Lipumba na Tanzania

Naona CCM itatawala daima. Katika hali ya mazingira ya Tanzania, Lipumba tayari anaonekana alijaribu na kushindwa.

Hivi ni uchaguzi wa gani uliotoa nafasi kwa vyama vya upinzani kushinda?

Kama vyama vya upinzani havipewi nafasi za kikatiba kushinda uchaguzi basi Lipumba, Mrema, Mbowe na wengine wanaweza kuendelea kugombea na wala nafasi zao zisifananishwe na vyama vya upinzani vya Korea au Marekani ambavyo vinapigania katika mazingira ya kidemokrasia.
 
Kitila,

It speaks highly of you as "Mpinzani" if you speak credible on Lipumba than Mwiba and the fact that you are Chadema!

Now if that is the case that he is better than Makunyanzi or Chekacheka, then why he continues to fail to get a solidarity support from him compadres (Mbowe, Cheyo, Mrema, Makaidi)?

Is it due to skepticism that Watanzania have with CUF and Maalim Sefu? is he in the right opposition party?

I do not think Watanzania and Mazoea kulishwa ubwabwa wa CCM is the case here! Maana even his party can barely get seats in Mainland!
 
Kitila,

Is it due to skepticism that Watanzania have with CUF and Maalim Sefu? is he in the right opposition party?

This is a different issue all together. All I am saying the guy has a very good message and he knows how to deliver it well. Now whether he is using the right boat to take him where he wants to go is another different issue that I cannot comment now.
 
Mimi naona Prof. Lipumba ni makini sana kwenye sera na huenda hata akawa rais mzuri kama angepata. Lakini kuna kitu kimoja ambacho kinanishangaza kuhusu Lipumba, pamoja na umaarufu wake wote, ameshindwa kuwasaidia CUF kushinda hata kiti kimoja kule anakotoka (Tabora). Kwa mwanasiasa yoyote, charity starts at home.

Ninashindwa kupata jibu lakini huenda pamoja na usomi wote, ameshindwa kuzifanya baadhi ya hizo sera zifanye kazi kwenye kijiji chake au wilaya yake.

Mimi huwa napenda kuangalia zaidi huyu binadamu amefanya nini huko nyuma ambacho kinalingana na anayoahidi kufanya? Kuna watu
hawawi na nafasi ya kufanya hayo wanayokusudia kufanya lakini kuna watu wengine wako kwenye positions za kupeleka changes wanakotoka lakini miaka na miaka hakuna walichofanya na sasa wanajifanya wanaweza kuongoza nchi?

Ndio makosa hayo hayo tuliyofanya kwa JK, kule anakotoka kashindwa kabisa kutekeleza hiyo kasi mpya, tukamwamini eti ataweza kuwa na kasi mpya kwa Tanzania nzima?

Kwa CUF kushindwa kupata hata jimbo moja Tabora na failure kubwa sana kwa Lipumba.
 
Naona CCM itatawala daima. Katika hali ya mazingira ya Tanzania, Lipumba tayari anaonekana alijaribu na kushindwa.

Hivi ni uchaguzi wa gani uliotoa nafasi kwa vyama vya upinzani kushinda?

Kama vyama vya upinzani havipewi nafasi za kikatiba kushinda uchaguzi basi Lipumba, Mrema, Mbowe na wengine wanaweza kuendelea kugombea na wala nafasi zao zisifananishwe na vyama vya upinzani vya Korea au Marekani ambavyo vinapigania katika mazingira ya kidemokrasia.

Aminia mkuu
Wachilia Lipumba, Mrema na wengine wengi, hata ashuke malaika upinzani hashindi Tz. Wasimamizi wa uchaguzi wanaamini kuwa wapo pale kwa kujuana na sio uwezo (elimu na ufanisi) wao katika kazi, so ni lazima walipe fadhila kwa aliyewachagua ili wakae hapo milele. Ikiwa kama wataamini wapo pale kwa uwezo wao na sio kujuana amini mabadiliko yatakuja tu Tz.
Tuangalie Kenya mazee, kwanini Tz isiwezekane?

A day will come
 
Mtanzania and Rev Kishoka
Nakubaliana na nyinyi kwa asilimia mia moja. Lipumba anaujua uchumi, probably he is one of the best economist in the country, lakini jamaa ameshindwa kuuzika ndani ya nchi. This is simple as 1,2,3, upinzani need to change their tactics kuhusu uchaguaji wa rahis wa nchi, i believe there is someone in Upinzani who will convince people about his/her agenda.

Kunga'ng'ana na kwamba lipumba ndio the only choice watanzania needs does not make any sense at all.CUF wameshajaribu kwa miaka na miaka kuwaweka Malim Seif na Lipumba on the same spot.What does it implied? This two are dictators, walafi and so fourth. Upinzani need to create easy ladder toward leadership, and this will be only way ya kupata best leader. Kushikilia ya kwamba Mrema, Cheyo, Lipumba and Maalim ndio only options, then give us the brake.
 
Kitila,Rev.Kishoka,Mtanzania,Bin Maryam,SiDE

Dr.Festus Limbu aliwahi kugombea kupitia NCCR akashindwa. Uchaguzi uliofuata akahamia CCM na kushinda uchaguzi. Baada ya hapo "akaukwaa" unaibu waziri wa fedha.

kwa kweli sijui tatizo ni nini hapa Tanzania. Lakini nilitegemea chama kilichovuruga nchi kama walivyofanya CCM, kingekuwa na wakati mgumu sana wakati wa Uchaguzi.
 
Please yaaani nimechoka mweeee! lets do away with all, I mean ondoa wotee kuanzia upinzani mpaka CCM toa wotee tuanze upya, I am sick, ishu ya wazee na vijana is dead, tumegundua wote ni bure, eti kina mama ndio even worse hawawezi kutusaidia, sasa tumebakia kujaribu only one idea nayo ni to do away na wote tuazne upya!
 
Mkuu tutawatoa wapi hao wapya, inabidi sasa watu tujitupe huku mia kwa mia. Vinginevyo watabaki haohao, hakuna jinsi. Kwa mfano watu wanaomlaumu Lipumba kwa kugombea mara nyingi wanamuonea au hawajui hali halisi. Nakumbuka 2000 Lipumba alikuwa anataka kurudi kufundisha mlimani na alikuwa si tu kwamba hataki kugombea urais, bali hata uenyekiti wa CUF alikuwa aachie, lakini amini usiamini hakuna aliyejitokeza ndipo hapo ilibidi wazee wa busara ndani ya CUF wamuombe aendelee kuwa mwenyekiti na agombee urais. Hivyohivyo mwaka 2005. Sasa nyie mnaona bora chama kikose mgombea kuliko huyo Lipumba kugombea? Tunasahahu kwamba kwa siasa za Tanzania Lipumba is a very special case. Wanasiasa wengi Tanzania wapo kwenye siasa ama kwa kuwa hawana kitu kingine cha kufanya (mostly in opposition) au wamegundua siasa ni mtaji wa kujipatia utajiri au kichaka cha kuficha madhambi yao (mostly in CCM). Wachache wamekwepa haya makundi mawili mfano wa wazi ukiwa ni Lipumba na Mbowe. Huyu ni mtu aliyejitoa sana kwa ajili ya nchi yake na demokrasia kwa ujumla, lakini anapigwa madongo. Hili ni tatizo tulilo nalo la kubeza watu wanaojitoa na kutukuza wahuni wa kisiasa.

Sasa ushauri wangu ni kwamba kama kweli mnataka hawa akina Lipumba wapumzike, wahamasisheni watu wengine au nyie wenyewe jitokezeni kuchukua nafasi zao. Vinginevyo haitakuwa busara kwa Lipumba kuacha vacuumu ya uongozi katika chama chake kwa kuogopa kuonekana anagombea mara nyingi, huo ni utoto. Kama hamuwezi kujitokeza kujiunga na upinzani na hatimaye kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kama hamuwezi kuwashawishi watu wengine kujitokeza basi na tunyamaze tu, tusiwakatisha tamaa watu walioamua kujitoa kwa kiwango cha akina Lipumba.
 
kuamua kuacha mambo yako ambayo yanakupatia riziki na kuamua kujitoa muhanga si shughuli nyepesi.

siasa za Tanzania zinajulikana ukitaka upate wakati mugumu ingia kwenye siasa na hasa za upinzani ndio utaiona dunia.

kwa hiyo nnaamini kuwa wengi wapo ila kujitokeza ni shughuli hawana ujasiri wanaangalia consequence, na baadhi ya wakati kuna ukweli.

wako wengi waliotaabika na maisha yao kudhorota na kupelekea kupata mradhi mbali mbali hadi kufikia kufa.

kule zenji kuna bwana mmoja AlHaji Pandu anaemjua anaweza akakueleza hali yake ilivyo maskini mzee wa watu, alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali na pia akawa waziri wa sheria, alipoingia upinzani hali yake ikoje.

sasa mfano mkubwa ukitaka kuingia utaoneshwa wengi tu na yaliyowakuta mpaka utaogopa, usione tunazungumza nyuma ya kioo hapa lkn tukiingia ulingoni ni shughuli.

ila wanapoamua wachache tuwapongeze na wengine wajitokeze tuwashajihisheni, mie ningekuwa bongo ningeangalia suala hili.

japokuwa pia msimamo wangu hakuna chama cha upinzani nnachokiona imara kwa sasa zaidi ya CCM
 
Kitila unachotetea ni sahihi kabisa, hii hoja kuwa kwa kuwa alishindwa uchaguzi mara tatu basi awapishe wengine haina mashiko. Lets extends the line of reasoning here, hivi kwa kuwa upinzani ( kuwa ujumla wao) wameshindwa uchaguzi mara 3 na CCM ina maana wasigombee tena?

Halafu huko kunakoitwa "kushindwa" ndugu zangu tutafakari hivi kweli wanashindwa au wanashindishwa? ( i hope u know wat i mean) kwa uchaguzi huu usiokuwa na level field hata huyo Kikwete angegombea say Chadema 2005 na Brazameni akasimama CCM still Brazameni angepata 80%

Ninachojaribu kusema hapa tuna matatizo makubwa ktk mfumo mzima wa demokrasia Tanzania unaopelekea matokeo ya uchaguzi kuto reflect matakwa ya walio wananchi
 
Masatu now is good that you back your sense . Mfumo wa demokrasia ni mbovu una unawapa CCM kushinda kila mara na kama utabadilishwa kama CCM hawatakataa basi ujue CCM yako inapigwa bao kweupee. Wizi na matumizi mabaya ya State security , forces etc
 
Ishakuwa yangu tena... kidogo kidogo tunaharibu mjadala Im out...
 
ameshindwa kuwasaidia CUF kushinda hata kiti kimoja kule anakotoka (Tabora).
ameshindwa kuzifanya baadhi ya hizo sera zifanye kazi kwenye kijiji chake au wilaya yake.
Kuna watu hawawi na nafasi ya kufanya hayo wanayokusudia kufanya lakini kuna watu wengine wako kwenye positions za kupeleka changes wanakotoka lakini miaka na miaka hakuna walichofanya na sasa wanajifanya wanaweza kuongoza nchi?
Kwa CUF kushindwa kupata hata jimbo moja Tabora na failure kubwa sana kwa Lipumba.
Kwa namna unavyoeleza inaonekana una siasa za ubaguzi,kama Jakaya akianza kujenga kwao na kuimarisha huko alikotoka ,tayari watu dizaini zenu mtazuka na kumvalia njuga,hivi tunapoandika kuna hisia za kuigawa Nchi kwa mfumo wa Mawaziri jambo ambalo si jema ni katika harufu ya ubaguzi kwa madai kwa nini mawaziri wengi wanatoka mkoa fulani,hivi Tanzania ina mikoa mingapi sasa Raisi wa Nchi akiamua kila mkoa utoe waziri huoni kama mtakuja na msemo wa Baraza lake ni kubwa na linafisdi fedha za walala hoi.
Kama nilivyosema kwa siasa zilizopo chini ya Chaguzi zinazosimamiwa na CCM ambapo wagombea wengi wamesikika wakisema hata kura yao na ya mke wake hawakuziona ,hapo ujue kuna tatizo kubwa katika uchaguzi mzima,sioni ajabu kwa Lipumba au mgombea mwengine yeyote kukosa jimbo ,hizi ni tactic za kumdidimiza mgombea kwamba hata kule atokako hakubaliki ni major crime ambayo inafanywa na Utawala wa CCM.
Na hata kufanya mabadiliko kwa ile sehemu inayowahusu upinzani pia nayo hufanyiwa njama kuna mifano mingi ambayo upinzani umekosa kibali kufanya kama kujenga zahanati na pia kuna vituo vya polisi ambavyo vilijengwa na bada ya kumaliza havikupewa wanausalama hao kuvitumia ,sababu tu vipo katika maeneo waliyoyadhibiti wapinzani ,bado hiyo haijawa hoja ya kuwapima viongozi kutoka katika kambi ya upinzani,natumai ulisikia kisa cha Lwakatale kilicho tokea uwanja wa ndege cha kuvuliwa nguo na polisi ili kumdhalilisha na yako mambo mengi.Kesi za Mrema ambazo hazishi,kwa kweli mimi naamini Lipumba ni tishio kwa uongozi wa CCM ,hivyo kumzima asionekane ni jambo la lazima,hapa inatakiwa mtu ambae yupo tayari kuiona Tanzania ikiingia katika vita vya wananchi na vyombo vya serikali lakini Lipumba naona hakuwa tayari kwa maana yeye ni msomi anaefahamu hasara ya uamuzi wa mapambano.Kumbukumbu zinaonyesha watu wapo tayari ila wanafuata na kusikiliza maneno ya busara kutoka kwa viongozi walio makini.Zanzibar walijaribu na hadi hii leo hawajulikani wangapi walikufa na wangapi walikuwa raped mbali ya waliovunjika na kubaki na masalio ya risasi ndani ya miili yao.
 
Mwiba,

Nafikiri unakurupuka na kushindwa kuelewa hoja yangu. Charity starts at home haina maana mtu atumie madaraka yake vibaya na kutengeneza sehemu moja kwa gharama ya sehemu nyingine.

Kiongozi bora haanguki toka angani na badala yake matendo yake kwenye jamii anayotoka huwa kielelezo tosha. JK alikuwa mbunge wa Bagamoyo, je kuna maendeleo gani aliyaleta kwenye hilo jimbo lake? Kama kwa miaka 15 hakuna cha maana alichofanya, unategemea kwenye taifa atafanya nini?

Hivyo hivyo kwa Prof. Lipumba, nilikuwa nategema kati ya sehemu ambako ingelikuwa rahisi mafanikio yake kuonekana ni kule Tabora lakini bahati mbaya inaelekea hayo mafaniko hayapo.

Tumeona jinsi Mrema alivyoandamwa na serikali ya CCM, lakini kazi alizowahi kufanya huko nyuma zinajulikana na ndio maana aliweza kushinda wilaya ya Temeke na pia kule Kilimanjaro aliweza kuwawezesha NCCR na TLP kushinda viti. Pia tunamwona Hamad, pamoja na mikiki miki ya serikali lakini kule Pemba hata wafanye nini, CUF watashinda tu.

Sina ubaguzi wowote na wale wote wanaonijua wanajua hilo fika ila ni mtetezi wa dhana ya watu kujaribu kurudi kwao kuendeleza wilaya zao wapatapo nafasi. Kule wilayani kunahitahi role models
ambao wanaweza kuamsha ari ya maendeleo kwa vijana. Ni mpinzani wa hii dhana mpya ya wasomi kujichimbia Dar Es Salaam na kusahau walikotoka. Kama huo ni ubaguzi, basi una haki ya kuniita mbaguzi.
 
Tz ninavyofikiri ina matatiozo-
watanzania wenyewe -yani watanzania hawapendi maendeleo kwanini
moja hakuna mtanzania hata mmoja aliye tayari kuchangia mtoto wa mtanzania mwenzie aende shule wapo tayari kumchangia akapige ulabu au kufanya bongee la harusiiiiii yani TUPOWANAFIKI ILE MBAYA.
Na bado mzazi akijinyima akakusomesha wao bado inawakela watatafuta kila njia ujambazi ama vibuyu ili wakuangamize na hii utakuta watu wengi wenye fedha ama viongozi kwao ni choka mbaya wanaogopa kurudi kwani ni siri.

