LHRC Walaani RC Makonda Kuvamia Clouds Media, Wamtaka Rais Magufuli Amwajibishe

Kituo cha sheria na haki za binadamu kupitia kwa mkurugenzi wake mkuu, Dk Helen Kijo-Bisimba amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za RC Makonda kuingia ofisi za Clouds Media akiwa na askari wenye silaha.
Bisimba ametoa wito kwa Serikali imchukulie hatua za kinidhamu na kijinai mkuu huyo wa mkoa.
Serikali imchukulie hatua gani sasa?? inamaana hajamsikia raisi jana kasemaje? Kuna walio juu ya sheria na walio chini ya sheria hilo lieleweke.
 
Kituo cha sheria na haki za binadamu kupitia kwa mkurugenzi wake mkuu, Dk Helen Kijo-Bisimba kimesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za RC Makonda kuingia ofisi za Clouds Media akiwa na askari wenye silaha.

Bisimba ameitaka Serikali imchukulie hatua za kinidhamu na kijinai mkuu huyo wa mkoa ili kukomesha tabia hiyo.

Alitumwa na Magufuli mwenyewe kwhy hakuna hatua itakayochukuliwa
 
Mama Kijo Bisimba amewaasa watanzania kuonyesha hasira zao dhidi ya utawala unaowadharau. Amesikitishwa na kauli ya Mh.Rais kwamba yeye hapangiwi na mtu nini cha kufanya

Bisimba ameenda mbali zaidi na kuwaasa watanzania kuchukua hatua za kuonyesha hasira zao. Moja ya hatua aliyoshauri ni kuacha kufanya kazi na watu hawa.

"Watanzania tuache uwoga....Ni wakati wa kumwondoa Pombe ..Anafanya mambo ya kihuni...Tuache kufanya nae kazi" amesema
- Dk. Kijo-Bisimba, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu!

Ametolea mfano wanapokwenda kwenye mikutano ya wazi watanzania wanaweza kugoma kuhudhuria mikutano yao na kuwaacha viongozi hao peke yao

Source:Ayo Tv
 
Mama Kijo Bisimba amewaasa watanzania kuonyesha hasira zao dhidi ya utawala unaowadharau. Amesikitishwa na kauli ya Mh.Rais kwamba yeye hapangiwi na mtu mini cha kufanya

Bisimba ameenda mbali zaidi na kuwaasa watanzania kuchukua hatua za kuonyesha hasira zao. Moja ya hatua aliyishauri ni kuacha kufanya kazi na watu hawa. Ametolea mfano wanapokwenda kwenye mikutano ya wazi watanzania wanaweza kugoma kuhudhuria mikutano yao na kuwaacha viongozi hao peke yao

Source:Ayo Tv

Anaendeleaje?

Mara ya mwisho nilimsikia kwenye ile ajali...!
 
Huyu mama anaweza kutumbuliwa na sizo kiaina! Anatuambia tusishirikiane na 'mtukufu' sana!!!
 
Labda Rais wa Kenya anaweza kumuwajibisha huyu jamaa wa kwetu amemuagiza achape kazi maana yake yale aliyofanya yana baraka zake na ana weza hata kuzidisha atalindwa.
 
Nadhani kwa umri wake anaelewa kuwa Rais ni taasisi ...awache mambo ya kitoto Kijo.
 
Nadhani kwa umri wake anaelewa kuwa Rais ni taasisi ...awache mambo ya kitoto Kijo.
Kwahiyo kama rais ni taasisi amejichagua mwenyewe? rais lazima awaheshimu walio mchagua, hakuna cha rais taasisi wala nini, tunataka heshima, by the way hanihusu maana siku vote yeye.
 
Nadhani kwa umri wake anaelewa kuwa Rais ni taasisi ...awache mambo ya kitoto Kijo.

Huyu anaelewa Rais ni taasisi ndiyo, ila Rais hilo halijui, anahisi yeye peke yake ndo kila kitu. Bora huyu aongee kuliko Dr.Hasira
 
Nadhani kwa mujibu wa muongozo uliotolewa alichofanya Mkuu wa Mkoa ilikuwa ni moja ya kazi alizotumwa na mwajiri wake na ameagizwa kuchapa kazi zaidi bila kujali huu "umbea" wa mitandao.
 
Mama Kijo Bisimba amewaasa watanzania kuonyesha hasira zao dhidi ya utawala unaowadharau. Amesikitishwa na kauli ya Mh.Rais kwamba yeye hapangiwi na mtu nini cha kufanya

Bisimba ameenda mbali zaidi na kuwaasa watanzania kuchukua hatua za kuonyesha hasira zao. Moja ya hatua aliyoshauri ni kuacha kufanya kazi na watu hawa.

"Watanzania tuache uwoga....Ni wakati wa kumwondoa Pombe ..Anafanya mambo ya kihuni...Tuache kufanya nae kazi" amesema
- Dk. Kijo-Bisimba, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu!

Ametolea mfano wanapokwenda kwenye mikutano ya wazi watanzania wanaweza kugoma kuhudhuria mikutano yao na kuwaacha viongozi hao peke yao

Source:Ayo Tv
LHRC ni chama cha siasa kisicho na usajili,lakini kwa kipindi hiki kipo upande wa CHADEMA. Watanzania wengi tuna imani na Rais Magufuli na Serikali yake,kwa hiyo huyu Kijo Bisimba ndo anapaswa kupingwa kwa kauli zake za kichochezi za kutaka kutugawa Watanzania. Tunajua chuki zake kubwa zinatokana na jina la Lowassa kukatwa CCM na asitegemee kwamba huyo mtu wao atakuja kuwa Rais wa nchi hii.
 
Jansni mbna mnamsakama sana mama wa watu?Hili tamko lingetolewa na Tundu lissu lingekuwa na mashiko sana lkn kwa kuwa amelitoa fulani duh....ndvyo tulivyo wabongo
 
Back
Top Bottom