Elections 2010 Lipumba live on ITV

Na uongo mwengine huooooo!!!!!!!

Kaulizwa swali la kipuuzi na akalijibu kipuuzi. Muuliza swali akadai kuwa ushindani ni kati ya Jakaya Kikwete na Wilbord Slaa. Yeye Prof. Lipumba anamuunga mkono nani. Lipumba akajibu kwa kusema "mimi namuunga mkono Professor Ibrahim Haruna Lipumba" na kuacha kicheko!

Sasa mtoa mada atuelezee kipi kingine kiliulizwa kuhusiana na Dr. Slaa na nini lilikuwa jibu la Prof. Lipumba. Acheni unazi na uongo kwani Oktoba 31, 2010 si unazi wala uongo utakaopiga kura! :A S angry:

Acha u-ccm huo, kuongea nadharia tu bila facts. weka video hapa wana JF tutaamua wenyewe kama ni uongo au vinginevyo. hapa hakuna zidumu fikira za yule mra pale kwenye kiti
 
Katika hali ya kukosa utashi wa kisiasa Prof. Lipumba alitoa mpya pale alipombeza Dr. Slaa ni kichuguu na kujikweza yeye mwenye kwa kudai yeye ni mlima wa Kilimanjaro.

Majigambo hayo Prof. Lipumba aliyatoa wakati akilijibu swali moja la wahudhuria mdahalo wake pale Movenpick. La kushangaza Prof. Lipumba alipokuwa analijibu swali hilo alijifananisha na Mzee Rukhsa ambaye alipoulizwa mwaka 1985 juu anajionaje yeye na Raisi aliyemtangulia Nyerere Mzee Rukhsa kwa unyenyekevu mkubwa alisema yeye hafai kulinganishwa na Nyerere kwa sababu Nyerere ni sawasawa na Mlima Kilimanjaro na yeye ni sawasawa na kichuguu.

Kwa lugha nyingine Mzee Rukhsa yeye alijikwaza lakini Prof. Lipumba akitumia mfano uleule amejikweza na ni jukumu la wapigakura kumkwaza hapo kesho kutwa tu.

Msemo wa "Anayejikweza atakwaza" utatimia hivi punde..
 
Katika hali ya kukosa utashi wa kisiasa Prof. Lipumba alitoa mpya pale alipombeza Dr. Slaa ni kichuguu na kujikwaza yeye mwenye kwa kudai yeye ni mlima wa Kilimanjaro.

Majigambo hayo Prof. Lipumba aliyatoa wakati akilijibu swali moja la wahudhurio mdahalo wake pale Movenpick. La kushangaza Prof. Lipumba alipokuwa analijibi swali hilo alijifananisha na Mzee Rukhsa ambaye alipoulizwa mwaka 185 juu anajionaje yeye na Raisi aliyemtangulia Nyerere Mzee Rukhsa kwa unyenyekevu mkubwa alisema yeye hafai kulingaqnishwa na Nyerere kwa sababu Nyerere ni sawasawa na Mlima Kilimanjaro na yeye ni sawasawa na kichuguu.

Kwa lugha nyingine Mzee Rukhsa yeye alijikwaza lakini Prof. Lipumba akitumia mfano uleule amejikweza na ni jukumu la wapigakura kumkwaza hapo kesho kutwa tu.

Msemo wa "Anayejikweza atakwaza" utatimia hivi punde..

Huyu naye sijui ni JUHA mwingine pandikizi la CCM
 
Kidogo Sijakuelewa mwaka 185 nyerere mwenyewe hajakuwepo au mwenzetu unaota mchana?Halafu lazima ujue siasa ndio uanze kujadili tu kuna msemo wa kiingereza unasema NO RESEARCH NO DATA NO RIGHT TO SPEAK.You are speaking without all those halafu eti na wewe ni PUBLIC POLICY ANALYST TO whom?Lipumba kujifananisha na kilimanjaro na slaa kuwa kichuguu sio ajabu,hata huyo Mwinyi wa 185 alizungumza yale kisiasa zaidi lakini maana yake ilikuwa vice versa,kwa nyerere kulikuwa hakuna sukari kwa mwinyi tele,kwa nyerere watu tulivaa viroba kwa mwinyi nguo za kumwaga kwa nyerere......................alimradi tafran kwa mwinyi kila kitu poa sasa kumbe Mwinyi alikuwa kilimanjaro na nyerere alikuwa kichuguu huo ndio mchezo wa siasa ukiujua kuucheza kama kumsukuma................:yield:
 
