lijue jiji la Mbeya (Green city), makabila makuu matatu na shughuli zinazowapa heshima

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
MUHIMU: jiji la Mbeya ni wilaya moja tu ndani ya Mkoa na sio wilaya zote za Mbeya

WANYAKYUSA

Hawa kwa asili sio wazawa wa wilaya ya Mbeya jiji, wametokea wilaya jirani za Rungwe (ulipo mji maarufu wa Tukuyu) na Kyela. Walikuja Mbeya jiji kwasababu ndipo yalipokuwa makao makuu ya mkoa mzima na wilaya zote za Mbeya.

(a) Elimu

Si kwa Mbeya tu, kwa mikoa yote ya kusini mwa Tanzania wanyakyusa ndio vinara kwenye elimu, kwa hapa jiji la Mbeya shule nzuri za kulipia na Vyuo wao ndio wanaongoza kwa kujaza,

(b) Ajira za maofisini

kwa vile ndio vinara wa kwenye elimu, wengi huwa na sifa za kuajirika katika nafasi za mameneja, wahasibu, wahandisi, wanasheria, n.k.

(c) Siasa

Wameweza kushika kwa kiasi kikubwa nafasi za siasa katika jiji hili la Mbeya, hata katika historia wabunge wengi wa hapa Mbeya jiji ni wanyaki.

(d)Wachungaji na waimba gospel :

kama umewahi kusikia kwamba Mbeya ndio jiji la pili Africa kwa kuwa na makanisa mengi basi jua nyuma ya hayo makanisa ni wanyakyusa, na hata wachungaji maarufu Tanzania wengi ni wanyakyusa kuanzia Mwamposa, Mwalimu Mwakasege, Lusekelo, n.k. ukija kwa waimba gospel nako wamejaa hapa Mbeya ila kwa nchi wanaofahamika ni kina Bahati bukuku, Boby Mwaitege, n.k.


WAKINGA

Hawa kwa asili sio wazawa wa wilaya ya Mbeya jiji, wametokea wilaya ya Makete mkoa wa Njombe, hapo zamani walikuwa wakija wachache ila kuanzia miaka ya 90 ni wengi wamefikia jiji hil.

(a) Biashara:

Shughuli kuu ya wakinga ni biashara, wameweza kulitawala soko kubwa nchi nzima la Kariakoo basi na huku Mbeya hawajapaacha salama.

kwao biashara ni kama utamaduni kama ilivyo kwa waarabu, ni kawaida kukuta mkinga amesoma ana degree lakini hana muda wa kutafuta ajira na hata akiajiriwa akaja kuiacha ili afanye biashara, wanapenda biashara hawa watu acha tu!

Matajiri wengi wa jiji hili ni wakinga wale walioweza kupiga mshindo kwenye biashara zao.

Maduka ya mtaani yanayouza mahitaji ya nyumbani, maduka makubwa ya kujumua, mahoteli, maduka ya hardware za ujenzi, na biashara nyingi wakinga wamezi shika.

(b) Siasa;

kisiasa nao hawajalala, hapo 2010 hadi 2020 chadema chini ya Joseph Mbilinyi (Sugu) waliishika Mbeya jiji kisawa sawa,

WASAFWA

Hawa ndio wazawa asili wa jiji hili la Mbeya, hawa ndio walikutwa hapa Mbeya mjini.

Wanathamini sana utamaduni lakini katika moja ya tamaduni ni kwamba wao ni kama mwiko kuishi katika jamii yenye makabila mengine, wanafanya hivi ili kulinda tamaduni zao zisiingiliwe na zile za kigeni na pia kizazi kisichanganywe na makabila mengine. Kwa hali hii wasafwa wengi walikuwa wenyeji lakini walipoanza kuona wageni wanakuja mjini wakawa wanawapisha huku wao wanaenda kuishi mbali na mji wa wageni. kwa siku hizi kuna nafuu, jiji limepanuka sana, wapo walioacha hizo mila wanaishi na wageni vizuri tu.

(a) Shughuli za mila

Matambiko yote ya hapa Mbeya ni wasafwa wazawa asili wa hili jiji ndio wenye jukumu, Matambiko maarufu ni yale ya mlima wa nyoka na Mteremko wa Mbalizi ambako kunasifika kwa magari mengi kupata ajali, wakifanya matambiko yao huwa ajali zinapungua.

Kiongozi wa kimila anaejulikana zaidi kwa jiji hili ni chifu Rocket Mwashinga wa wasafwa, ndie figure head kwa mambo ya mila ya hapa Mbeya,

(b) Kilimo

Kutokana na wengi kuishi maeneo ya mbali na mji, huko wemeweza kujishughulisha na kilimo, wanasifika zaidi kwa kilimo cha viazi mviringo, mazao mengine ni kama mboga mboga, maharage, n.k.
 
Back
Top Bottom