Leveling na kuanza ujenzi

pedama

JF-Expert Member
May 11, 2015
236
142
Habar zenu. Nimefanya leveling mwez January mwaka huu kwenye kiwanja kilichokuwa na mteremko. Kama haitoshi nimemwaga vifusi kadhaa vya udongo ili kusawazisha kiwanja kile kwan hata baada ya kulevo Bado mteremko uliendelea kuwepo .
Kwa wazoefu na wajuzi Ni muda gani mzuri naweza kuanza ujenzi na kusiwe na athar za kutitia kwa jengo?
 
ishu sio muda boss. Muhimu ni kuwa kama umerudishia udongo ilikupata ‘levo’, basi wakati wa kuchimba msingi hakikisha unaikuta ile ardhi asilia. usichimbe huo udongo uliorudishiwa ukasema ndio umechikba msingi.
 
Hivi kiwanja ulipewa bure au ndio vile vya bei rahisi?
 
Wawekee wataalamu na picha ili wakushauri vizuri namna gani yakufanya
 
ishu sio muda boss. Muhimu ni kuwa kama umerudishia udongo ilikupata ‘levo’, basi wakati wa kuchimba msingi hakikisha unaikuta ile ardhi asilia. usichimbe huo udongo uliorudishiwa ukasema ndio umechikba msingi.
Kumbe sijaokoa kitu nilidhan baada ya levo nitatumia mawe kidogo Sana. Daah sikushaurisha mapema
 
Hivi kiwanja ulipewa bure au ndio vile vya bei rahisi?
Tena nakwambia ni bei mkas Sana. Sema Kiko mtaa niliokuwa nikiupenda. Kwa Sasa ukipaona pako vizur tambalale kabisa. Sema ndo ivyo sikujua mapema athar za kutifua vile
 
Ulifanya kuosa, ungetafuta wataalamu wa ujenzi wangekusaidia sana. Pia punguza gharama kwa kujenga kutokana na eneo lilivo. Unaweka steps tu
 
Mkuu kama ni nyumba kubwa kwa aina ya viwanja hivyo basi amini kwamba utazika nyumba nyingine kwenye msingi tu.

Hapo mbinu nzuri ilikuwa ni kuitafuta level kwa kunyanyua msingi mrefu (kutoka kwenye ardhi halisia uliyoikuta) upande wenye slope mpaka ulingane na ule upande ulioko kwenye muinuko, baada ya hapo yale mashimo marefu yatakayopatikana kwenye partition za msingi ndo ujaze vifusi utakavyo mpaka palingane.

Lakini pia kifusi utakachojaza kwenye hizo partition za msingi kakikisha zinashindiliwa vizuri kabida either kwa kuziacha muda fulani au kama upo vizuri mfukoni na una haraka za kuanza ujemzi, jaza maji mengi kabisa kwenye hizo partition ili udogo utitie vizuri na ujishindilie kisha leta comprassor shindilia tena.

Kama msingi ni wa tofali (nashauri ziwe nchi sita), kabla haujaanza kunyanyua boma basi funga beam na umwage zege, weka PVC halafu anza kupandisha boma sasa.

Kujenge kwenye viwanja vyenye miteremko ni gharama sana ikiwa utataka kujenga nyumba yenye standard, kwakua gharama za kuset msingi tu zinaweza kulingana au kuzudi kabisa gharama za kunyanyua boma kwenye kiwanja ambacho ni tambarare.

NB: Msingi wako upigwe maji ya kutosha na ratio ya cement isiwe ya kinyemela (ndoo 12 ndogo za mchanga kwa mfuko mmoja wa cement)
 
Mkuu kwa swala la muda sio kipaumbele sana...BUT hapo lazima uache for at least miaka 3+ ili ardhi ikae sawa kidogo,,,na hapa ni kwa ujenzi wa nyumba ndogo tu ya kuishi...

Kama uko speed Hakikisha msingi wako unaanzia kwenye Ardhi asilia....

Ukifanikisha hilo anza kujenga...Otherwise usipofika chini msingi utaelea..

Nitakuja na picha
 
Habar zenu. Nimefanya leveling mwez January mwaka huu kwenye kiwanja kilichokuwa na mteremko. Kama haitoshi nimemwaga vifusi kadhaa vya udongo ili kusawazisha kiwanja kile kwan hata baada ya kulevo Bado mteremko uliendelea kuwepo .
Kwa wazoefu na wajuzi Ni muda gani mzuri naweza kuanza ujenzi na kusiwe na athar za kutitia kwa jengo?
Kwa hiyo unataka kukalisha nyumba kwenye huo udongo ulio back fill itakula kwako
 
Habari kaka.

Je, ulitumia engineer au mtaalam wa ujenzi kufanya hilo zoezi?

Nakuhakikishia, umetengeneza changamoto na hapo pesa zaidi itatumika kuitatua.

Kifusi ulichomwanga sio udongo asili hyo ni artificial land, gripping yake sio sio mwaka mmoja, hata hivyo kwa jambo hili muda sio jambo tena.

Kwa ushauri na utendaji wasiliana na wataalam wa Uvimo Civil Group

0629361896 -Kupiga
0753927572 -WhatsApp
Mimi Ni Dada. Asante nitakutafuta kwa ushaur
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom