Lionel Messi akubali kujiunga na PSG kwa mkataba wa miaka miwili, kulipwa £ milioni 25 kwa mwaka

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,815
1628611918916.png

Messi (34) amekubali kujiunga na PSG baada ya kuondoka katika Klabu ya FC Barcelona aliyoichezea kwa miaka 21

Inaelezwa atasaini mkataba wa miaka 2 wa thamani ya kulipwa Paundi Milioni 25 (baada ya kodi) kwa mwaka.
---

✍Lionel Messi amefikia makubaliano na PSG kujiunga nao akiwa mchezaji huru

✍PSG watatangaza muda wowote kuanzia sasa usajili wa Lionel Messi . Mkataba mpaka Juni 2023 na kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi

✍Messi atatambulishwa rasmi , Neymar amekuwa akisukuma sana uhamisho wa rafiki yake kutua PSG.

Pia soma
- Rasmi: Barcelona yatangaza Messi kuondoka Klabuni hapo baada ya kushindwa kuongeza Mkataba
 
Hii ni baada ya dili lake la kujiunga PSG akitokea Barcelona kama akifaulu vipimo vya afya, Messi atapokea kiasi cha £25 m kwa mwaka, Messi atasaini mkataba wa miaka miwili na option ya kuongeza wa tatu.

Anaenda kuungana na Neymar waliekuwa nae Barcelona na kutingisha pamoja ligi ya Hispania kabla ya mbrazil huyo hajaenda PSG kwa ada ya £200m.

Kama Messi anaenda kuwapa ubingwa wa ulaya waliokuwa wakiusaka kwa miaka kadhaa bila mafanikio ni jambo la kusubiri tuone.
 
Kwa jinsi wababe wa Europe wa soka walivyochoka Real madrid,Barca,Man U n,k na hakika psg itakua on fire.
 
Hii ni baada ya dili lake la kujiunga PSG akitokea Barcelona kama akifaulu vipimo vya afya, Messi atapokea kiasi cha £25 m kwa mwaka, Messi atasaini mkataba wa miaka miwili na option ya kuongeza wa tatu.

Anaenda kuungana na Neymar waliekuwa nae Barcelona na kutingisha pamoja ligi ya Hispania kabla ya mbrazil huyo hajaenda PSG kwa ada ya £200m.

Kama Messi anaenda kuwapa ubingwa wa ulaya waliokuwa wakiusaka kwa miaka kadhaa bila mafanikio ni jambo la kusubiri tuone.
Kaishatua

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Duniani hakuna usawa kabisa! Yaani mshahara wa mwaka mmoja wa huyu kiumbe unatosha kununua hisa zote za mnyama na chenji ya kutosha inabaki!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom