Likizo za shule kufuata ratiba ya Serikali

Likizo za shule kufuata ratiba ya Serikali

drilling

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
4,905
Reaction score
5,088
Naiomba Serikali/wizara husika kufikiria tena ratiba zenu za likizo. Ndugu zetu wa madhehebu ya kikristo wao hawana tatizo na likizo hizi za wanafunzi.

Naomba Serikali kufikiria upya ratiba za likizo za wanafunzi mara zote sikukuu za kikristo; Pasaka na Krismass shule hufungwa lakini sikukuu ya kiislamu shule hazifungwi.

Utakuta wanafunzi wa kiislaamu wanafunga swaum ya ramadhani kwa mazingira magumu wakiwa wapo shule hata futari yao pia ya shida.

Inapofika siku ya Iddi e-fitri wanafunzi wa kiislamu wapo shule wanaedelea na masomo Idd kubwa pia wapo shule labda itokee bahati nzuri ratiba ya serikali imeangukia kwenye Iddi hapo watapumua.

Nawaomba bakwata ingawa chama hiki cha bakwata sikiamini kabisa walizungumzie suala hili nawaomba wabunge mliangalie na mlisemee
 
Mada kama hizi mnaifanya serikali iendelee kuwashikilia masheikh wenu wa uamsho
 
Mkuu kwa kweli nchi hi 'the ground is not levelled' all Tznia are equal but some are more equal than others......mid term ulipaswa kua mwezi wa tatu, ili wakirudi wanafunzi wasome wanne watano na wasita wafunge lakini kwasababu ya pasaka imesogezwa mpaka wa nne kwahiyo wanafunzu wana soma mwezi moja tu nakufunga tarehe 7 mwezi wa sita kwa mhula mkubwa' kwakweli watafika nakufanya mtihani bila kusoma chochote......imagine serikali haina dini. Ila wanacho fanya sio sahihi.
 
Mkuu sikukuu za kiislamu mpaka uangalie mwezi utoke, kwa ujumla hamna calendar inayoeleweka
 
Karenda zenyewe za kiislamu hazieleweki. Sikukuu zinapishana pishana.

Hivi ni lazima kila mambo yaende 50/50
 
Umeniwahi mkuu
Nilitaka kukoment ivi
Kajichanganya mtoa mada
Ili hoja yako iwe na mashiko ni lazima pia ushauri serikali ifuate kalenda ya kiislam, vinginevyo itakuwa vigumu sana kwani sikukuu za kiislam zinazunguka kama saa!!
 
Ili hoja yako iwe na mashiko ni lazima pia ushauri serikali ifuate kalenda ya kiislam, vinginevyo itakuwa vigumu sana kwani sikukuu za kiislam zinazunguka kama saa!!
... uko sahihi. Sikukuu za kiislamu hususan Idd el Fitr inazunguka kiasi kwamba ndani ya miaka 12 hivi inakuwa imeangukia almost kila mwezi (January to December) of course kwa kufuata Kalenda ya Gregory ambayo ndio tunayoifuata. Suluhisho la hili ni kujenga hoja kubadili Katiba ili Tanzania ifuate Islamic Calendar na maamrisho mengine ya Allah.
 
Ni kweli lakini, unapokuwa kwenye swaumu siunaendelea na majukumu kama kawaida? Kuhusu sikuu za idd mbona watoto huwa hawaendi shule pia tatizo ni kuwa siku yenyewe haieleweki kwani inategemea kuonekana kwa mwezi,
 
Back
Top Bottom