Likizo za shule kufuata ratiba ya Serikali

Likizo za shule kufuata ratiba ya Serikali

Naiomba Serikali/wizara husika kufikiria tena ratiba zenu za likizo. Ndugu zetu wa madhehebu ya kikristo wao hawana tatizo na likizo hizi za wanafunzi.

Naomba Serikali kufikiria upya ratiba za likizo za wanafunzi mara zote sikukuu za kikristo; Pasaka na Krismass shule hufungwa lakini sikukuu ya kiislamu shule hazifungwi.

Utakuta wanafunzi wa kiislaamu wanafunga swaum ya ramadhani kwa mazingira magumu wakiwa wapo shule hata futari yao pia ya shida.

Inapofika siku ya Iddi e-fitri wanafunzi wa kiislamu wapo shule wanaedelea na masomo Idd kubwa pia wapo shule labda itokee bahati nzuri ratiba ya serikali imeangukia kwenye Iddi hapo watapumua.

Nawaomba bakwata ingawa chama hiki cha bakwata sikiamini kabisa walizungumzie suala hili nawaomba wabunge mliangalie na mlisemee
Ndugu;
Kama unaushawishi wa calender anza na siku ya ijumaa iwe kama jumapili msiwe mnaenda kazini, lakini kama hilo huliwezi leave pie as pie.
 
Mkuu naona kichwani kwako una double standards na mentality finyu. Kumbuka pia wakristo hufunga quaresma so ipe uzito kama ramadhani they are almost the same.kuhusu eid ina fluctuate ni ngumu shule kuwa na mfumo unao fluctuate kila mwaka ni hayo tu

unafunga quaresma unailinganisha na swaum ya ramadhani . quaresma unafunga chakula unachopenda ndio huli kama unapenda kula nyama basi unafunga kule nyama chakula kingine unakula sasa hiyo ni funga. kama mnafunga funga kula chochote pia funga matamanio ya kimwili pia funga kusema uongo pia funga kuiba. hiyo ndio funga ya waislamu . sio unafunga kula msosi unaoupenda. fungeni kama mitume waliopita kina musa issa ibrahimu na mitume wote
 
Hili halitakaa litokee Duniani maana tunatembelea calendar ya Kirumi mpaka sasa mahesabu yanafata YESU Kristo so ili hoja yako ifanikiwe kwanza muangushe calendar ya Kirumi /Kikiristo.
 
Nafikiri mtoa mada ana hoja ya msingi ingawa inawezekana asieleweke kwa kila mtu. Na nafikiri pia hamaanishi waislamu wakati wa ramadhan basi Shule zifungwe. Nadhani il I mjadala huu uwe na Afya lazima maswala ya msingi bila kusukumwa na chembe au hisia za" udini upendeleo" bali yale ya kweli. Ni kweli waislam kalenda yao ni dynamic na hivo ni ngumu kuifuata kwa ajili ya mapumziko kwa wanafunzi. Lakini pia hoja ya mid term nadhan ni miezi mitatu na si minne km ilivojitokeza mwaka huu. Mim ni mtumish Wa serikali ambako ktk secta niliyopo huwa tunalipwa mshahara kila tar 24 ya kila mwezi Kwa awamu hii ya magufuli. Ktk moja ya magroup yetu ya wasapp kuna mchangiaji mmoja alipost na kusema NMB oyee akimaanisha mshahara tiyari na hii ilikuwa tar 19 mwezi Wa nne. Alishambuliwa sana na wanagroup kwamba uenda anavuta bangi au amelogwa. Lakin ukweli serikali ilitoa mshahara siku hyo ya alhamis. Manake nn ijumaa ilikuwa ijumaa kuu, na tar 24 ilikuwa jumanne baada ya jtatu ya pasaka. Sasa kwann mshahara haukulipwa tar hyo. Kwhy kuna mambo mengi ya kujadili
Mimi mshahara wa mwezi wa nne uliingia tarehe 17
 
unafunga quaresma unailinganisha na swaum ya ramadhani . quaresma unafunga chakula unachopenda ndio huli kama unapenda kula nyama basi unafunga kule nyama chakula kingine unakula sasa hiyo ni funga. kama mnafunga funga kula chochote pia funga matamanio ya kimwili pia funga kusema uongo pia funga kuiba. hiyo ndio funga ya waislamu . sio unafunga kula msosi unaoupenda. fungeni kama mitume waliopita kina musa issa ibrahimu na mitume wote
SIKUTAKA KABISA KU COMMENT HII MAMBO LAKINI NIKUSIHI TU KUFUNGA SIYO KULA NA ULIVYOANDIKA KAMA MTU ANAENDA LIKIZO HALAFU ANARUDIA UCHAFU ULE ULE ALIOUCHA KABLA YA KUFUNGA


PIA SWALA LA KUFUNGA LINATEGEMEA NA MAFUNDISHO YA IMANI YAKE NAMNA INAVYOMFUNDISHA MFANO WAKRISTO WAKIFUNGA WALICHOFUNGA WANAWAPELEKEA WASIONACHO ILA WENGINE WAKIFUNGA WANAKULA KILE CHOTE ALICHOFUNGA KWA MDA WALIOJIPANGIA

PIA UKIWAZUNGUMZIA AKINA IBRAHIM,ISSA,MUSA NK HAO WALIFUNGA BILA KULA CHOCHOTE HEBU JARIBU WEWE THEN SISI TUTAKUFUATA HUWEZI TOFAUTISHA HAO WATU NA WEWE MKUU ?

MWISHO USIDHARAU IMANI YA MTU KWA TAMAA YA IMANI YAKO NA USIJIDANGANYE SANA KUWA KUNA IMANI BORA ZAIDI YA NYINGINE IMANI BORA NI ILE ANAYOIAMINI MTU MUHUSIKA TU NA SIYO MWINGINE
 
unafunga quaresma unailinganisha na swaum ya ramadhani . quaresma unafunga chakula unachopenda ndio huli kama unapenda kula nyama basi unafunga kule nyama chakula kingine unakula sasa hiyo ni funga. kama mnafunga funga kula chochote pia funga matamanio ya kimwili pia funga kusema uongo pia funga kuiba. hiyo ndio funga ya waislamu . sio unafunga kula msosi unaoupenda. fungeni kama mitume waliopita kina musa issa ibrahimu na mitume wote
Mzee kama ijumaa tu ni siku ya kazi kupata likizo ya mfungo ndo itawezekana?
 
Naiomba Serikali/wizara husika kufikiria tena ratiba zenu za likizo. Ndugu zetu wa madhehebu ya kikristo wao hawana tatizo na likizo hizi za wanafunzi.

Naomba Serikali kufikiria upya ratiba za likizo za wanafunzi mara zote sikukuu za kikristo; Pasaka na Krismass shule hufungwa lakini sikukuu ya kiislamu shule hazifungwi.

Utakuta wanafunzi wa kiislaamu wanafunga swaum ya ramadhani kwa mazingira magumu wakiwa wapo shule hata futari yao pia ya shida.

Inapofika siku ya Iddi e-fitri wanafunzi wa kiislamu wapo shule wanaedelea na masomo Idd kubwa pia wapo shule labda itokee bahati nzuri ratiba ya serikali imeangukia kwenye Iddi hapo watapumua.

Nawaomba bakwata ingawa chama hiki cha bakwata sikiamini kabisa walizungumzie suala hili nawaomba wabunge mliangalie na mlisemee
Siku za Eid ni public holidays kama ilivyo kwa Pasaka na Christmas.

Labda sijakuelewa vizuri. Una maana wakati wa mfungo mtukufu wa Ramadan shule zifungwe mwezi mzima? Kumbuka Pasaka hutanguliwa na mfungo wa Kwaresma na shule hazifungwi. Hoja yako iko wapi hasa?

Kwa sababu za kihistoria, ukumbuke serikali yetu inafuata kalenda ya magharibi. Maana yake mfungo wa Ramadan hutokea vipindi tofauti kwenye kalenda hiyo.
 
Hili halitakaa litokee Duniani maana tunatembelea calendar ya Kirumi mpaka sasa mahesabu yanafata YESU Kristo so ili hoja yako ifanikiwe kwanza muangushe calendar ya Kirumi /Kikiristo.
Na ndicho kitu kisichowezekana...maana hata wachina wana miaka yao lakini ya mrumi ndiyo ametamalaki
 
Mkuu sikukuu za kiislamu mpaka uangalie mwezi utoke, kwa ujumla hamna calendar inayoeleweka
Kalenda ya Kiislamu inaeleweka lakini haiendani na ile ya mafharibi inayofuatwa na serikali.
 
... huyo anajitoa ufahamu Mkuu. Anataka kujenga hoja uchwara eti wapumzike kipindi cha mfungo!
Kamanda, hilo ni wazo lake. Tusiliite uchwara.
Hoja iwe kwamba, wakipumzika wakati wa mfungo, je nayo kwaresma itakuwa mapumziko?
Maadam tunafuata kalenda ya kirumi, itakuwa vigumu kufanya lolote la aina hiyo.
 
Mleta mada wewe ushauri wako ni upi? lete mapendekezo tuyafanyie kazi, je unataka shule zifungwe wakati wa ramadhani ? je inchi za kiislam wanafunzi wao ufunga vp labda tuige kutoka huko.
 
Back
Top Bottom