CHADEMA angeshinda?

hivi wapinzani wakifanya kampeni ya kuwapumbaza Watanzania kama alivyofanya Kikwete wanaweza kushinda uchaguzi? Kwa kweli kampeni za Uraisi zilikuwa formalities tu, lakini Kikwete alishashinda.

watanzania tunapaswa tujiandae kwa kampeni ndefu ya kuiondoa CCM. Mfumo mzima wa uongozi CCM umeoza, hata ukiweka mtu msafi awaongoze naye atavunda tu.
 
Bin Maryam,

kuna wanaodai Kikwete alikuwa tayari kuhamia upinzani kama CCM wangemuwekea mzengwe. je, alikuwa na imani kwamba atashinda? je, angehamia NCCR au CHADEMA angeshinda?

hivi wapinzani wakifanya kampeni ya kuwapumbaza Watanzania kama alivyofanya Kikwete wanaweza kushinda uchaguzi? Kwa kweli kampeni za Uraisi zilikuwa formalities tu, lakini Kikwete alishashinda.

watanzania tunapaswa tujiandae kwa kampeni ndefu ya kuiondoa CCM. Mfumo mzima wa uongozi CCM umeoza, hata ukiweka mtu msafi awaongoze naye atavunda tu.


Kwa siasa za Afrika mashariki hicho kitu kinawezekana. Chama cha Kibaki kilikuwa hakina mazingira yoyote ya kushinga mpaka pale Moi alipompendekeza mtoto wa Kenyatta kuwa mgombea na kuwaudhi wakina Saitoi.

Inaonekana wapinzani au watanzania kwa ujumla wanasubiri high profile kutoka CCM kuhamia vyama vyao kama vile alivyofanya Mrema.

Nikiwa shule kwenye somo la siasa nilisoma sana mambo ya chama cha mapinduzi kuliko haki zangu za kikatiba. Na hilo ndio tatizo la watanzania wengi. Tunaelewa sana siasa lakini hatuelewi haki zetu zinazotakiwa kuelezwa na katiba.

Mtanzania awe na haki ya kugombea nafasi za uongozi bila kujali affliation yake na vyama vya kisiasa. Tukianzia hapa mabadiliko yatatokea tu. Wagombea huru waruhusiwe na hawa ndio watakaoleta changamoto ndani ya CCM.
 
Lipumba is very smart, just like John Kerry or Al Gore, however average Joe of Tanzana can not relate to him just like how Americans failed to relate to Gore or Kerry and elected a clown!
 
Kitila kaweka mambo WAZI kwa mtu mwenye AKILI anatakiwa aweke ktk ROAD MAP yake juu ya mapinduzi ya DEMOKRASIA nchini...Hakuna Uchaguzi wa Democracy uliofanyika hadi sasa...

Hoja ya kuwa Kongozi XYZ hafai eti amegombea zaidi ya mara X hafai ni hoja MFU. ILI uchaguzi uwe HURU basi TUME ya UCHAGUZi lazima IWE HURU...kwa utaratibu uliopo wao CCM wataendelea kushinda... Haiwezekana wewe una-UHAKIKA umepiga kura yako kwa MTU XYZ, lkn matokeo yakija hata kura yako HAIPO..unajiuliza haya Mazingaombwe au vipi?

ELIMU ya URAIA Tanzania BARA kubwa si KUBWA, Zbar wenzetu wametuzidi, uelewa wao ni mkubwa. na ndio maana CCM hawataki wanaogopa znz kuwa chini ya chama cha Upinzani. the so called wabunge wa bara ni Kwanini CUF wanakosa...TUME ya UCHAGUZI inajua inachofanya ku-pika matokea...

KILA LENYE MWANZO LINA MWISHO...DHULMA zinazofanyika zina mwisho pale wananchi watakapo sema sasa DHULMA BASI CCM na matawi yake vitakaa kando...
 
Back
Top Bottom