mwaminifuhalisi
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 329
- 419
Katika thread hii tutaelimishana changamoto, faida, misaada na mambo mbalimbali yanayohusiana mifumo endeshi ya kompyuta na vifaa vingine vinavyotumia linux.
Utangulizi
Linux ni mfumo endeshi wa kompyuta ulio na asili ya ule uliokuwa unaitwa UNIX, kwa mara ya kwanza Linux iliundwa na mwanafunzi aliyekuwa ametoka kumaliza masomo ya kompyuta sayansi mwanzoni mwa miaka ya tisini aitwae Linus Torvalds.
linus torvalds
Mwanzoni Linux haikuanza kama OS bali ilikuwa ni kernel(drivers zinazoweza kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na hardware ya kifaa chochote). Lakini kwa kuwa Linus aliifanya kernel yake kuwa ni open source(mifumo huria) ndipo kukatokea na watu wengine waliotumia maarifa yao na kuifanya linux kuwa kwa ajili hata ya kompyuta tena ikiwa na mtindo wa GUI (graphical user interface).
Mmoja wa watu hao ni marehemu Ian Murdock ambaye ni mwanzilishi wa OS kongwe ya linux ambayo ni GUI, Ian Murdock aliunda DEBIAN OS wakati akiwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu akichukua shahada ya kwanza ya kompyuta sayansi kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali na kuiachia mwaka 1993, kwa bahati mbaya Ian Murdock alijiua kwa kujinyonga mwaka 2015.
ian murdock
Linux ni moja ya mradi uliofanikiwa sana kwa ushirikiano wa wataalamu mbalimbali wa kompyuta kutoka sehemu mbalimbali duniani kwani hivi leo asilimia kubwa ya seva duniani wanatumia linux, uwepo wa Android unafanya linux kuwa na watumiaji wengi sana kuliko mfumo mwingine wowote.
Hakika kama wanaIT tanzania tunataka kufanikisha vitu vingi vikubwa ni lazima tushirikiane na kushare maarifa huwezi fanya kila kitu ukiwa peke yako.
Tutaendelea kupeana maujuzi mbalimbali ya kwenye linux kwa kutumia Debian based OS kama vile Ubuntu ,Linux mint na Debian yenyewe.