Nimeanza ujenzi, kaa hapa tujenge pamoja

albab

JF-Expert Member
Jul 6, 2018
1,034
1,999
Miezi kadhaa nyuma niliomba ushari kuhusu ujenzi. Leo narudi tena kwenu. Wazoefu na wajuzi mnisaidie.

Nitatumia tofali za kuchoma na ntajengea tope mpaka lenta ambapo ntamalizia kwa cement (ushauri wa fundi ni kwamba wakati wa upauaji tope halitahimili gonga gonga)

Nimeanza na msingi na kesho nategemea utakamilika ntaleta mrejesho hapa na gharama zake siku zijazo.

Ushauri wenu nauhitaji hapa.

Ukweli ni kwamba sitakua na uwezo wa kujenga hadi kupaua kwa mara moja nilipenda niende kwa steps.

Je, nitunze pesa mpaka zitakapo timia mpaka upauaji?? Au nijenge tu then stage ya upauaji isubiri kwa miezi mnne mpaka mitano?
Ramani niliyopewa ina roof plan ambayo sijaipenda sana je mafundi wa upauaji wanaweza kuja roof plan nzuri baada ya ujenzi kukamilika?

( Uzi huu utakua endelevu nataka uwe motivation kwa vijana wenzangu)

Gharama za MSINGI.

Wakati nanunua kiwanja kulikua na msingi mfupi wa ramani ya vumba viwili so ilinibidi nibomoe
So...

Mawe gari mbili @70,000 = 140000 hapa endapo usingekuepo mzingi ingenilazimu kununua trip 5

Mchanga gari mbili @60,000 = 120000 (huu utatumika mpaka lenta)

Maji (vinatumika visima) kusomba day 8000*3 =24000

Cement 6 20000 = 120000 zimetumika kucover nje na juu ya mawe msingi nimeyumia tope)

Fundi = 250000 (hapa fundi alitoa punguzo kutoka 350000) ametaget ujenzi wa boma apewe kazi (kulinda ofisi)/

Kamba na mambo = 15000 ( hapa fundi aliomba tu na nkampa kutoka na punguzo lake mana hua wanavyo hivi)

Usafi visiki na kubomoa msingi =20000

Kifusi = 50000 ( kipo kwa jirani yangu so nimetumia mahusiano tu) hapa kupunguza gharama ntaanza na shimo (chamber) udongo utatumika kama kifusi pia.

JUMLA 739,000 (KAMA NIKIWEKA NA GHARAMA NDOGO KAMA MAFUTA NK NI 750,000/-

Awamu ya kwanza imeishia hapa tutaendelea awamu yapi

UPDATES:
Baada ya kujenga msingi likaja swala la kujaza kifusi ambapo nilifikiria sana kuja ingehitaji gari 5 mpaka 6 kwa kila gari TSH 65,000/=

So ikanilazimu kuchumba shimo (chamber ya chooo) udongo utakaotolewa utumike kama kifusi.

Gharama ni kama ifuatavyo.
Kuchimba shimo Ft 14 (5*5) =195,000
Tofali 200 =210,000
Cement 4 =80,000
Fundi = 100,000
Wiremesh 1 + nondo mm12(1) +nondo mm 10 (5) + misumari ½ + mabanzi (7) + mbao 14 (za kukodi) + binding wire +maji + nk
GHARAMA ZA SHIMO MPAKA KUFUNIKA 736,000/=

KIFUSI KILIJAZA NA IKABAKI SEHEMU NDOGO SANAAA

NOTE.
KAZI YA KUJAZA KIFUSI NILIIFANYA MWENYEWE .

.............
MAPAKA SASA nimekwama kwenye msingi baada ya kugundua
1.mawe mengi yamesimamishwa badala ya kulazwa
2. Kina kifupi cha msingi japo ardhi ni ngumu ila kinanipa.mashaka.

Baadhi ya mafundi wanashauri niweke bim katika msingi, wengine wanasema hautaleta shida niendelee tu, mmoja alinambia atalaza nondo sehem zenye nyufa hata ndogoo tu itazuia, mwingine akasema nitafute angles muhimu niweke nguzo zitakazo kuja kuungana na bim ya msingi. mpaka sasa nimekwama cha kufanya

Ushauri wenu ni muhimu.... je nianze ujenzi au niimairishe msingi na nitumie mbinu gani kuuimarisha?
Salaaam.

