Leyla Rashid vs Jokha Kassim, yupi unamkubali?

Yusomwasha

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
2,092
838
Leo tunaye malkia wa jahazi leyla rashidi aka mamake na lujayina.
Ni mwimbaji wa jahazi modern taarab na pia ni mke halali wa mfalme mzee yusuff ambaye ni mkurugenzi na mmiliki wa bendi ya jahazi modern taarab

Pia tuna jokha kassim aka malkia wa Tanzania moto. Modern taarab au t-moto. Joha ameolewa na Amin salmin ambaye pia ndo.mmiliki na mkurugenzi wa bendi ya taarab ya t- moto

Leyla na jokha wamekuwa wakiimbana kwa kupigana vijembe ndani ya nyimbo zao mfano katika nyimbo ya sina mda huo ya leyla, inasemekana kamwiimba joha ambaye naye kaamua kumjibu leyla na jisong la domo la udaku.

Kumekuwepo na vita vya maneno kati ya amin salmin mme wa joha na mzee yussuf mme wa leyla

Pia kumekuwepo kwa majibizano kati ya bendi mbili mfano Amin salmin alimtaja mzee yusuf na jahazi kuwa ni wa binafsi hawatak kunyanyua bendi nyingine

Na mzee naye alijibu kwa kumwiita amin salmin na bendi yake ya t- moto kuwa ni gari bovu hivyo halifai.

Pia tuhuma za ushirikina zimekuwa zikitolewa kati ya hizi bendi mbili yaani jahazi na t- moto

Tupe mtizamo yupi unamkubali kati ya leyla rashidi na jokha kassim?
 
Leyla Rashidi
 

Attachments

  • 1460821940883.jpg
    1460821940883.jpg
    10.7 KB · Views: 367
Leyla
 

Attachments

  • 1460822107559.jpg
    1460822107559.jpg
    5.9 KB · Views: 438
  • 1460822141540.jpg
    1460822141540.jpg
    8.6 KB · Views: 735
Najitahidi kuwapuuza kwa,sababu sababu sitaki stress
Ila najua ndo binadamu mnazua unafiki hamkosi
Nawambia laa hasha tushawachoka kwa mnayoyazusha
Haiwi kila siku mie mniseme mie
Mmekamilika nini nyie au malaika nyie
YAANI HUU WIMBO WA NINA MOYO SIO JIWE WA LEYLA NI HATAREEEE PAMBEE YAAN NIKIRUDI NAKUJA KUENDELEA
 
Jisong lake la nina moyo sio jiwe ni shidaaaa
Najitahidi kuwapuuza kwa,sababu sababu sitaki stress
Ila najua ndo binadamu mnazua unafiki hamkosi
Nawambia laa hasha tushawachoka kwa mnayoyazusha
Haiwi kila siku mie mniseme mie
Mmekamilika nini nyie au malaika nyie
YAANI HUU WIMBO WA NINA MOYO SIO JIWE WA LEYLA NI HATAREEEE PAMBEE YAAN NIKIRUDI NAKUJA KUENDELEA

Huu huu ndio nilikuwa nausemea mimi.
Ni kawimbo flani kafupi lakini katamu.
Nasikia eti no dongo la wifi mtu Khadija Yussufu, kweli eti?
 
Huu huu ndio nilikuwa nausemea mimi.
Ni kawimbo flani kafupi lakini katamu.
Nasikia eti no dongo la wifi mtu Khadija Yussufu, kweli eti?
Hapana ni dongo kwa jokha na amin salmin
Ila sasa hivi leyla na hadija haziivi yaan walichambana instagram.kati ya hadija na team leyla kisa matuc
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom