Kikwete amteua Msekwa kuongoza Mamlaka ya Ngorongoro
Na Leon Bahati
RAIS Jakaya Kikwete amemteua tena makamu mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Msekwa ataongoza bodi hiyo yenye wajumbe 11, wakiwemo wabunge watatu ambao ni mahiri kwa kujenga hoja bungeni.
Wabunge hao ni Lucas Seleli (Nzega-CCM), Job Ndugai (Kongwa-CCM) na Halima Mamuya (Viti maalumu-CCM).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Ladislaus Komba alisema katika taarifa yake aliyoitoa jana jijini Dar es Salaam kwamba uteuzi wa Msekwa ulifanywa na Rais Kikwete Oktoba 5, mwaka huu wakati bodi hiyo imeteuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga.
Dk Komba aliwataja wakurugenzi wengine kuwa ni Emmanuel Lomayani (mwakilishi wa wafanyakazi Ngorongoro), Metui Ole-Shaudo (mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji) na Donatius Kamamba (mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale).
Wengine ni Deogratius Ntukamazina (katibu mkuu mstaafu, Utumishi), Yona Nnko (mkazi wa Arusha), George Kaindoh (mshauri mwelekezi) na mjumbe mwingine ambaye jina lake halijatajwa ambaye atatoka Jeshi la Polisi. Kulingana na uteuzi huo, Katibu wa Bodi ataendelea kuwa mhifadhi mkuu wa Mamlaka ya Ngorongoro ambaye ni Bernard Murunya.
YALE YALE