UPDATES 29/10/2021

nitaenda fasta sana....

niliamua kuweka mkanda katika msingi ili kuuimarisha ambapo kila kitu kiligharimu 763,500 hivyo kufanya gharama za msingi kuwa 1,382,500.

nilianza kunyanyua boma mwezi may 2021 kwa awamu mbili....

awamu ya kwanza ilikua kufikia level ya madirisha kozi 4 na mkanda iligharimu TSH 1,705,000/= NA ILIKAMILIKA JUNE 2021

Awamu ya pili ilianza July,2021 ambapo nililenga kukamilisha boma na nilijenga kozi 9 kufikia lenta, then lenta na kumalizia kozi 3 za juu ikinigharimu TSH 3,250,000/=

Mpaka kufika hapo nilitumia tofali 1800+ ivi na nilinunua 2000

kumbuka..... gharama ninazotaja ni jumuishi ya ufundi, mbao kukodi na baadhi kununua, maji, kumwagilia nk.

awamu ya pili ilienda sambamba na kumwaga jamvi na lili gharimu TSH 430,000/=


MPAKA KUFIKIA August, 2021 boma lilikua limekamilika ka jumla ya TSH 7,519,500
inaweza kuwa kuna gharama sikuziweka kama gharama za muda, mafuta ya usafiri nk..... ila hizo ni gharama halisi

Subscribe tujenge wote.

IMG_20210730_173924.jpg


Muendelezo wa nimeanza Ujenzi sehemu ya pili
=========12/02/2022=====

PIA SOMA "NIMEANZA UJENZI" Nimeanza ujenzi, kaa hapa tujenge pamoja



TUENDEE TULIPOISHIA............
bada ysa kukamilisha kwa wamu ya boma niliamu akuvuta nguvu na kujipanga kwa awamu inayo fuata na yafuatayo ilibidi yafanyike katika awamu hiyo
=== kupaua: hapa nilitumia bati kampuni ya KIBOKO baada ya kushindwa bei za alafu na ando ambayo yalikua ni machaguo yangu. jumla ya bati 120 zilitumika na bati moja iligharimu Tsh 30,000/=
zilitumika jumla ya mbao 280 kwa mgawanyo wa 2/2, 2/3, 2/4 na 1/8 kwa bei ya 2500, 4000, 5000 na 11000/= hela ya ufundi ikiwa ni Tsh 650,000/=.

=== blandering ilitumia jumla ya mbao 110 za 2/2 na na chache sana za 2/3 huku hela ya ufundi ikiwa ni Tsh 400,000/=

=== jengo lina madisha 11 (mawili kati ya hayo ni madogo) na milango miwili mbele na nyuma ambapo GRILL moja ya dirisha iligharimu Tsh 115,000/= na Tsh 45,000/= Kwa dirisha ndogo.. mlango mkubwa uligharimu 195,000/= na mdogo 115,000/= gharama za kupachika grill na kujenga hanamu 2 zilikua 120,000/=

=== kilichofuata ilikua ni kuweka miundombinu ya awali ya maji na umeme ambapo kwa miundombinu ya maji vifaaa viligharimu Tsh 270,500/= na ufundi uligharimu 50,000/= huku miundombinu ya umeme vifaa viligharimu 273.000/= na fedha ya ufundi ikiwa ni Tsh 250.000/=
NB. upauaji na kazi zingine zilianza tarehe 5/01/2022 na kukamilika tarehe 5/02/2022 huku shughuli zote zikigharimu jumla ya THS 8,422,000/=. GHARAMA HIZI NI JUMISHI KWA VIFAA VYOTE.

GHARAMA KUU=== 8,422,000+7,519,500 = 15,941,500/=



tukutane awamu ifuatayo. (mwisho kabisaa nitaweka document ikionesha gharama zote ila itabidi kusubiri document hii itaonesha kila kitu ikiwemo majina ya vifaa gharama zake).

View attachment 2159030

View attachment 2159032
 
hongera mkuu, kwa sababu umesema tofali ni za udongo na unajengea udongo sikushauri kujenga boma na ukaliacha kwa muda mrefu bila kupaua maana mvua itakuharibia tofali zako na kuta kwa ujumla, ingekuwa tofali za cement kawaida ningekushauri ujenge boma na kufunga linta kisha uvute pumzi kadri utakavyo alafu upaue hata baadae sana.

Kwa hiyo sasa mimi binafsi nakushauri ujipange kwa hatua zote kwa pamoja, yani ukishapandisha boma basi ulifunike moja kwa moja alafu finishing baadae taratibu.


BTW Kila la kheri
 
hongera mkuu, kwa sababu umesema tofali ni za udongo na unajengea udongo sikushauri kujenga boma na ukaliacha kwa muda mrefu bila kupaua maana mvua itakuharibia tofali zako na kuta kwa ujumla...
Nalifanyia kazi hili pia.

Aina ya ujenzi nitakao ufanya tofali zitawekwa mota ndogooo saanaa (wanaita kulambisa) na kwambali zitaonekana kama zimepangwa
Sababu

Kueppusha ukuta kuyumba kutokana na wingi mota. Pia madhara ya mvua

Kuipa nyumba muonekano

Kupunguza cost katika kuziba mapengo wakati wa plasta

Mrejesho ntauweka hapa.
 
Usingoje hela mpaka kutimia, fanya kupambana upande hapo juu, ukimaliza stages hizo utatamani kwenda stage nyingine zaidi, kujimenga ni mipangao na mipango ni kuchagua
Nalichakata boss
 
Ina vyumba vingapi nyumba nyumba yako ila naona umeibana sana au macho yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom