Niliwahi kutoa maoni kuwa, mfumo wa kuuza Korosho unatakiwa uwe flexible kulingana na mazingira/soko na sio kuwa kama maandko ya Biblia/Quran (yaani haubadiliki)
Mfano kwa sasa mtanzania kununua korosho kwa Mkulima anaonekana kama vile amenunu pembe za Ndovu (haramu)
Najua wakulima hukopeshwa Pembejeo ambazo hukatwa pale wanapo uza Korosho lakini pia kama korosho itakosa soko na kuharibika au pengine kuuzwa kwa bei ya hasara kwa kushindwa kuweka utaratibu rafiki wa kuuza kwenye soko la ndani naona sio sawa
Bei ya Korosho kwa Nje ya nchi inafahamika kwa kila wakati; kwa nini wasiweke bei elekezi na kuruhusu watanzania wanunue ghalani walau kuanzia gunia moja la kilo mia na kuendele pengine hadi gunia 5. Zaidi ya hapo ndio wafuate utaratibu wa kununua kama kampuni.
Naamini tukiweka utaratibu, soko la ndani linaweza kula Korosho kwa kiasi kikubwa kwa bei ya kati na kuepusha hasara kwa wakulima hata kama hawatapata faida kubwa .
Nimejaribu kufuatilia Nchi yenye watu wengi kama China na kugundua kuwa hutegemea soko la ndani kwa bidhaa zao za kilimo na wanapata hela nzuri tu