Limebuniwa na Kutengenezwa Dr Patric Jonathan Mkoani Arusha

Limebuniwa na Kutengenezwa Dr Patric Jonathan Mkoani Arusha

Kuna mikakati gani yakulifanya liwakomboe wakulima wa TANZANIA. Au ndio kasumba ile ya kuthamini vya mzungu. Hapa serikali yenye akili timamu lazima iintervene

Ndugu umenena vema hapo; ila bahati mbaya Tanzania miaka hii serikali yenye akili timamu ni bidhaa adimu kabisa. Nasita tu kusema hatuna serikali.
 
Mh! mbona ame-copy na lu-paste Valmet?....kubuni kitu kipya it should be different from what is existing....ni wazi hata hayo matairi alinunua dukani akaja kufunga humo....Bado sana aisee!!
IMG_0796.jpg
We Bwana vipi? Hata Toyota au kampuni yoyote ya magari haitengenezi kila kitu yenyewe. Kuna makampuni ambayo ni suppliers wa parts (vipuri) mbalimabili, matairi, rejeta, na vitu vingine. Sana sana kampuni husika hutengeneza engine, bodi na sehemu zingine nyeti. Hivyo ndivyo wanavyoweza kupunguza gharama na kufanya productsa zao kuwa na bei nafuu.
 
Linauzwa Tshs ngapi? Kama kuna nayefahamu tafadhali.....
Mimi nadhani hii bado ni modeli ya majaribio. Kwa kitaalamu inaitwa prototype. Kabla ya kuingizwa sokoni zinaweza kutengenezwa proptotype kam 3 au 4 hivi.Hizo zinatumika kufanyia majaribio kuhakikisha kuwa technical problems zote zimeondolewa kama vile utumiaji wa mafuta, balance, speed, safety, n.k. Ni baada ya hapo ndiyo linaweza kupata kibali cha kuingia sokoni. Sijui kama Tanzania tumeishakuwa na taasisi ya kusimamia shughuli kama hizo.
 
Siyo kila mahali panahitaji umwagiliaji. Usukumani matreka yametumiwa tangu miaka ya 1950 kwenye kilimo cha pamba na kulikuwa na ufanisi mkubwa. Matatizo yalianza baada ya kuuwa vyama vya ushirika vya awali na kuingiza haya mabodi kama Bodi ya Pamaba ambayo yalileta ufisadi unaoendelea mpaka leo kwa kuwakandamiza wakulima. Teknolojia yakisasa inahitajika hata bila ya umwagiliaji. Lakini mkulima wa kawaida ataweza kuinunua wakatii bei anazopewa ni za wizi wa mchana?
nakumbuka bado mdogo nilikua singida vijijini kule walikua wanalima sana pamba, ukifika wakati wa kuchuma pamba ni peupeee hadi panapendeza utafikiri kuna snow, mambo yaliianza kugeuka wakati wakipeleke pamba yao kwenye ghala na kuambiwa wasubiri hela, basi kule kijijini magari sio sana , kwa vile kuna vimilimamilima watu wakiona gari tuu basi wanakimbilia kwenye ghala wakidhani hela za pamba zao ambayo walishauza siku nyingi zimekuja, basi kila siku ni mchezo huo , sio kila gari linalokuja ni lililolta hela, basi mambo yakenda hivyo hivyo mwisho walilazimishwa kupewa baiskeli za kijani za phoenix, baada ya hapo sikuona shamba la pamba tena singida vijijini, kudadadeki, sasa hivi ni kitunguu na alizeti tuu, ndio maana mafuta ya kupikia ya alizeti ni bei chee singida,kuna mengi sana yanatakiwa yarekebishwe ili kilimo chetu kiwe bora
 
Hiyo tractor au terekita? Maana naona hicho kiti kilivyo, akimaliza kulimia na kiuno hana.
 
Trekta hii ina uwezo wa kulima ekari 5 kwa siku,linasaga na kukoboa nafaka kilo 300 kwa siku.Pia linatumika kama pampu ya maji. Ilibuniwa na kutengenezwa na Dr Patric Jonathan mwaka 2008 mkoani Arusha katika kituo cha zana za kilimo na ufundi vijijini (CAMARTEC).Picha ni leo mchana katika Banda la CAMARTEC kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika Maadhimisho ya Wiki Ya Utumishi wa Umma. Picha na Victor Makinda

IMG_0796.jpg

Bonge la Trekta lkn ka rangi kake mbona kamekaa kimagambamagamba hivi....
 
Nnavyoijua bongo hizo innovations zinaishiaga kwenye maonyesho tu, kuna wale jamaa pale mlimani IPI wana compactor waliitengeneza mwishoni mwa miaka ya tisini lakini huwa inaonekana kwenye maonyesho tu, baada ya hapo stoo, kufuli. Sijaelewa bado tatizo ni nini.

Kweli kabisa, watoe data toka mwaka 2008 mpaka leo wametengeneza tena mangapi? Huu ni usanii tangu presdar mpaka watu wake!
 
Badala ya SUMA kuagiza matrekta kutoka India, wangelitoa oda ya aina hii ya matrekta ili kuchangia gharama za utafiti na uboreshaji wake

Uko sahiihi tanzania tumekalia siasa. WE angalia speaker alieyamaliza muda wake Sitta. Gharama ya samani zailiztumika wkenye ofisi yake ya ubunge. Yaani hata viti vya ukalia wageni vinaagizwa kutoka nje wakati mkoa wa tabora una mbao z amti mgumu.

  • Kwa nini hawakupenwa mafundi wa tabora tenda japo ya samani za wageni. Au japo viwanda vidogo vya ndani.
Then tunasikia beno ndulu anasema thamani ya fedha inashuka sababu tunaagiza sana zaidi ya kile tunacho export. Hata zile gari za nyumbu za JWTZ nadhani ni maonyesho tu.
 
Back
Top Bottom