Lijue Gereza la Kijeshi Hatari zaidi duniani linalofunga hadi Raia la Sednaya lililoko Jijini Damascus nchini Syria

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,036
Ni Gereza linalochukua Wafungwa Elfu Tatu tu ila lina Wafungwa zaidi ya Elfu Ishirini

Ni Gereza la Kijeshi ila linalochukua Raia wa Makosa mbalimbali

Ni Gereza ambalo Wafungwa wakiingia Siku ya Kwanza hufanyiwa Sherehe ya Mateso na Vipigo vikali ambavyo huwafanya Wafungwa hao washindwe Kuona kwa Siku Kumi na Tano kutokana na Maumivu waliyoyapata na waliyonayo

Ni Gereza ambalo kila Siku Wafungwa Hamsini Wanazikwa ( hasa kwa Kuchomwa Moto ) au Miili yao Kutupwa Mitoni na Baharini

Ni Gereza ambalo Wanafunzi wa Udaktari huruhusiwa kwenda bure kufanyia Uchunguzi ( Postmortem ) Miili ya Marehemu badala ya Kuhangaika kuwafanyia Panya kwakuwa Watu wanaokufa huko / humo Gerezani ni Wengi hata kuliko Panya

Ni Gereza ambalo Mtu / Mfungwa akijua anapelekwa huko hulazkmika ama Kujiua Mwenyewe au Kuhonga ili atoroke au apelekws Gereza lingine la afadhali

Ni Gereza ambalo idadi ya Wafungwa wanaotakiwa Kufa kwa Siku hiyo haijatimia ( hakidi haijatosha ) basi haraka sana Wafungwa hulazimishwa Kupigana na Kuumizana hadi Vifo Vitokee na watakaofanikisha hilo Siku hiyo hupewa Chakula Kizuri kama Shukran Kwao

Pongezi ( Credits ) nyingi kwa EFM Radio ( hasa ile Segment yao ) ya Unalijua / Walijua hili ambayo GENTAMYCINE nimeitoa Kwao na Facts zingine baadhi kuzitoa Mtandaoni wa Kulihusu Gereza hili Hatari zaidi duniani ambalo UN na Marekani limeamuru lifungwe na Vitendo hivi vya Ukatili kwa Wafungwa vikome / viachwe mara moja.

Je, na Tanzania tuna Sednaya yetu?
 
Unarekodi huku kazi unaendelea kufanya sikila mtu anasikiliza muda huohuo
Ungeachana nae tu huyo Mnafiki Mkuu. Kuna Watu wanapenda sana Kunizoea na Kunishobokea vibaya sana hapa JamiiForums na bahati nzuri majibu yao Mujarab / Kuntu kabisa ya Kuwapa na Kuwashikisha Adabu huwa ninayo.

Cc: Mr Slim
 
Back
Top Bottom