Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,805
- 1,873
Lijuakali kaonyesha udhaifu mkubwa sana katika hotuba yake bungeni na katika andiko lake juu ya kupatikana kwa ubunge Wake Kilombero 2015 humu JF.
Nikianza na mchango Wake bungeni: Katika mchango Wake kaonyesha hana ujasiri wa kukabiliana na mitikisiko ambayo kwenye siasa ni vitu vya kawaida. Katika dakika takriban 10 alizozungumza kama nisingetajiwa umri Wake ningedhani ana umri wa miaka 11 - 16. Ameuhakikishia umma kuwa aligombea ubunge wa Kilombero kwa lengo la kutafuta ajira tu na sio kuwapigania wananchi. Anasema, ah hata boda boda nitaendesha- kwani aliambiwa kuwa kuendesha boda boda ni dhambi au hao wanaofanya kazi hiyo sio binadamu? Kawadharau vijana wote kwa kudhani kuwa kupata ubunge amepanda daraja la kutofanya kazi nyingine kama boda boda, ukulima, biashara nk.
Hii imedhihirisha kuwa alikinzana na wenzake kwenda bungeni kwa ajili ya POSHO TU. Na kinachomtisha zaidi ni kuelewa kuwa CHADEMA haitamsaidia tena kupata ama udiwani ama ubunge kama si kumtosa. Na biashara ya CCM ya kununua wabunge wa upinzani imefungwa, hivyo kilichobaki ni kumuomba Ndugai ampokee kwa kumuonea huruma bila masherti yeyote yale-buree, huku akitoa machozi danganya.
Kuhusu andiko lake humu JF kaeleza mengi, lakini kubwa ni moja tu kuwa kushinda kwake kulitokana na DC, OCD nk kuwa watu wa Lowasa waliopata maelekezo toka kwa Lowasa na kuyatekeleza. Kama hivyo ndivyo basi kaitukana zaidi CCM kuliko alivyodhani kuwa kaivua nguo CHADEMA. Kwa maana kwa mfano kuelekea uchaguzi 2020 ma-DC, OCD wataje tu mpaka umalize wamechaguliwa na Mwenyekiti wa CCM.
Kwa hiyo kama formula ya mahesabu itakwenda kama yeye alivyosema, inamaanisha chaguzi zote CCM inashinda kwa sababu, hao wazito wote huteuliwa na Mwenyekiti wa CCM/Rais. Arudi nyuma na kujitafakari kauli zake, kwani akutukanae hakuchagulii tusi. Mbaya zaidi anawatukana watu ambao leo amewamba wampokee/ CCM.
Huyu kijana hakustahili kuwa mbunge, kwani anawashushia hadhi wabunge wote vijana. Anatakiwa awaombe radhi vijana wote mara moja.