Ukizamia mjini na wa huko hawachelewi kuanza kuhoji amepata wapi fedha mshahara wake elfu sitini INDEED TANZANIANS LIKE POVERTY .
ukiwa masikini unakula mlo mmoja wa kulumangia they have good news to publish and sometimes they used to go deep down kwa kuombea ukose hata huo mlo mmoja.

If u have something it is owful news for them going here and there barking obvious ur Fisadi whereby the best soln for them is to drop u down and zap all of urs so that they can gather good news.

Na zaidi watanzania hatukubali makosa ila nikutafuta mchawi ambaye ndiye unafikiri ni source of ur problem kumbe source of ur problem ni wewe mwenyewe.Watanzania hawafanyi kazi ila tunategemea santa clous afanye mambo yake.

Watu wa ugaibuni hebu niambieni mnalala masaa mangapi??nje huwa kunakuchagua kazi?? matako ya vijibibi si tunaviosha?? kuosha vyobo je? na kuchuma stawbell mgongo vipi unaupindisha karibu ukatike au vipi? lakini mtu huyohuyo akija bongo hataki kwenda kigoma .
Matatizo yetu si Lipumba wala Mbowe wala JK ila atakayeweza kubadili mentality yetu ndiye atakuwa mshindi

tuna matatizo amabyo yameanzia chini kiasi kwamba yanaharibu mfumo mzima na inafika mahala fulani mtanzania akikuhangaisha anajiona yeye ndi yeye ->njoo kesho njoo kesho njoo kesho sio ofisini tu hadi kwa mtu binafsi umeenda kukopa fedha upeleke mgonjwa hospitali hadi mgonjwa ISRAEL anamwita ,huyo huyo ndiye wakwanza kuangua bonge la kilio na kutoa rambi rambi fedha ambayo ni zaidi mara nyingi ya ile uliyotaka kukopa.
UNAFIKI UNAFIKI UNAFIKI UNAFIKI UNAFIKI KWENDA MBELE
Tuna matatizo makubwa mno
tujiangilieni kwanza harafu tukimaliza ndiyo tumfuate JK
 
Mwiba,

Nafikiri unakurupuka na kushindwa kuelewa hoja yangu. Charity starts at home haina maana mtu atumie madaraka yake vibaya na kutengeneza sehemu moja kwa gharama ya sehemu nyingine.

Kiongozi bora haanguki toka angani na badala yake matendo yake kwenye jamii anayotoka huwa kielelezo tosha. JK alikuwa mbunge wa Bagamoyo, je kuna maendeleo gani aliyaleta kwenye hilo jimbo lake? Kama kwa miaka 15 hakuna cha maana alichofanya, unategemea kwenye taifa atafanya nini?

Hivyo hivyo kwa Prof. Lipumba, nilikuwa nategema kati ya sehemu ambako ingelikuwa rahisi mafanikio yake kuonekana ni kule Tabora lakini bahati mbaya inaelekea hayo mafaniko hayapo.

Tumeona jinsi Mrema alivyoandamwa na serikali ya CCM, lakini kazi alizowahi kufanya huko nyuma zinajulikana na ndio maana aliweza kushinda wilaya ya Temeke na pia kule Kilimanjaro aliweza kuwawezesha NCCR na TLP kushinda viti. Pia tunamwona Hamad, pamoja na mikiki miki ya serikali lakini kule Pemba hata wafanye nini, CUF watashinda tu.

kumlinganisha profesa Lipumba na Mrema ni comparison isiyo sawa kabisa, Mrema ashakaa katika nafasi ya kutoa maamuzi na kuyasimamia, keshakuwa naibu waziri Mkuu na pia waziri wa mambo ya ndani, kwa hiyo kwa nafasi zake ni rahisi kufanya kazi za kuwaletea watu wengi maendeleo kwa sababu yupo katika position ya kutekeleza vipaumbele vyake.
Au ukichukulia maalim seif ,yeye ameshakuwa waziri kiongozi, nafasi inayompa nafasi ya kudictate sera kwa mujibu wa cheo chake.
Sasa kwa mtu kama profesa Lipumba, unategemea yeye kama Mwenyekiti tu wa CUF atafanya nini kubwa kwa wananchi hao unaowasema wa Tabora, wakati mtu hayuko katika nafasi ya kufanya maamuzi ya kisera?(bimaana hana rungu).
au kwa kuwa ni profesa basi aende kuitisha mikutano ya hadhara atoe lecture juu ya uchumi na umasikini?.laiti huko tabora kungekuwa hata na chuo kikuu basi ungesema profesa akafundishe huko chuoni ili kusaidia mkoa wake, lakini otherwise unataka profesa akafanye nini haswaaa huko tabora.

kikubwa anachoweza kukifanya profesa Lipumba ni kuikosoa serikali,kwa hiyo ukitaka kumpima profesa kipimo kizuri ni je ana/ameikosoa /ameishauri serikali barabara?

Sina ubaguzi wowote na wale wote wanaonijua wanajua hilo fika ila ni mtetezi wa dhana ya watu kujaribu kurudi kwao kuendeleza wilaya zao wapatapo nafasi. Kule wilayani kunahitahi role models
ambao wanaweza kuamsha ari ya maendeleo kwa vijana. Ni mpinzani wa hii dhana mpya ya wasomi kujichimbia Dar Es Salaam na kusahau walikotoka. Kama huo ni ubaguzi, basi una haki ya kuniita mbaguzi
.

Mtu kama profesa Lipumba au ambao wapo katika upinzani kwa sasa kazi kubwa wanayoweza kuifanya katika Tanzania ni kufanya kila namna kuleta mabadiliko ya uongozi katika Tanzania, na wala si kurudi walipozaliwa wakajichimbie huko ama sijui wakasaidie walipotoka, isitoshe watasaidiaje? wakati hawapo katika nafasi ya kufanya maamuzi ya kisera?
 
kumlinganisha profesa Lipumba na Mrema ni comparison isiyo sawa kabisa, Mrema ashakaa katika nafasi ya kutoa maamuzi na kuyasimamia, keshakuwa naibu waziri Mkuu na pia waziri wa mambo ya ndani, kwa hiyo kwa nafasi zake ni rahisi kufanya kazi za kuwaletea watu wengi maendeleo kwa sababu yupo katika position ya kutekeleza vipaumbele vyake.
Au ukichukulia maalim seif ,yeye ameshakuwa waziri kiongozi, nafasi inayompa nafasi ya kudictate sera kwa mujibu wa cheo chake.
Sasa kwa mtu kama profesa Lipumba, unategemea yeye kama Mwenyekiti tu wa CUF atafanya nini kubwa kwa wananchi hao unaowasema wa Tabora, wakati mtu hayuko katika nafasi ya kufanya maamuzi ya kisera?(bimaana hana rungu).
au kwa kuwa ni profesa basi aende kuitisha mikutano ya hadhara atoe lecture juu ya uchumi na umasikini?.laiti huko tabora kungekuwa hata na chuo kikuu basi ungesema profesa akafundishe huko chuoni ili kusaidia mkoa wake, lakini otherwise unataka profesa akafanye nini haswaaa huko tabora.

kikubwa anachoweza kukifanya profesa Lipumba ni kuikosoa serikali,kwa hiyo ukitaka kumpima profesa kipimo kizuri ni je ana/ameikosoa /ameishauri serikali barabara?

.

Mtu kama profesa Lipumba au ambao wapo katika upinzani kwa sasa kazi kubwa wanayoweza kuifanya katika Tanzania ni kufanya kila namna kuleta mabadiliko ya uongozi katika Tanzania, na wala si kurudi walipozaliwa wakajichimbie huko ama sijui wakasaidie walipotoka, isitoshe watasaidiaje? wakati hawapo katika nafasi ya kufanya maamuzi ya kisera?

Gamba La Nyoka,

Unaongelea Prof. Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF, mimi namwongelea Lipumba kama msomi kutoka Tabora. Labda hapo ndipo tunapotofautiana. Kuwa mwenyekiti wa CUF kaanza miaka kama 10 iliyopita lakini yeye ni msomi aliyebobea wa miaka na miaka.