Nadhani LIPUMBA si mpinzani mdahalo wake wa jana na ITV uliniacha hoi na majibu yake
Mimi Binafsi naona kama ni kibaraka
 
Tatizo la lipumba haonyeshi dhamira ya kweli ya kupambana na mafisadi kitu ambacho kinampotezea credibility.
 
Mpaka sasa siwaelewi wapinzani kuto kuungana kama kweli wana nia moja ya kuikomboa nchi yetu.
Usifumbue macho ya kichwani fungua na macho ya moyoni uone vyema Lipumba kafanya mikutano lukuki lakini hata siku moja sijaona chombo cha habari kikisema au kuonesha huoni ipo namna??? unaungana na nani? maana kuna vyama muasisi wake ni mwalimu tunavijua na mjengo wake. tutafika tu.
 
Wapinzani kweli siwaelewi. Unafiki huu kweli wana uchungu na nchi? Lipumba anajua kabisaaaa, hashindi kwa vyovyote. Badala ya kuunganisha nguvu ampe Slaa kura za urais wanaanza kutuletea hadithi za mlima Kilimanjaro na Kichuguu. Nilikasirika sana kuangalia hotuba yake. Siwaelewi!!!:A S angry:
 
Uwe unasoma vitu na kuelewa sio unakurupuka tu utadhani unaoga nje
Nimesoma nimeelewa elimu yangu haifanani na yako. yangu=yako x1000 kwa hiyo hutalingana nami kielimu elimu yako bado sana unahitaji elimu kuu ya UPAMBANUZI ndio maana unaweza hata kuwanyima wageni mafuta ya kupakaa eti kwasababu tu yako kwako acha ubinafsi.
 
Sheria za nchi haziruhusu mkuu!!! Vyama vikiungana.... maana yake ni kwamba kama ni vyama vitatu, basi lazima viwili vife(na vifutwe katika list ya msajili wa vyama)...Hiyo ndiyo sheria ya kuua democrasia tz
Mpaka sasa siwaelewi wapinzani kuto kuungana kama kweli wana nia moja ya kuikomboa nchi yetu.
 
aliongea vizuru sana agape tv kiasi nilitaka kuamini kuwa siyo ccm b, i was dead wrong!
ni kweli hata mimi nilipenda sana alivyoongea atn lakini jana kwenye mdahalo mmmhh uwezo ulishuka sana hakujibu hoja vyema!
 
Nadhani LIPUMBA si mpinzani mdahalo wake wa jana na ITV uliniacha hoi na majibu yake
Mimi Binafsi naona kama ni kibaraka

Kuna mgombea mmoja anajijua hawezi kuupata urais na kwakua alikuwa mbunge amefanya MoU na chama chake akishindwa alipwe mshahara wake wa ubunge kwa miaka mitano kama yupo bungeni sasa sijui hapo lipumba na huyo bwana mkubwa nani ni mpinzani na nani mamluki.

Kisha nadhani wagombea wa Urais waliotembelea sehemu nyingi kwenye kampeni ukiachia ushabiki wa kisiasa au unaokaribia wa kibwetere ni wa CUF wao wametembea kwa usafiri wanaotumia wananchi wa kawaida hii imewasaidia kuona hali halisi ya maisha ya watanzania wa kawaida. Wamelala vijijini wamepita kwenye mashimo wanayopita wananchi wa kawaida. Ni vizuri mtu hata kama humpendi umpe haki yake as mimi nampigia Kura ninaemjua kwani ni siri yangu lakini lenye stahili kusifia kwa Slaa nitamsifia, Kuga Mzirai akitoa au akifanya la maana nitampa sifa yake wala sitambeza na huu ndio uungwana na ustaarabu. Ustaarabu sio kuwa Chadema au kumshabikia Slaa. Badilikeni.
 
Back
Top Bottom