Lindi: Watu watano wafariki kwa kunywa dawa ya kuacha pombe

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,917
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Hassan Ngoma amesema Watu watano wamefariki katika Kijiji cha Nambilanje Wilayani Ruangwa, Lindi baada ya kunywa dawa waliyopewa na Mganga wa tiba asili, Shigela Malehe(39), ili iwasaidie kuacha pombe.

Akiongea na Ayo TV kwa njia ya simu DC Ngoma amesema “Wamefariki walipopewa dawa ya kuwafanya waache pombe, tumefika eneo la tukio ni mashambani mbali kabisa na Kijiji kama KM 10 hivi, kuna Mtu anaitwa Shabani Macheni alitembelewa na Rafiki yake Mfugaji wa Kabila la Kisukuma anayeitwa Shigela akamwambia ana dawa ya kuacha pombe, Shabani na wenzake wakakubali kunywa”

“Mganga alikuwa na kidumu na kikombe akawaambia masharti unasimama kwenye kizingiti cha mgongo unaupa mgongo mlango unakunywa dawa unaondoka kisha akawaambia waende Mtoni kwa maana watatapika na kuhara na yeye akawafuata baadaye kule hali ikawa mbaya Mganga akarudi akamwambia Mke wa Shabani pika uji walipofika kule Shabani akawa tayari amefariki”

“Wakarudi tena akamwambia Mke wa Shabani ampe ngano wawape wapunguze kuhara, waliporudi wote wakawa wamefariki, waliofariki ni Shaban Machenn(52), Omari Libungu (48), Mikidadi Chilika (42), Mohamedi Juma (41) na Maulidi Alli (40)”
 
Hawa wote waliofariki pamoja na mganga wao ni wapumbavu, elimu hata ya kulumangia ugali na kachumbari. Wangejizuia tu kunywa si ingewezekana? Maana ni kujinyima tu. Kuna mwinine ni mama aliomba ushauri wa kuacha kula udongo pemba, muuza mitishamba akamuambia ampe dawa ya kuacha, eti nae alipewa dawa ya mitishamba ili aache kula udongo. Tabia haina dawa ni uamuzi tu wa kuachana na matumizi ya kilevi hicho
 
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Hassan Ngoma amesema Watu watano wamefariki katika Kijiji cha Nambilanje Wilayani Ruangwa, Lindi baada ya kunywa dawa waliyopewa na Mganga wa tiba asili, Shigela Malehe(39), ili iwasaidie kuacha pombe.

Akiongea na Ayo TV kwa njia ya simu DC Ngoma amesema “Wamefariki walipopewa dawa ya kuwafanya waache pombe, tumefika eneo la tukio ni mashambani mbali kabisa na Kijiji kama KM 10 hivi, kuna Mtu anaitwa Shabani Macheni alitembelewa na Rafiki yake Mfugaji wa Kabila la Kisukuma anayeitwa Shigela akamwambia ana dawa ya kuacha pombe, Shabani na wenzake wakakubali kunywa”

“Mganga alikuwa na kidumu na kikombe akawaambia masharti unasimama kwenye kizingiti cha mgongo unaupa mgongo mlango unakunywa dawa unaondoka kisha akawaambia waende Mtoni kwa maana watatapika na kuhara na yeye akawafuata baadaye kule hali ikawa mbaya Mganga akarudi akamwambia Mke wa Shabani pika uji walipofika kule Shabani akawa tayari amefariki”

“Wakarudi tena akamwambia Mke wa Shabani ampe ngano wawape wapunguze kuhara, waliporudi wote wakawa wamefariki, waliofariki ni Shaban Machenn(52), Omari Libungu (48), Mikidadi Chilika (42), Mohamedi Juma (41) na Maulidi Alli (40)”
Watu watano wamefariki katika Kijiji cha Nambilanje Wilayani Ruangwa, Lindi baada ya kunywa dawa waliyopewa na Mganga wa tiba asili, Shigela Malehe(39), ili iwasaidie kuacha pombe.
 
Mkuu vitu vyenye uraibu sio rahisi kuacha, ni vigumu mno tofauti na unavyofikilia.

Mtu ukishakua mraibu wa madawa ya kulevya hasa pombe kali , unakua tegemezi kwa hiyo pombe kiasi kwamba Siku usipotumia hiyo pombe mwili unadhoofu unakosa nguvu na pengine unatetemeka mithili ya mgonjwa, lakini pindi anapopata pombe na kunywa mwili unarudi kwenye hali yake ya kawaida unaweza akaendelea na shughuli zake.( kwahiyo inakua ni sehemu ya maisha yake)

Uraibu ni mbaya sana... Unaweza ukawa radhi ki-fikra kuacha pombe lakini mwili haupo tayari ulishazoea kupata kile kilevi, hivyo utahitaji dawa maalumu zilizo thibitishwa na kuidhinishwa na mamlaka maalumu na sio waganga wa kienyeji.

Similar Discussions

Back
Top Bottom