Mbeya inaishinda arusha labda kwa wingi wa watu tu
Hotel: mbeya inayovutia ukiipeleka arusha yaweza kuwa lodge, Mbeya hotel yao ya hill view ni kituko kuipambanisha na naura springs ama kibo palace ya a town city.
Starehe: mbeya wapo nyuma mno, night club ya vibe haipo active kabisa, swimming pool zinahesabika kama sio moja ile ya forest sijawahi kusikia mwengine, cinema hall hakuna mbeya, kukweli mbeya sehemu zinazosifika labda ni city pub....A town kwenye starehe ndo penyewe, night clubs kama triple A na hii ya kisasa "club D" ni next level, kutalii mbuga za wanyama kama serengeti na ngorongoro, swimming pools zimejaa vibaya mno, movie theatre ipo njiro complex hapo utacheki hata movie iliyotoka jana, Pia wana kitu kiwango cha juu "kitu cha arusha"🙂🙂 (UTANI)
Mzunguko wa pesa; tunacheki private sector, public sector na trade sector. Arusha biashara zipo kibao za madini, pesa za kigeni nyingi sana zinaingia,biashara zimechangamka, n.k Hali ya Mbeya kwa mzunguko wa pesa ni mbaya, Mbeya maisha yapo chini sana kwahio hata mzunguko wa pesa ni mdogo, Chipsi zipo za buku na unajaziwa sahani.
Matajiri: Aisee Arusha kuna matajiri nyie, Nenda uzunguni relini na njiro ndio utajua namaanisha nini...ni kawaida sana kuona range rovers, Bentleys, na gari za ajabu ajabu hata helicopters kutumika kama usafiri, ...kwa Mbeya range rover zinahesabika kabisa na ni model za zamani...range rover utayobahatisha kuiona ni ile inayokodishwa kwenye misafara ya harusi na ni model ya zamani kidogo.
Stendi ya mabasi: bila shaka hapa mbeya kaibuka kidedea kwa ile stendi yao ya nane nane na hata ile stendi kuu ya mjini, Arusha wana stendi ndogo sana pale town na haivutii.
Huduma za usafiri wa anga: Arusha without doubt kwenye air services unapata kila kitu, ndege zipo hata zinazenda nje ya nchi na kuna ndege zinaenda Mara 2 kwa siku Dar, Kwa Arushnhata helicopter zipo pale uwanjani kwajili ya kukodishwa. Mbeya ndege zinakuja Mara chache sana baada ya fastjey kutimuliwa, kwa hali ya sasa ndege inayokuja ni air Tanzania tu tena mara chache sana kwa sababu zile nauli za bei chee za fast jet hazipo tena bila kusahau mzunguko wa pesa ni mdogo kwa hio wana mbeya wengi hawawezi kumudu bei kubwa za air Tanzania na mambo yakiendelea hivi wataanza kuja Mara moja kwa wiki....
Makazi: kwa makazi ambayo ni mfano wa kuigwa kwa jiji la mbeya ni maeneo kama forest mpya, isyesye na uzunguni.... hayo maeneo yote ya Mbeya hayawezi kushindana na sehemu kama njiro pale atown...A town sehemu kama uzunguni ile ya relini unaweza kudhani ni ulaya.
Shule: Arusha wameenda mbele zaidi kiasi kwamba wana shule international kama braeburn, ist, ism, consolata, n.k hizi shule zina mfumo wa kimataifa wa elimu bora na ada zao zinatembea milioni 18 hadi 40 kwa mwaka na wanafata syllabus za kimataifa, sio syllabus ya necta. kwa Mbeya wana shule nzuri zinazofata mitaala ya Tanzania necta kama saint francis ila hawana shule ambazo zina syllubus international
Watoto wazuri: Arusha kuna watoto jamani ushindwe wewe tu, watoto wa kichaga, wairaqw, wambulu na hata watoto wa nchi za nje wamejazana wengi tu kwavile hili ni jiji la kitalii..Mbeya mabinti ni wa kawaida sana.
Maisha ya chuoni: tatizo la mbeya ni kwamba vyuo vimekusanyika eneo moja lenye hali mbaya ya malazi, vyuo vimejazana sehemu moja kuanzia tia , mzumbe, saut, adem, cbe, open univeraity, grace college na green college. vyuo vichache vina hostel za ndani kwa hio hostel za nje zinakuwa na mrundikano wa wanafunzi wa vyuo tofauti, mageto ya maeneo haya mengi hayana hadhi na huwa madogo sana kiasi kwamba huwezi kuweka kitanda 4x6 na meza ya kujisomea. Arusha vyuo havijabanana eneo moja. hostels zimejaa na mageto yapo fresh, kwa mfano pale chuo cha uhasibu pande za Njiro wanafunzi wanaishi vizuri sana kwasababu ya hostel zenye hadhi na pia mageto ni makubwa na yapo fresh, Pia arusha kuna mashirika mengi kama ya utalii, umoja wa mataifa, Umoja wa Africa mashariki na mengine ya kiserikali ambayo wanafunzi wa vyuo huomba kufanyia field na hata wakihitimu kujaribu Bahati yao katika kupata ajira.
vimiji vidogo nje ya town: Arusha papo poa sana....huwezi kulinganisha USA ya arusha na mbalizi ya mbeya,
Bidhaa feki / orijino:Mbeya kitovu kikuu cha biashara pale wanapaita "Mwanjelwa" maduka mengi wanauza bidhaa za china ama ambazo ni feki kuanzia simu, laptops, subwoofers, tv, n.k labda ubahatishe original kwa maduka ya town centre, Kwa upande wa A town mzunguko wa pesa ni mkubwa kiashiria tosha kwamba watu wanaweza kumudu bidhaa za bei ya juu ambazo ni original kuanzia simu za bei kali kama iphone ama samsung, tv zinazotrend duniani, laptops za macbook, n.k pia kuna maduka yanayouza bidhaa za chini kwajili ya wasioweza kumudu vya juu.
Hali ya hewa kwa majiji yote iko poa