Mbeya inaishinda arusha labda kwa wingi wa watu tu, hata kwa vimiji vidogo nje ya town Arusha papo poa sana....huwezi kulinganisha USA ya arusha na mbalizi ya mbeya,
town centre ya mbeya maduka mengi wanauza Chinese products labda ubahatishe og pale Dubai electronics wakati a town ukienda pale Benson ama sound vision unafunga kazi na vitu latest original
Hotel mbeya inayovutia ukiipeleka arusha yaweza kuwa lodge, Mbeya hotel yao ya hill view ni kituko kuipambanisha na naura springs ama kibo palace ya a town city.
Viwanja vya starehe mbeya wapo nyuma mno, night club ya vibe haipo active kabisa, swimming pool zinahesabika kama sio moja ile ya forest sijawahi kusikia mwengine, cinema hall hakuna mbeya, kukweli mbeya sehemu zinazosifika labda ni city pub....A town kwenye starehe ndo penyewe, night clubs kama club D ni next level, swimming pools zimejaa vibaya mno, movie theatre ipo njiro complex hapo utacheki hata movie iliyotoka jana.
Mzunguko wa pesa; nimefanya biashara ya simu nilivyokua arusha kwa mafanikio makubwa sana arusha, kuuza simu ilikuwa ni ndani ya Muda mchache sana nikiiweka sokoni ...Nlivorudi mbeya unaambiwa naweka mzigo, calls na sms asilimia kubwa wanaomba washushiwe bei na hata nkiwashushia wanaingia mitini. Hapa mbeya simu wanazopenda ni za chini ya laki 2, ukiuza hizi Samsung za laki 8 itakaa sana bila mteja.
Stendi ya mabasi: bila shaka hapa mbeya kaibuka kidedea, Arusha wana atendi ndogo sana pale town.
Huduma za usafiri wa anga: Mbeya ndege zinakuja Mara chache sana na kwa hali ya sasa ndege inayokuja ni air Tanzania tu tena mara chache sana na ukizingatia mzunguko wa pesa ni mdogo ndege huwa haijai, mambo yakiendelea hivi wataanza kuja Mara moja kwa wiki na hatimae kutemana kabisa na mbeya....Arusha without doubt kwenye air services unapata kila kitu, ndege zinaenda Mara 2 kwa siku na mashirika yako mengi hata helicopter zipo pale uwanjani kwajili ya kukodishwa.
Makazi: kwa makazi ambayo ni mfano wa kuigwa kwa jiji la mbeya ni maeneo kama forest mpya, isyesye na uzunguni.... hayo maeneo yote ya Mbeya hayawezi kushindana na sehemu kama njiro pale atown...A town sehemu kama uzunguni ile ya relini unaweza kudhani ni ulaya.
Shule: hapa naona aibu kabisa, nahisi nawaonea mbeya sasa, Arusha wameenda mbele zaidi kiasi kwamba wana shule international kama braeburn, ist, ism, consolata, n.k hizi shule zina mfumo wa kimataifa wa elimu bora na ada zao zinatembea milioni 18 hadi 40 kwa mwaka....
Watoto wazuri: A town kachukua kombe hapa, hakuna haja ya maelezo mana ntaonekana siwaheshimu mbeya
Maisha ya chuoni: mbeya vyuo vimekusanyika eneo moja na accommodation facilities ni below average, vyuo vimejazana sehemu moja kuanzia open university, grace college, mzumbe, tia, green college, cbe, adem, n.k...ubaya wa hili eneo ni kawaida kukuta mageto hayana silingi, mageto kuwa madogo sana kiasi kwamba huwezi kuweka kitanda 4x6 na meza ya kujisomea, kifupi nayo maeneo kupata mageto standard ni kazi sana kitu kinachofanya wanavyuo wapachukie....Arusha vyuo havijabanana na mageto na mazingira ya chuo yapo amazing, kwa mfank chuo cha uhasibu pale njiro Institute of Accountancy Arusha wanavyuo wanaishi vizuri sana mana kama ni mageto yapo fresh na ni makubwa yenye ulinzi wa kutosha, hata hostels nje ya chuo zipo standard, pia arusha kuna mashirika mengi sana ya ziada kama ya utalii, umoja wa mataifa na Africa mashariki na megine kadha na kadha ambayo wanafunzi wa vyuo vya arusha wanaweza kuomba kufanyia field na hata wakihitimu kujaribu Bahati yao katika kupata ajira
Hali ya hewa kwa majiji yote iko poa