TANZIA Leung Choi-Sang nyota wa filamu ya kung-fu hustle afariki dunia

TANZIA Leung Choi-Sang nyota wa filamu ya kung-fu hustle afariki dunia

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Ndugu wana jukwaa,

Leo ni siku ya huzuni tunapopokea habari za kuondoka kwa mmoja wa magwiji wa kweli wa filamu za mapigano kutoka Hong Kong—Leung Choi-sang.
i-will-teach-you-photo-u1.jpeg

Kwa wale tuliozaliwa na kukua tukitazama mikanda ya VHS na filamu za kusisimua za miaka ya 70 na 80, Leung hakuwa mwigizaji tu, bali alikuwa nembo ya ufundi na nidhamu ya kutoa vichapo heavy.
images - 2026-01-18T223711.348.jpeg

Kung Fu Hustle: Wengi tutamkumbuka kama "The Beast"—yule mzee mfungwa mwenye nguvu za ajabu ambaye alitikisa hisia za watu alivyomnyoosha Stephen Chow. Hili lilikuwa jukumu lake la kwanza kama adui (villain), na alitupa msisimko usiosahaulika.
images - 2026-01-18T223647.488.jpeg

Enzi za Bruce Lee: Alijipatia umaarufu kwa kuigiza kama Bruce Lee kwenye filamu ya The Dragon Lives Again, na pia alihusika nyuma ya pazia kama mratibu wa mapigano (choreographer) kwenye filamu ya The Tattoo Connection pamoja na filamu zingine kadhaa.
images - 2026-01-18T223640.156.jpeg

Kazi Nyinginezo: Aling'ara katika filamu ni kama My Kung-Fu 12 Kicks pamoja na Magnificent Bodyguards akiwa na Jackie Chan.
1768764388583.jpg

Baada ya kustaafu kwa muda mrefu, alirejea kwa kishindo na kutuonyesha kuwa "chuma ni chuma" hata kikiwa cha zamani. Mwaka 2020, alionekana kwa mara ya mwisho kwenye tamthilia ya Heroes, akituachia urithi wa mwisho wa kipaji chake.
images - 2026-01-18T223711.348.jpeg

Sanaa yake ya mapigano, kasi yake, na uwezo wake wa kuchekesha na kutisha kwa wakati mmoja utabaki mioyoni mwetu daima. Tunapoteza mwalimu, mwigizaji, na shujaa wa kizazi chetu.

Lala salama, "The Beast." 🥋
 
Back
Top Bottom