Linux (Ubuntu, kubuntu, Debian, fedora, linux mint, kali linux, android etc) special thread

Linux (Ubuntu, kubuntu, Debian, fedora, linux mint, kali linux, android etc) special thread

KWA WAPENZI MAGEMU
Japokuwa makampuni mengi makubwa yanayojihusha na uundaji wa magemu huwa wanalenga OS zinazotumiwa na watu wengi ambazo ni windows lakini pia kwenye linux zipo gemu nyingi tu ambazo unaweza kutumia moja wapo ni UrbanTerror.
UrbanTerror_cover.jpg

Jinsi ya kuinstall urban terror kwenye ubuntu fuata njia zifuatazo
Fungua Terminal kwa kubonyeza ctrl+alt+T, kisha andika kodi zifuatazao
Code:
wget -q -O - http://archive.getdeb.net/getdeb-archive.key | sudo apt-key add -
sudo sh -c 'echo "deb http://archive.getdeb.net/ubuntu trusty-getdeb games" >> /etc/apt/sources.list.d/getdeb.list'
sudo apt-get update
sudo apt-get install urbanterror

Magemu mingine kwa ajili ya Linux ni kama
1. OpenArena
2. Tremulous
3. TORCS
4. Xonotic
5. 0 A D

na mengineyo mengi.
 
ALTERNATIVE TO IDM IN LINUX
zipo software zinazoweza fanya kazi kama IDM japo si kwa kiasi kile kama ilivyo Internet Downloader Manager, software hiyo ni Xtreme Download Manager (XDM), jinisi ya kuinstall kwa kutumia Terminal.
Code:
sudo add-apt-repository ppa:noobslab/apps
halafu andika code ku-update

Code:
sudo apt-get update

Install xdman
Code:
sudo apt-get install xdman
 
Kuna app kama kde connect mimi huwa natumia kulink android phone yangu na Ubuntu using wifi. Hii huwa naipenda sababu
1. Naweza share copy clipboard between PC na Android phone yangu. i.e. kwamba nikikopy kitu kwenye kwenye android naweza paste straight kwenye pc
2. Naweza tumia phone yangu kama remote control ya Ubuntu. E.g kuchange tracks
3. Napata notification za simu kwenye Ubuntu.
4. Naweza transfer file from PC to phone wirelessly.

Just Google kde connect PPA on how to install
mi pia naitumia......but nikiwa nabrowse phone ....storage ambayo ni visible ni internal storage ya sim Ila SD card haionyeshi files zake.....tatizo nn?
 
Leo nilikuwa na download image ya Kali Linux karibia Mara 5 hawa washenzi tanesco wamekata umeme mpaka wamenikata maini halafu ukizingatia image zenyewe mpaka imalize kudownload huchukua muda ,kila nikidownload ikifika kati wanakata umeme halafu nilikuwa na mzuka Leo na Kali linux

Hawa Tanesco wamenikatisha tamaa Leo

Kali Linux
download kwa kutumia torrent......
 
KWA WAPENZI WA ONLINE STREAMING
Zipo software kama kodi na vlc ambazo unaweza ukaziweka kwenye linux yako na kuangalia TV kupitia internet yako bila bughudha.
687474703a2f2f6e65772e74696e79677261622e636f6d2f6439303732656635363438346562623434346363326663376263313166313865396631373036663638662e706e67
jinsi ya kuinstall kodi kwenye ubuntu ama linux mint fanya yafuatayo
1. Kwanza fungua Terminal kwa kubonyeza ctrl+alt+T

2. andika codes zifuatazo, kwa ajili ya kuongeza repository
Code:
sudo add-apt-repository ppa:team-xbmc/ppa

3. kuweka kodi andika codes zifuatazo
Code:
sudo apt-get update
sudo apt-get install kodi

4. pia andika line zifuatazo kwa ajili ya encoder
Code:
sudo apt-get install kodi-audioencoder-* kodi-pvr-*
popcorn time ndio mpango asee iko poa
 
MIFUMO ENDESHI(OPERATING SYSTEMs) MINGINE KWA AJILI YA SIMU INAYOTUMIA LINUX
Japokuwa Android ndio ni mfumo ulio maarufu na unaotumiwa na watu wengi hata hapa tanzania kwa sasa, lakini linux ina mifumo mingine mbali na Android iliyo mahususi kwa ajili ya simu za mikononi, baadhi ya OS hizo ni,
1. Ubuntu
Ubuntu ni moja ya mfumo wa linux ulio maarufu sana kwa upande wa kompyuta, hivi karibuni na yenyewe pia iliingia kwenye soko la simu za mkononi japokuwa bado zimeshindwa kabisa kufanya maajabu katika soko la simu za mkononi.
Ubuntu-android-phone.jpg

2. Tizen
Huu ni mfumo mwingine ambao unaotumia Linux, na ulikuwa ni mahususi kwa ajili ya Samsung galaxy III lakini ni copy chache sana za simu hizo zilizotolewa kwa kutumia mfumo wa Tizen, mwaka 2013 ilitarajiwa kampuni ya Huawei kutangaza kutengeneza simu zinazotumia Tizen lakini na wenyewe wamekuwa na mwendo wa kusuasua.
Tizen-logo.jpg

3. Firefox OS
Huu ni mfumo mwingine ambao application zake zimeundwa kwa muundo wa WEB APP kwa kutumia HTML5, kwa hiyo kwa wale web developer nadhani hapa utaweza kutengeneza APP kwa uwepesi na ikizangatiwa hardware zake za simu zinawasiliana moja kwa moja na html5, kampuni mojawapo iliyotengeneza simu zinazotumia firefox ilikuwa ni ZTE ya china.
Firefox-OS-phone.jpg

OS ZINGINE,
4. OpenWeb OS
5. Sailfish.
 
Nilishindwa kuinstal printa zangu ikabid niitoe baada ya siku mbili tu
 
TOP TEN TOOLS FOR HACKING WIFI NETWORK PASSWORD IN KALI LINUX​
1. Aircrack-ng
2. Reaver
3. Pixiewp
4. Wifite
5. Wireshark
6. oclHashcat
7. Fern Wifi Cracker
8. Wash
9. Crunch
10. Mac Changer
Top-10-Wifi-Hacking-Tools-in-Kali-Linux.jpg

Kumbuka swala la kuhack wifi si jepesi, unaweza ukatumia karibu tools na bado ukashindwa kufikia malengo.
 
Dah! Niliwah kutumia Ubuntu nikaipenda sana mpaka leo.
Najuta nimeweka Window 8.1 kwenye Pc yangu kisha nika Instal Kaspersky Internet Security niliyonunua.

Then hivi Majuz kuna virus anaitwa RECYLEBIN ( System volume Control) ameingia kwenye Pc yangu wakati nafanya Recovery hivyo nikaconect External had disk ndipo alipoingia.

Dah! Aisee ananisumbua kinyama Data zangu zote GB 400 Kwenye External Had disk zote zimepotea ukifungua hamna kitu.

But ukicheki properties inaonyesha zishatumika GB 400.

SIJA IFORMAT bado kwakuhofia kuzipoteza kabisa...

Plz naomba Elimu mwenye ujanja hapo nifanyeje maana ndipo nilipoanza kukumbuka Ubuntu.

Nataka nimwondoe huyu mdudu but sijajua Application gani naweza kuitumia kumwondoa kwenye Pc na External...
 
Dah! Niliwah kutumia Ubuntu nikaipenda sana mpaka leo.
Najuta nimeweka Window 8.1 kwenye Pc yangu kisha nika Instal Kaspersky Internet Security niliyonunua.

Then hivi Majuz kuna virus anaitwa RECYLEBIN ( System volume Control) ameingia kwenye Pc yangu wakati nafanya Recovery hivyo nikaconect External had disk ndipo alipoingia.

Dah! Aisee ananisumbua kinyama Data zangu zote GB 400 Kwenye External Had disk zote zimepotea ukifungua hamna kitu.

But ukicheki properties inaonyesha zishatumika GB 400.

SIJA IFORMAT bado kwakuhofia kuzipoteza kabisa...

Plz naomba Elimu mwenye ujanja hapo nifanyeje maana ndipo nilipoanza kukumbuka Ubuntu.

Nataka nimwondoe huyu mdudu but sijajua Application gani naweza kuitumia kumwondoa kwenye Pc na External...
Hiyo ni mwepesi sana anaondoka, ngoja nifunue library yangu nikupe maelekezo. Ila hakikisha una Linux yoyote.
 
Back
Top Bottom