Ukisoma hotuba ya Zitto kwa hao wasomi toka Kigoma, ndio kitu ninachoongelea mimi. Wala sina maana viongozi hao watumie resources za serikali au vyama vyao kuendeleza kwao. Ninachotaka ni kwa watu kama hao kuwa role models wa sehemu wanakotoka na kushirikiana na wananchi kwa mawazo na namna ya kutumia resources zilizopo kule wilayani ili kujiletea maendeleo.

Hicho ndicho kinawashinda watu wengi na hata baadaye wakiingia kwenye siasa na kurudi kwao wanaonekana wageni. Wanaishia kutoa rushwa ili wapate hizo nafasi.

Utasema Mrema ni kwasababu alikuwa waziri, labda huelewi historia ya Mrema. Mrema hata kabla ya kuwa waziri alikuwa na reputation ya mtu anayeweza kutetea maslahi ya wanyonge.

Angalia wabunge wengi wa upinzani kila baada ya miaka mitano wanatupwa nje kwasababu ya njama mbalimbali za CCM, lakini mbona Dr. Slaa hajatupwa nje?

Hata ninakotoka mimi tuna watu waliobweteka Dar wengi tu. Nilipokuwa mlimani kulikuwa na walimu kutoka kule kwetu, tulikuwa tunafanya mikutano ya kuwashawishi wanafunzi ili waende kufundisha shule za huko wakati wa likizo. Hao walimu hata kuhudhuria mikutano tu na kutupa mawazo walikuwa hawataki. Sasa baadhi yao ni wanasiasa na eti wanataka kusaidia maendeleo. Ukweli ni kwamba watu kama hao hakuna jipya wanaloweza kufanya.

Kwa usomi na nafasi alizowahi kushika prof. Lipumba kama kweli
kwa wakati wote alikuwa anajali maendeleo ya kule kwao, ningetegemea CUF wawe na kiti angalau kimoja kule Tabora.
 
Tz ninavyofikiri ina matatiozo-
watanzania wenyewe -yani watanzania hawapendi maendeleo kwanini
moja hakuna mtanzania hata mmoja aliye tayari kuchangia mtoto wa mtanzania mwenzie aende shule wapo tayari kumchangia akapige ulabu au kufanya bongee la harusiiiiii yani TUPOWANAFIKI ILE MBAYA.
Na bado mzazi akijinyima akakusomesha wao bado inawakela watatafuta kila njia ujambazi ama vibuyu ili wakuangamize na hii utakuta watu wengi wenye fedha ama viongozi kwao ni choka mbaya wanaogopa kurudi kwani ni siri.

Ukizamia mjini na wa huko hawachelewi kuanza kuhoji amepata wapi fedha mshahara wake elfu sitini INDEED TANZANIANS LIKE POVERTY .
ukiwa masikini unakula mlo mmoja wa kulumangia they have good news to publish and sometimes they used to go deep down kwa kuombea ukose hata huo mlo mmoja.

If u have something it is owful news for them going here and there barking obvious ur Fisadi whereby the best soln for them is to drop u down and zap all of urs so that they can gather good news.

Na zaidi watanzania hatukubali makosa ila nikutafuta mchawi ambaye ndiye unafikiri ni source of ur problem kumbe source of ur problem ni wewe mwenyewe.Watanzania hawafanyi kazi ila tunategemea santa clous afanye mambo yake.

Watu wa ugaibuni hebu niambieni mnalala masaa mangapi??nje huwa kunakuchagua kazi?? matako ya vijibibi si tunaviosha?? kuosha vyobo je? na kuchuma stawbell mgongo vipi unaupindisha karibu ukatike au vipi? lakini mtu huyohuyo akija bongo hataki kwenda kigoma .
Matatizo yetu si Lipumba wala Mbowe wala JK ila atakayeweza kubadili mentality yetu ndiye atakuwa mshindi

tuna matatizo amabyo yameanzia chini kiasi kwamba yanaharibu mfumo mzima na inafika mahala fulani mtanzania akikuhangaisha anajiona yeye ndi yeye ->njoo kesho njoo kesho njoo kesho sio ofisini tu hadi kwa mtu binafsi umeenda kukopa fedha upeleke mgonjwa hospitali hadi mgonjwa ISRAEL anamwita ,huyo huyo ndiye wakwanza kuangua bonge la kilio na kutoa rambi rambi fedha ambayo ni zaidi mara nyingi ya ile uliyotaka kukopa.
UNAFIKI UNAFIKI UNAFIKI UNAFIKI UNAFIKI KWENDA MBELE
Tuna matatizo makubwa mno
tujiangilieni kwanza harafu tukimaliza ndiyo tumfuate JK

Mkamap,

Kuna watu wanafanya hayo unayoyasema ya kuchangia elimu za watoto ambao wala sio ndugu zao. Sio wengi ila wapo.

Mengine yote uliyosema nakubaliana nawe kwa asilimia 100. Tuna watu wengi sana wanaojichimbia mjini Dar na kusahau wanakotoka. Ukienda angalia maisha ambayo familia zao zinaishi huko vijijini, unajiuliza mara 20, hivi hawa watu wameelemika au wamejaza elimu kichwani ambayo imewapumbaza.

Watu wanafikiri mambo makubwa makubwa huku madogo yanawashinda. Wanafanya parties za mamilioni mjini, huku mama zao wanavujiwa na mvua. Kuna wengi tu wanaogopa hata kuwapeleka watoto zao kule walikozaliwa.

Sisemi prof. Lipumba yuko hivyo, ila mimi nilikuwa nategemea kama
alikuwa na ushirikiano mzuri wa kutumia elimu yake kusaidiana na watu wengine kusukuma maendeleo kule kwao, ningetegemea CUF wawe na hata jimbo moja Tabora. Waliosema mcheza kwao hutuzwa, walikuwa na maana yake.

Labda wanaomjua prof. Lipumba vizuri wanaweza kutusaidia juu ya contribution yake kule Tabora.
 
Aminia mkuu
Wachilia Lipumba, Mrema na wengine wengi, hata ashuke malaika upinzani hashindi Tz. Wasimamizi wa uchaguzi wanaamini kuwa wapo pale kwa kujuana na sio uwezo (elimu na ufanisi) wao katika kazi, so ni lazima walipe fadhila kwa aliyewachagua ili wakae hapo milele. Ikiwa kama wataamini wapo pale kwa uwezo wao na sio kujuana amini mabadiliko yatakuja tu Tz.
Tuangalie Kenya mazee, kwanini Tz isiwezekane?

A day will come

Hiyo ni kutafuta mchawi wa kushindwa kwa upinzani.

Lazima ukubali, Malawi upinzani walikuwa na matatizo hayo hayo, Zambia walikuwa nayo, Kenya walikuwa nayo nk.

Sio rahisi kumwondoa mtu aliye madarakani bila kujali ni siasa au hata boxing. Ukitaka kumtwanga bingwa kwenye ngumi, inatakiwa knockout.

Upinzani TZ hawajafikia level ya kuwa na support ya kutosha kushinda uchaguzi mkuu, achilia mbali hayo matatizo ya watawala kuiba kura na mambo mengine.

Mwaka 1995 laiti Mrema angeelewa kazi iliyokuwa mbele yake, huenda ilikuwa ni nafasi pekee ambayo upinzani wangeweza kushinda kura. Ilitakiwa atumie nguvu aliyokuwa nayo kuwaunganisha Wapinzani, kuwavuta watu mbalimbali ambao walikuwa wamechukuzwa na yale yaliyokuwa yanaendelea CCM hata kama walikuwa hawafai.

Labda mwaka 2010 na hii kujikanyaga kwa CCM huenda mambo yakabadilika ila tu inabidi Upinzani wajitahidi kuzunguka huko wilaya ambako ndio ngome ya CCM.

Tusing'ang'anie sana kutafuta mchawi na badala yake tujiangalie sisi wenyewe, je kweli tumefanya home work ya kutosha kabla ya kulaumu wengine.

Nakubaliana na Kitila kwamba watu wengi wenye uwezo wanaogopa kwenda upinzania kwa kuhofia nafasi zao na umafia wa CCM. Hilo ni tatizo la sisi wengine wote, na kwahilo mimi nawasifu ambao wamejitoa muhanga kwenye vyama vya siasa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom