LG TV tatizo la kugoma kuwaka

uzeebusara

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
657
514
Habari zenu wanajf
Naomba msaada kwa mafundi wa tv hususani Lg tv yenye sifa hizi
1. Model no 32LC2D-AA
2. Product code 32LC2D-AA.AAULLBD
3. Power AC 100-240V~50/60Hz 1.5A
4. Serial no 609INNG2C215
5. Manufactured 2006
6. Made in Indonesia
Tatizo
Imekuwa ikitoa mlio wa tick tack pasina kuwaka. Hili tatizo lilianza taratibu kwa kuchelewa kuwaka. Mwanzo nikajua labda umeme mdogo hivyo nikanunua stabilizer ya 1500W lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote ya kuwaka haraka. Ikawa inachelewa kuwaka kama kwa dakika 10, then 20 then 30 na sasa leo siku ya tatu haiwaki kabisaa zaidi ya kuishia kuwasha taa na kuzima huku ikitoa mlio wa tick tack kama video ntaiweka hapo chini inavyoonyesha
Kwa kuwa hili ni jukwa la technolojia naamini ntapata msaada wa mawazo na ufundi ulio bora kabisa. Sijawahi kuipeleka kwa fundi hata hapo katika video niliifungua mwenyewe nikidhani labda vumbi limejaa. Kiumri ina miaka 3 toka niinunue
Niwieni radhi video imekataa kuapload ikifika 90% inaleta error hivyo kuna picha tu
Regards
8021c97c50e26a9158db8dc3abdfa4dc.jpg

75ca39b873b55f08ae972fafb8630e5b.jpg
 
Sasa hiyo ni yakureplace if you bought 10 yrs ago ,then no loss
Sawa mkuu
Lakini malengo kikwazo, huku kuhangaika kujenga huku biashara zenyewe mzunguko kausimamisha Magufuli basi nilitaka kucheki namna nisogeze muda kidogo ilihali mipango mingine iendelee na ratiba kama kawaida
Thanks, ntalifanyia kazi
 
Ndugu mlalamikaji:

Kutokana na maelezo yako, huo mlio wa tick tick huwa unatokea kwenye relay na hiyo ni hali ya protection mode kwamba protection mode is activated. Na protection mode inakuwa active kwasababu zifuatazo:
1. Kuna short circuit kwenye secondary side ya powersupply , shot circuit inaweza kuwa ni transistor/diode/ic/capacitor imeungua.

2. Inawezekana ni capacitor imeharibika na haina uwezo wa kuhifadhi umeme vizuri.

tv kuchelewa kuwaka kunasababishwa na na capacitor/filter ya kwenye psu kuharibika au kupoteza uwezo wake wa kuhifadhi umeme.

Tv huanza kuchelewa kuwaka na mwishowe haiwaki kabisa pale capacitor husika inapokuwa imekufa moja kwa moja.

Ushauri. Tafuta fundi anayejielewa ili asikuongezee tatizo.
 
Pole sana maana na Mimi TV yangu Samsung inatatizo kama lakwako sijui nitapataje fundi wa uhakika nipo Arusha town
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom