Limebuniwa na Kutengenezwa Dr Patric Jonathan Mkoani Arusha

NDINDA

Platinum Member
Apr 4, 2011
10,319
47,026
Trekta hii ina uwezo wa kulima ekari 5 kwa siku,linasaga na kukoboa nafaka kilo 300 kwa siku.Pia linatumika kama pampu ya maji. Ilibuniwa na kutengenezwa na Dr Patric Jonathan mwaka 2008 mkoani Arusha katika kituo cha zana za kilimo na ufundi vijijini (CAMARTEC).Picha ni leo mchana katika Banda la CAMARTEC kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika Maadhimisho ya Wiki Ya Utumishi wa Umma. Picha na Victor Makinda

IMG_0796.jpg
 
Kuna mikakati gani yakulifanya liwakomboe wakulima wa TANZANIA. Au ndio kasumba ile ya kuthamini vya mzungu. Hapa serikali yenye akili timamu lazima iintervene
 
Tatizo siyo zana za kilimo ila kilimo cha uhakika sasa kama utakuwa na zana bora za kisasa halafu mkishalima shamba mnasubiria mvua hapo mi sioni kama kuna ufanisi wowote.pamoja na serikali kuendelea kubuni zana mpya na za kisasa mbinu hizo zingetakiwa ziende sambamba na uendelezaji wa mabonde ya umwagiliaji.
 
nyumbu motor works pia si wanatengeneza magari? at least washirikiane watengeneze kitu matata, ntafurahi kama siku moja bongo tutakua na magri yetu yenye majina ya kitanzania, mfano ningependa kuona gari la mizigo lenye kichwa cha nymbu na likiitwa nyumbu truck au tukawa na mabasi yetu mazuri au sports car lenye jina la cheetah kwani ni fastest land animal alive, IMO, tureplace sacania na volvo mungu akipenda, nadhani wanaweza kushirikiana, superdoll watatengeneza matela na nyumbu watengenze engine waasemble basi itakua shwari
 
Trekta hii ina uwezo wa kulima ekari 5 kwa siku,linasaga na kukoboa nafaka kilo 300 kwa siku.Pia linatumika kama pampu ya maji. Ilibuniwa na kutengenezwa na Dr Patric Jonathan mwaka 2008 mkoani Arusha katika kituo cha zana za kilimo na ufundi vijijini (CAMARTEC).Picha ni leo mchana katika Banda la CAMARTEC kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika Maadhimisho ya Wiki Ya Utumishi wa Umma. Picha na Victor Makinda

IMG_0796.jpg
Badala ya SUMA kuagiza matrekta kutoka India, wangelitoa oda ya aina hii ya matrekta ili kuchangia gharama za utafiti na uboreshaji wake
 
Nnavyoijua bongo hizo innovations zinaishiaga kwenye maonyesho tu, kuna wale jamaa pale mlimani IPI wana compactor waliitengeneza mwishoni mwa miaka ya tisini lakini huwa inaonekana kwenye maonyesho tu, baada ya hapo stoo, kufuli. Sijaelewa bado tatizo ni nini.
 
Tatizo tukikubali kila kitu kitengenezwe Tanzania na kila mtu atajua bei ile 10 % ya watafunaji itatokea wapi mkuu Nyambala.
 
Mh! mbona ame-copy na lu-paste Valmet?....kubuni kitu kipya it should be different from what is existing....ni wazi hata hayo matairi alinunua dukani akaja kufunga humo....Bado sana aisee!!

Mkuu Sajenti; naomba ufahamu kwamba katika UBUNIFU kuna wa aina mbili, kuna UBUNIFU unaotokana na kuona kitu cha mwenzio na ukatafuta jinsi ya kuboresha zaidi na hapa ndipo walipo wengi. UBUNIFU mwingine ni ule unaohusisha kitu ambacho hakijawahi kuwapo kabisa katika ulimwengu huu, ambapo hawa ni wachache sana. Watengenezaji wote wa magari kama TOYOTA hawatengenezi kila kitu wenyewe, kuna wengine wanahusika kutengeneza engine, matairi nk na wao mwisho wa siku huwa wana-design model ya hiyo gari na kufanya assemble ya hivyo vitu wanavyonunua kutoka kwa wengine.

Hivyo basi MTANZANIA mwenzetu huyu amepiga hatua kubwa sana na tunahitaji kumpongeza na kuona jinsi gani tunaweza ku-support hizi jitihada kwa gharama yeyote ile.

MAWAZO YANGU - CHADEMA wangeandaa maandamano ya kupongeza jitihada hizi na kulaani uagizwaji wa matrekta kutoka China na wakati kuna mtanzania aliyejaribu.
 
Mh! mbona ame-copy na lu-paste Valmet?....kubuni kitu kipya it should be different from what is existing....ni wazi hata hayo matairi alinunua dukani akaja kufunga humo....Bado sana aisee!!
IMG_0796.jpg

Sio kweli!
JE WACHINA WANAKUZIDI KWA TEKNOLOJIA?
Kama ndio ujue walianza hivyo, then wakaendelea kuboresha na wengine (hukohuko China) wakakopi na kuboresha na etc hadi leo unaona wanavyo vyakwao ambavyo wengine hawana.

It is not logic kuponda mtu aliyejaribu kufanya kitu na kikaonekana badala yake nigeona ni vyema kuwaamsha waliosoma na kusoma na wana phdz etc kwenye kila fani lakini hawana cha kujivunia kuwa wamefanya kwaajili ya jamii inayowahitaji zaidi ya "so called papers".

"I love innovations"
 
Hiyo trekta bei yake ikoje? Ni bei inayoweza kufanya hata mkulima wa kipato cha kati aweze kununua? Tatizo tulilonalo ni bei juu...! Mchina oyeee!
 
Hili lilibuniwa mwak 2008 leo ni 2011 kuelekea 2012 almost miaka 4 hakuna muelekeo wa kutengeneza matrekta haya hapa nchini badala yake tunaishiwa kuagiza ma farm track toka India na Kubota (power tillers) za KiChina vya kwetu tunabaki tukiweka kwenye vibanda vya ,maonyesho...hii kumaa...aanisha nin i? Angalia pale SUMA JKT kuna matrekta hovyo kibao toka China na India, kwa nini hao CAMATEC au Nyumbu wasitengeneze ya kutosha na yanayofaa kwa mazingira yetu na yakauzawa kwa bei nafuu kwa wakulima wa kitanzania ?
 
Wakuu mnaohudhuria hayo maonyesho, mnapata majibu gani mnapohoji mikakati iliyopo ya kuendeleza hiyo technology? Hao CAMATEC na NYUMBU wana project lini gari ama trekta la kwanza litaenda sokoni? Au mnasifu/kufurahi na kupiga picha tu baaas, hamuulizi! YE!
 
Tatizo siyo zana za kilimo ila kilimo cha uhakika sasa kama utakuwa na zana bora za kisasa halafu mkishalima shamba mnasubiria mvua hapo mi sioni kama kuna ufanisi wowote.pamoja na serikali kuendelea kubuni zana mpya na za kisasa mbinu hizo zingetakiwa ziende sambamba na uendelezaji wa mabonde ya umwagiliaji.
Siyo kila mahali panahitaji umwagiliaji. Usukumani matreka yametumiwa tangu miaka ya 1950 kwenye kilimo cha pamba na kulikuwa na ufanisi mkubwa. Matatizo yalianza baada ya kuuwa vyama vya ushirika vya awali na kuingiza haya mabodi kama Bodi ya Pamaba ambayo yalileta ufisadi unaoendelea mpaka leo kwa kuwakandamiza wakulima. Teknolojia yakisasa inahitajika hata bila ya umwagiliaji. Lakini mkulima wa kawaida ataweza kuinunua wakatii bei anazopewa ni za wizi wa mchana?
 
Back
Top Bottom