Ligi yako inakuzwa na Ubora wa Wachezaji wa Kigeni Wewe unawawekea Wachezaji wako Wazawa Wavivu Ahadi ya Tsh Milioni 500

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,621
108,984
Kwa Uganda Taifa langu la Pili Kiuraia (kutokana na Kunilea na Kuishi huko Kimasomo) na ninavyojua Uwekezaji wao katika Michezo na Seriousness yao hata Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ingewekewa Ahadi ya Tsh Bilioni Tano bado tusingewaweza.

Akina Okwi, Owino, Ochan na Wengineo mliowajua hawakuibuka tu kama Uyoga bali walitokea / walijulikana kwa Vipaji vyao tokea wakiwa katika Shule za Upili (Secondary) huko nchini Uganda kisha wakatengenezwa na Makocha mahiri.

Utakuwaje na Timu ya Taifa (Taifa Stars) bora wakati 95% ya Vikosi vya Timu zako Kubwa nchini Tanzania na ambazo ndizo zinatengeneza Wachezaji wa Timu ya Taifa za Simba, Yanga, Azam, Singida nakadhalika First Eleven zao zimetawaliwa na Wachezaji wa Kigeni akina Chama, Mayele, Akaminko na Bruno?

Utakuwaje na Timu ya Taifa Bora wakati 85% ya Makocha wako Wazawa hawajiamini, hawataki Kujaribu fursa nje ya Tanzania na wako tayari kuwa Makocha Wasaidizi kwa Makocha wa Kigeni ambao Wengine wana CV"s sawa na zao?

Kipindi nikiwa Masomoni nchini Uganda 1996 hadi 2002 GENTAMYCINE (najua kuna Mapopoma Watakaobisha na Kutoamini) kwa Kipaji cha Mpira nilichokuwa nacho nikiwa Kidato cha Kwanza tu niliweza Kuitwa Timu za Shule na kubahatika Kucheza Michuano yao Mikubwa ya Shule hali iliyonifanya Kutembelea Mikoa mingi ya nchini Uganda na kujua hasa Mifumo yao ya Kutambua Vipaji, Kuvikuza, Kuviendeleza na hata Kuvitangaza pia.

Taifa Stars (Tanzania) kuifunga Uganda (The Cranes) katika Mechi zetu Mbili zijazo itakuwa ni Bahati tu ila kama Uganda na Wachezaji wa Uganda Wakiamua na Serikali yao ikiwatimizia Wanayotaka au kupewa Ahadi Nono sioni ni wapi Taifa Stars itaifunga The Cranes.

Na katika Mechi hizi Mbili GENTAMYCINE natangaza rasmi hapa hapa kuwa kwakuwa Uganda is my Second Home baada ya Tanzania katika Mechi hizi Mbili nitakuwa Neutral katika Kushangilia na hivi sasa natafuta Mbunifu wa Jezi ili anibunie Jezi ambayo nusu itakuwa ni ya Tanzania (Taifa Stars) na nusu iwe ni ya Uganda (The Cranes)

Ukiununia huu Ukweli Jinyonge Ufe!!!
 
GENTAMYCINE natangaza rasmi hapa hapa kuwa kwakuwa Uganda is my Second Home baada ya Tanzania katika Mechi hizi Mbili nitakuwa Neutral katika Kushangilia na hivi sasa natafuta Mbunifu wa Jezi ili anibunie Jezi ambayo nusu itakuwa ni ya Tanzania ( Taifa Stars ) na nusu iwe ni ya Uganda ( The Cranes )
😂😂Mkuu angalia usijekuwa Kama Don Namilson ,,alianza hivihivi kuukataa utanzania wake
 
Kikubwa ni kuwatia hamasa kama mhe.raisi wetu amewaahidi donge nono endapo watafuzu kwenye AFCON pia wajengewe Imani kubwa kwamba tunaweza ...na sio kuwakatisha tamaa
 
😅😅😅 wanachekesha wqnadhani hamasa inaweza shinda uwezo wa wachezaji!!, Hamasa ni kitu cha mwisho katika mafanikio ya mpira uwanjani. Bila maandalizi madhubuti na uwekezaji mkubwa hata tuwaahidi B moja moja hatutoboi.... Simba imepata matokeo na horoya kupitia wachezaji wa kigeni ...
Chama 3
Baleke 2
Kanoute 2!!
Yanga... Msonda 1
Mayele 1.
 
Huo ndio ukweli, acha waendelee na hamasa waache kuwekeza kwenye academy, umitashumita na umiseta zitiliwe mkazo, mpira hauhitaji uongouongo unahitaji uwekezaji na kukuza vipaji toka watoto wakiwa wadogo mbape hajaibuka tu, waliandaliwa hao tatizo la viongozi ni long term plans hawana ndio maana unaona tunasuasua kila leo
 
Kwa Uganda Taifa langu la Pili Kiuraia (kutokana na Kunilea na Kuishi huko Kimasomo) na ninavyojua Uwekezaji wao katika Michezo na Seriousness yao hata Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ingewekewa Ahadi ya Tsh Bilioni Tano bado tusingewaweza.

Akina Okwi, Owino, Ochan na Wengineo mliowajua hawakuibuka tu kama Uyoga bali walitokea / walijulikana kwa Vipaji vyao tokea wakiwa katika Shule za Upili (Secondary) huko nchini Uganda kisha wakatengenezwa na Makocha mahiri.

Utakuwaje na Timu ya Taifa (Taifa Stars) bora wakati 95% ya Vikosi vya Timu zako Kubwa nchini Tanzania na ambazo ndizo zinatengeneza Wachezaji wa Timu ya Taifa za Simba, Yanga, Azam, Singida nakadhalika First Eleven zao zimetawaliwa na Wachezaji wa Kigeni akina Chama, Mayele, Akaminko na Bruno?

Utakuwaje na Timu ya Taifa Bora wakati 85% ya Makocha wako Wazawa hawajiamini, hawataki Kujaribu fursa nje ya Tanzania na wako tayari kuwa Makocha Wasaidizi kwa Makocha wa Kigeni ambao Wengine wana CV"s sawa na zao?

Kipindi nikiwa Masomoni nchini Uganda 1996 hadi 2002 GENTAMYCINE (najua kuna Mapopoma Watakaobisha na Kutoamini) kwa Kipaji cha Mpira nilichokuwa nacho nikiwa Kidato cha Kwanza tu niliweza Kuitwa Timu za Shule na kubahatika Kucheza Michuano yao Mikubwa ya Shule hali iliyonifanya Kutembelea Mikoa mingi ya nchini Uganda na kujua hasa Mifumo yao ya Kutambua Vipaji, Kuvikuza, Kuviendeleza na hata Kuvitangaza pia.

Taifa Stars (Tanzania) kuifunga Uganda (The Cranes) katika Mechi zetu Mbili zijazo itakuwa ni Bahati tu ila kama Uganda na Wachezaji wa Uganda Wakiamua na Serikali yao ikiwatimizia Wanayotaka au kupewa Ahadi Nono sioni ni wapi Taifa Stars itaifunga The Cranes.

Na katika Mechi hizi Mbili GENTAMYCINE natangaza rasmi hapa hapa kuwa kwakuwa Uganda is my Second Home baada ya Tanzania katika Mechi hizi Mbili nitakuwa Neutral katika Kushangilia na hivi sasa natafuta Mbunifu wa Jezi ili anibunie Jezi ambayo nusu itakuwa ni ya Tanzania (Taifa Stars) na nusu iwe ni ya Uganda (The Cranes)

Ukiununia huu Ukweli Jinyonge Ufe!!!
Naenda kutafuta kamba ya kudu nijining'inize
 
Back
Top Bottom