Lini msimu wa Kilimo cha Ufuta unaanza?

farm 360

Member
Sep 27, 2020
11
10
Habari wana JF, naomba kujua ni lini msimu rasmi wa kuanza kilimo cha Ufuta, nataraji kulima Ufuta maeneo ya Babati mkoani Manyara. Pia nahitaji ufafanuzi kwa wataalamu wa muda mrefu wa zao la ufuta katika vipengele hivi.

1. Je heka moja ya ufuta inatoa kiasi gani cha gunia au debe ngapi za ufuta?

2. Nahitaji kufahamu kama kuna mbegu nyeupe peee ya ufuta tofauti na Ile yenye vidoti doti vyeusi. Au ni namna tu ya kusafisha ufuta wakati wa kuvuna!

3. Nahitaji kufahamu aina ya udongo sahihi kwa ajili ya zao la ufuta.

4. Nahitaji kujua msimu rasmi unaanza lini/mwezi kwa maana ya masika.

5. Mbolea gani nzuri kwa kustawisha zao la ufuta kwa tija.

● Mwisho naamini mwakani 2021 zao la ufuta litakuwa kwenye chat yake kama awali maana wadau wa soko hili wazungu/wahindi wanaendelea kuja nchini na shughuli nyingi zimeanza kurudi mahali pake baada ya janga la COVID 19 kuepushwa.

Mungu ni mwema sana.

Karibuni kwa msaada wa mawazo.

Asante

The Farmer
 
Wala inshu sio corona, iliyoharibu biashara hii ya ufuta bali ni Serikali, kutaka kila kitu kukirudisha kwenye mambo ya ushirika!! Huko Katavi watu wanalia na bei, wakati huko nyuma ndimo watu walikuwa wanapiga pesa!

Ili mkulima afaidike na jasho lake acha soko ndio liamue bei!! Mazao yote waliyoyaingiza kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani kwisha habari yake!!
 
Wala inshu sio corona, iliyoharibu biashara hii ya ufuta bali ni serikali, kutaka kila kitu kukirudisha kwenye mambo ya ushirika!! Huko katavi watu wanalia na bei, wakati huko nyuma ndimo watu walikuwa wanapiga pesa!! Ili mkulima afaidike na jasho lake acha soko ndio liamue bei!! Mazao yote waliyoyaingiza kwenye mfumo wa stakabadhi gharani kwisha habari yake!!
Wizard, what..! Oooooops Good news.

Sikujua kama nalo Lipo kwa stakabadhi ghalani. Hebu niambie unanishauri nn, nisitie mbegu shambani?

Anyway ngoja tuone comments zaidi!
 
Wizard, what..! Oooooops Good news.
Sikujua kama nalo Lipo kwa stakabadhi ghalani. Hebu niambie unanishauri nn , nisitie mbegu shambani.!?
Anyway ngoja tuone comments zaidi.!
Nalo wameshaliweka kwenye utaratibu huo, huko Katavi watu wanalia vibaya mno!! Msimu huu ni kilio tupu, kukushauri nini ufanye kwangu ni ngumu, ila hiyo ndio hali halisi kwa sasa hivi, ndio maana hata huko Lindi ni kilio tupu tani 1700, zimekosa wanunuzi!! Serikali inapoingiza tu mkono wake kwenye biashara yoyote ile hasa hizi za mazao anayeumia ni mkulima!

Any way sijui kwa msimu ujao labda watabadilisha utaratibu, mfano ktk zao la pamba uhuni uliofanyika mwaka jana kwenye bei na malipo, kwa Serikali kupanga bei, kilichotokea kila mtu anajua, matokeo yake mwaka huu huko Katavi karibia asilimia 75 wameacha kulima pamba!!! Kaa chini tu utafakari kama vipi JILIPUE TU KITAKACHOTOKEA UTAKUBALIANA NACHO TU!!!
 
Nalo wameshaliweka kwenye utaratibu huo, huko katavi watu wanalia vibaya mno!! Msimu huu ni kilio tupu,kukushauri nini ufanye kwangu ni ngumu, ila hiyo ndio hali halisi kwa sasa hivi, ndio maana hata huko lindi ni kilio tupu tani 1700,zimekosa wanunuzi!...
Daaaaah, kwel nafwa na serikali yangu.! Mazao yepi hayajaingia kwenye mfumo huo, waweza niorodheshea please maana kwenye kilimo sikuwa aware sana na tozo za upanga bei za mazao. Hope mahindi na maharage ni soko huria bado havijaingizwa!
 
Back
Top Bottom