Lindi Liwale: Mama mmoja auawa kwa kupigwa risasi na polisi

Chuoni wanafunzwa kuvaa sare na kupiga salute. Lini umesikia polisi Tanzania kamvunja mshukiwa mgumu? Jw wanafundishwa kuua, na Tanzania kwa uhaba wa polisi, wanajeshi wanavishwa sare za polisi ili jumuia ya kimataifa isiilaumu nchi kulitumia jeshi kwa shughuli za kipolisi.

Dah! Kumbe kuna siri kali yaani wajeda wanavalishwa kipolisi kama ni hivyo kulikoni tupo pabaya.
 
Hii Wilayabhaina tofauti na Kibiti ya kipindi kile.. Tatizo nn, kuna kila aja ya serikali kuiangalia hii Wilaya kwa jicho la 3
 
Akizungumzia tukio hilo, kamanda Kintinkwi alisema tarehe 19.12.2020 usiku katika kijiji cha Kibutuka, wilaya ya Liwale jeshi la polisi lilifanya msako kuwasaka watuhumiwa waliochoma moto gari. Ndipo walipokwenda nyumbani kwa Mawazo Halid Magumba ambao baada ya kujitambulisha walimtaka afungue mlango na atoke nje. Lakini Mawazo alikataa kufungua mlango na kutoka nje.

" Askari walivunja mlango, ndipo Mawazo alipotoka nje akiwa na panga. Hali iliyosababisha askari wajihami. Hata hivyo Aziza alikuwa nyuma ya Mawazo akijaribu kuwazuia polisi wasimkamate Mawazo," alisema Afande RPC Kitinkwi.

Alisema katika purushani hiyo Aziza alipigwa risasi ambayo ili mjeruhi na kusababisha kifo chake. Ingawa jeshi hilo halikudhamiria kumuuwa yeyote kati ya hao wawili.

RPC Kitinkwi aliweka wazi kwamba jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi ili kujua mazingira ya tukio la kifo cha marehemu Aziza ili kama ikibainika aliuawa kutokana na uzembe wa aliyemuua itabidi sheria ichukue mkondo wake kwa muuaji. Kwani hakuna aliye juu ya sheria
"An intention to shoot is not an intention to kill" Masipa Thokozile J
 
Back
Top Bottom