Kwanini dish (king'amuzi) chako kinasumbua signal mara kwa mara!?

Aug 16, 2020
37
48
1.Ufungwaji wa Dish
- Uimara wa sehemu ilipofungwa

- Fundi amefungaje je kama huyu

- Fundi alitumia signal finder? (kifaa cha kutafuta signal)

- kwenye dish (lnb) tundu inayofungwa cable inayopeleka signal kwenye king'amuzi imefunikwa ili maji yasiingie n.k?

2.Cable kama imeungwa (ilikuwa fupi) imeungwaje?
3.F connector kwenye king'amuzi imefungwa vizuri
Unapata changamoto yeyote ya kiufundi kwa king'amuzi chochote kati ya hivi:-
Azamtv
Dstv
Startimes
Zuku tv
Free to air
Piga/ whatsapp +255784378129
pia tunafunga na kurepair kwenye lodge, hotel n.k
Tunapatikana Dar kinondoni ila popote Dar tunafika!

Screenshot_2020-07-08-07-51-51-1.png
 
Hapo nimeona umeweka mawe ndio kusema umefunga vizuri?
IMG-20190606-WA0010.jpeg
 
Attachments

  • IMG-20190527-WA0042.jpeg
    IMG-20190527-WA0042.jpeg
    40.8 KB · Views: 6
Nina futi 6 prime focus njoo uniwindie nile sate 7w,njoo pm tubonge
Nilesat inategemea ulipo Kama upo Arusha Utapata Eutesalt 7w kwa haraka zaidi kuliko Nilesat na kama ni Nilesat hakikisha una lnb yenye Nguvu kama Fuji
 
Fundi Madish ( ving'amuzi ) anatafuta kazi!
Umri - 35
Elimu - O'level na training mbalimbali za ufundi zisizo rasmi ingawaje ndizo zilizomuwezesha kuwa mbobezi wa:-
1.Kufunga mfumo wa tv ( cable ) kwenye: Hotel, Apartment, Office n.k
2.Kujua yote yanayohusu ving'amuzi vyote Tanzania n FTA.
3.Kufunga satellite dish aina zote.
Uzoefu - zaidi ya miaka 12
Alishafunga na kusimamia majengo makubwa kama technical director na kazi ikawa safi!
Anafanyakazi na kuishi mkoa wowote ingawaje makazi yake Dar!
Kupiga / Whatsapp +255784378129
 
Siku za mechi ndo siku ambazo simu yangu huita kuliko siku za kawaida na issue huwa "nimelipia lakini sioni naomba msaada wako"

Naona kama imekuwa ni tabia kwa watumiaji wengi wa visimbuzi hasa mashabiki wa Simba na Yanga ingawaje na wengine wapo..

Hapa nalenga watumiaji wa Azam tv na DStv ingawaje na wa startimes pia.. Ratiba inaonesha kutakuwa na mechi siku tano mbele ama pengine ligi ndo inaanza nawe kifurushi chako kimeisha.. Unangoja siku husika ( siku ya mechi ) ndo unafanya malipo.

Katika watu 10 wanaofanya malipo yawezekana ikawa wawili kati yao ndo wanaofanikiwa kuona hiyo mechi.
Kwanini!?

1. Kulipia siku husika ni uzembe ingawaje unadhani ni ujanja kuwa ungelipia kabla unaona kama pesa yako itaenda bure!

2. Mara nyingi hawa wenye makampuni ya visimbuzi ni kama huzidiwa sio kwa ofisini sio namba ya huduma kwa wateja .

3. Kipindi hichi ndo kipindi ambacho mara nyingi system zao za malipo hufail yawezekana ukalipia kifurushi hicho hicho ila ikagoma kufunguka.

4. Pengine kifurushi ulicholipia mara ya mwisho sicho ulicholipia sasa.

5. Pengine umefanya malipo kipindi ambacho kisimbuzi chako umekizima.

USHAURI:

Washa kisimbuzi chako, angalia kina signal ( channel ya bure inaonyesha ), fanya malipo n hakikisha unaona siku mbili ama hata moja kabla ya mechi kuepuka usumbufu.
 
Kuna uboreshwaji umefanywa na Azam Tv hivyo kuna baadhi ya channel hupoteza signal mpaka uiscan upya.

Cha kufanya: bonyeza MENU, System, kisha OK mara 2 kwenye factory default. Au, MENU, Settings, System Settings, Factory Reset. Password ni 0000.Kama bado channels hazijarudi kuna hitilafu kwenye dish lako.

Wasiliana nasi tukuongezee signal 0784378129 na issue zote za kiufundi kuhusu ving'amuzi vyote tucheck.
 
Naskuru mdau, kwangu Azam imenisumbua mpaka nawaza kubadilisha kabisa hawa jamaa. Azam mara nyingi customer service wao hawapokei simu. Nimejaribu kuwapata zaidi ya wiki bila mafanikio.
 
Yaani Azam hawako serious na kitu chochote sio products zao redio Yao Wala timu Yao yaani Wana feli Sana wale jamaa kila kitu Wana bahatisha
 
hizo signal unakuja kuniongezea nyumban au remontly mm nimewapigia azam awapokei nimechat nao whatsapp wameniambia nibadilile transponder iwe10981 kwa set nomal setting

chaajab nimemuita fund katafuta signal ya izo kuzunguka nyumba yote akuna signal ikabid alirudishe lilivyokuwa 11044 izo inashika chanel zoote kasoro chanel za azam tu na zimejifuta kabisa imebak extra
Kuna uboreshwaji umefanywa na Azam Tv hivyo kuna baadhi ya channel hupoteza signal mpaka uiscan upya.

Cha kufanya: bonyeza MENU, System, kisha OK mara 2 kwenye factory default. Au, MENU, Settings, System Settings, Factory Reset. Password ni 0000.Kama bado channels hazijarudi kuna hitilafu kwenye dish lako.

Wasiliana nasi tukuongezee signal 0784378129 na issue zote za kiufundi kuhusu ving'amuzi vyote tucheck.
 
Azam acheni lazima muwe makini sana yaani dish mpaka apps zote mamtatizo tu - matatizo hamkujua kuyafyatua isipokua ligi imeanza.

mlitakiwa kufanya haya mapema kabla ya ligi-- apps imekua kama ya ndigila masanja!
 
hizo signal unakuja kuniongezea nyumban au remontly mm nimewapigia azam awapokei nimechat nao whatsapp wameniambia nibadilile transponder iwe10981 kwa set nomal setting

chaajab nimemuita fund katafuta signal ya izo kuzunguka nyumba yote akuna signal ikabid alirudishe lilivyokuwa 11044 izo inashika chanel zoote kasoro chanel za azam tu na zimejifuta kabisa imebak extra
Pole mkuu kama upo dar nikupe fundi akumalizie tatizo.
Ilivyo : kama signal ipo sawa ni kucheza na remote tu ila kama ipo weak ndo mpaka dish liguswe.
 
Yaani Azam hawako serious na kitu chochote sio products zao redio Yao Wala timu Yao yaani Wana feli Sana wale jamaa kila kitu Wana bahatisha
Kiukweli kwa walipoanzia mpaka kufikia hapa wanapiga kazi ila pana vijikasoro kidogo tu ambavyo wanatakiwa wapate watu wa kuviona na kuweza kuviondoa
 
Yaani wafanye yoooteee!! Ila kama Yanga itakuwa inaonekana basi inatosha. Mana ndio timu yenye mvuto sana hapa nchini na ndio inayochagiza sana faida yao ktk udhamini Wa ligi ya bongo!
 
Back
Top Bottom