LHRC Walaani RC Makonda Kuvamia Clouds Media, Wamtaka Rais Magufuli Amwajibishe

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
10,220
29,585

Kituo cha sheria na haki za binadamu kupitia kwa mkurugenzi wake mkuu, Dk Helen Kijo-Bisimba amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za RC Makonda kuingia ofisi za Clouds Media akiwa na askari wenye silaha.
Bisimba ametoa wito kwa Serikali imchukulie hatua za kinidhamu na kijinai mkuu huyo wa mkoa.
 
Rais wangu,
Nadhani kama ilivyo kawaida ya wapambe na watu walio karibu na mfalme hunena "yanayompendeza" tu mfalme.

Huenda wakawa wanakuambia unakubalika sana, unaaminika na unatisha. na huenda wanaenda mbali kwa kukudanganya kuwa ni "kelele" tu za mitandao ya kijamii lakini bado unapendwa.

Ukweli makundi yote yanakusema vibaya, wafanyabiashara, wafanyakazi, wakulima nk.

Kwa Sasa nchi iko ktk sintofahamu, watu wanashindwa kujua kesho yao. tafadhali amini hili japo linauma.

Uchumi mbovu, kukosekana kwa ajira, mishahara hafifu, mamilioni ya vijijini, uhuru wa bunge, kauli za ubabe, kutotoa fursa sawa za kidemokrasia baina ya vyama shindani ni miongoni mwa kero za huku mtaani

Najua hupendi kuamriwa wala kuambiwa ukweli wa aina hii, na pia mitandao ya kijamii kwako si mizuri(kwa maneno yako)

Ila nami nisipokuambia ukweli nahisi kupungukiwa jambo.
 
Serikali inatakiwa kuajiri Madaktari katika Vituo vya Afya na kuongeza madaktari katika Hospitali za Wilaya na Mkoa plus rufaa

HAPA KAZI tu maana yake nini? Kuvamia vituo vya Television?

bahati Nzuri Mungu sio Athumani...CCTV imewaanika uchi hadharani na Dunia imewaona

Sifa za kijinga tu...Benki ya DUNIA kutujengea FLYOVERS kwa mikopo ni jambo la kawaida sana...Ila masikini wa Tanzania ni jambo geni

Watanzania wanakufa kwenye foleni na kuumia zaidi kwa kucheleweshwa matibabu...UHABA WA MADOKTA

Wanafunzi wanafeli kwa waalimu kukosa morali

Wananchi wana njaa...pesa hakuna mtaani...Mfumuko wa bei...Shillingi imeanguka thamani

Mnatuletea sifa za kijinga...Mnajisifu kwa pesa za World Bank? Eboooo
 
well said

ukweli mtupu
 
Abanwe mbavu huyu uchwara mpaka kieleweke.
34187f3b34baa0a84bf9690d54d6d955.jpg

Umeisoma hii short tale mkuu?
 
Serikali inatakiwa kuajiri Madaktari katika Vituo vya Afya na kuongeza madaktari katika Hospitali za Wilaya na Mkoa plus rufaa

HAPA KAZI tu maana yake nini? Kuvamia vituo vya Television?

bahati Nzuri Mungu sio Athumani...CCTV imewaanika uchi hadharani na Dunia imewaona

Sifa za kijinga tu...Benki ya DUNIA kutujengea FLYOVERS kwa mikopo ni jambo la kawaida sana...Ila masikini wa Tanzania ni jambo geni

Watanzania wanakufa kwenye foleni na kuumia zaidi kwa kucheleweshwa matibabu...UHABA WA MADOKTA

Wanafunzi wanafeli kwa waalimu kukosa morali

Wananchi wana njaa...pesa hakuna mtaani...Mfumuko wa bei...Shillingi imeanguka thamani

Mnatuletea sifa za kijinga...Mnajisifu kwa pesa za World Bank? Eboooo

kweli mkuu nimeshangaa Sana sizonje kupeleka madaktari Kenya wakati hapa kwetu tuna uhaba wa madaktari zaidi ya elfu1

walimu Wanapata shida Sana hasa hii ishu ya elimu bure shule inapewa bajet ndogo ya laki Na nusu kwa mwaka apo Kuna stationary mlinzi mpishi maji umeme

Eti

Tanzania ya viwonder
 
Tangu lini wadau wa CHADEMA kumuunga mkono Magufuli,
Watu mna unazi.unafikishwa dar unaambiwa hii ndio dar unasema hapana hii ni Mwanza kisa ni unazi au unaona mwanga kabisa unaambiwa sasa hivi ni mchana unasema hapana ni usiku..penye ukweli tukubali ukweli jamani na tuache kuhusisha mambo ya msingi na sababu zisizo za msingi.Acheni hizo bwana mtu kama amefanya kosa tukubali amefanya kosa aombe radhi maisha yaendelee tusijitahidi kumficha kwenye vichaka ambavyo havina mashiko yoyote..oooh! wanaomshambulia team Membe,ooh ni team Ngada oooh! ni team chadema..ukijaribu kutafuta uhalisia wa hivyo visingizio haupo kabisa.
 
Mange na GWAjima walimpigia kura?Dar walimpa kura ngapi?.Sisi tuliompa kura anatusikiliza....mama endelea kula fedha za wazungu halafu ucheue..
 
Back
Top Bottom