Habari zenu.....
Swali hili linawalenga wanawake wenzangu waliopo kwenye ndoa na wale
wanaotarajia kuingia huko.....
Kwanza nianze kwa kusema hivi......Kwa imani yangu mimi,ukishaingia
kwenye ndoa hutoki mpaka kifo kimkute mmoja wenu....hata kwa wale
wenzetu ambao talaka inaruhusiwa.....sidhani kama wanafurahia kuvunjika
kwa ndoa....tumaini na furaha ya mwanandoa yeyote ni kuona ndoa yake
inadumu na kustawi siku hadi siku...kuvunjika kwa ndoa si jambo la
kufurahisha. Kwa maana hiyo ni wajibu wa kila mwanandoa kuilinda ndoa
yake isivunjike kwa kuvumilia mapungufu,makosa na vikwazo vinavyoibuka
kwenye maisha ya ndoa.
Back to the topic...
Kuna tabia hii ambayo wanaume wanayo...ya kuchepuka,najua wapo wanawake
wanaochepuka lakini kwa hapa niko upande mmoja.
Let's say unaishi na mumeo.wewe hujaona dalili zozote za kuchepuka,yani
anawahi kurudi, matunzo anatoa,haki zako zote unapata pasipo
longolongo....kuna ulazima wowote wa kujua kwamba anachepuka na
anachepuka na nani??... Ikitokea nimemshuhudia mumeo anaingia kabisa na
mwanamke gesti au huwa namuona anaingia nyumba fulani kwa siri na
inasemekana amemjengea hawara hiyo nyumba....natakiwa nikwambie au
nipige kimya?
Nikiuambia utapata faida /hasara gani wewe kama mke?
Na nikipiga kimya utapata faida/hasara gani?
Nimeamua niulize hivi maana mara nyingi kumetokea mabishano kuhusu
hili....wapo watu wanaoona raha kuletewa habari za waume zao,na ikitokea
wamegundua kuwa wewe ulikuwa na taarifa za uchepukaji wa wanaume wao na
hujawaambia kama ni rafiki utaitwa mnafiki. Pia wapo wale ambao
hawapendi kusikiliza habari za kuwahusu waume zao...as long as macho
yake yanaona mambo yako sawa kwa hiyo anaassume yako sawa even behind
their backs?
Ni lipi bora? Mtazamo wako pliiz....