Lindi: RC Zainabu Telack ameagiza kuteketezwa kwa tani 24 za Korosho zilizopo Mtama

Kwenye suala la korosho,
Serikali yetu ilishafeli na inaendelea kufeli.

Hii biashara walitakiwa waiche ijiendeshe yenyewe Kama yalivyo mazao mengine ya chakula.
Meko ndio ameua zao la korosho na watu wanamsifia tu
 
Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainabu Telack alipokuwa kwenye kikao cha utekelezaji wa mpango wa kuboresha usimamizi wa huduma za ugani kwa wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani ameagiza kuteketezwa kwa korosho tani 24 zilizopo ghala kuu la Mtama, lililopo halmashauri ya Mtama wilayani Lindi.

Hayo yamejiri baada ya Korosho hizo kupelekwa kwenye ghala kuu la hazina zikiwa na Grade One na Grade Two na baadae zikapoteza ubora na kushindwa kuuzika kwenye minada.

Sambamba na hilo Telack amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote mkoa wa Lindi kuwawezesha maafisa ugani ili weweze kuwasaidia wakulima kwenye zao la korosho.
Tembelea www.mashujaafm.co.tz kusoma habari mbalimbali #sisipamojanawe.

#mashujaahabari
 
Kwa hili tumbo langu lina tindikali tumboni ya kuyeyusha hata vyuma wanipe tu

Mjini hapa korosho tunanunua 2500.pakti
 
Niliwahi kutoa maoni kuwa, mfumo wa kuuza Korosho unatakiwa uwe flexible kulingana na mazingira/soko na sio kuwa kama maandko ya Biblia/Quran (yaani haubadiliki)

Mfano kwa sasa mtanzania kununua korosho kwa Mkulima anaonekana kama vile amenunu pembe za Ndovu (haramu)
Najua wakulima hukopeshwa Pembejeo ambazo hukatwa pale wanapo uza Korosho lakini pia kama korosho itakosa soko na kuharibika au pengine kuuzwa kwa bei ya hasara kwa kushindwa kuweka utaratibu rafiki wa kuuza kwenye soko la ndani naona sio sawa

Bei ya Korosho kwa Nje ya nchi inafahamika kwa kila wakati; kwa nini wasiweke bei elekezi na kuruhusu watanzania wanunue ghalani walau kuanzia gunia moja la kilo mia na kuendele pengine hadi gunia 5. Zaidi ya hapo ndio wafuate utaratibu wa kununua kama kampuni.

Naamini tukiweka utaratibu, soko la ndani linaweza kula Korosho kwa kiasi kikubwa kwa bei ya kati na kuepusha hasara kwa wakulima hata kama hawatapata faida kubwa .

Nimejaribu kufuatilia Nchi yenye watu wengi kama China na kugundua kuwa hutegemea soko la ndani kwa bidhaa zao za kilimo na wanapata hela nzuri tu
 
20220315_183130.jpg
 
Maamuzi ya wakati ule wa yule jamaa ndio yalichangia kuharibu hizo korosho
 
Zimepotezaje ubora wakati zilikua grade one..je suluhisho pekee ni kuzichoma moto..haziwezi banguliwa na kuuzwa soko la ndani?

Mbona kama tunakua na ufinyu wa kufikiria.

Je msimu ujao wamejipanga vipi kuondoa shida hii ya korosho kupoteza ubora..au wanasubiri zipoteze ubora wateketeze tena...absurd

#MaendeleoHayanaChama
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom