Lets just COPY & PASTE katiba ya Kenya

Game Theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2006
Posts
8,546
Reaction score
881
Ok, I'll say it naona watu wanasita kulisema but to hell...

Because thats what we are good at. Mfano Tazama Anti- Terrorism laws zetu.Prof Issa Shivji alisema kuwa what we did ni COPY & PASTE ileee PATRIOT ACT ya U.S yaani tumecopy mpaka nukta na kadhalika.


Hili la katiba sioni matatizo yake na kama kuna marekebisho ni machache tuuu kukidhi
Constitution of Kenya - Wikipedia, the free encyclopedia
Tutapunguza gharama na pili as it is majority ya watu wanataka hii katiba mpya (EXCEPT MKONO na MWANSHERIA MKUU BWANA WEREMA...amabo wameenda on the record KUPINGA umuhimu wa Katiba mpya)

Katiba ya Kenya hii hapa:
http://www.tikenya.org/documents/final_draft_constitution2010.pdf


Sababu za WEREMA kukataa hiii katiba mpya ni nyingi lakini mojawapo alijua tutataka kama ya Kenya na kama ikipita, then kuna kipengele hiki kwenye katiba yao ambayo inasema kuwa NOT ONLY majaji wa Mahakama za Kenya itabidi wawe VETTED bali mpaka hao MAWAZIRI so this basically means rais na PM hawawezi kujifungia chumbani kupitia majina then watu mnatangaziwa tuuu....nooo Majina yazima yapitishwe ili kupatikane waadilifu!
 

Ushauri mzuri sana huu! Thank you Great thinker
 
excellent, & that is what we against at, eti mawaziri wote wawe Presidential & state house
appointees, what is this? wanafanya kazi za Ikulu? lazima Bunge liwaridhie, Good job
 

kama wataondoa kipengele cha uwepo wa mahakama ya kadhi . . . sawa tukopi na ku-paste.
 
Ukweli sio kama tuna akiri cc za kukaa na kuandika katiba nzuri kama walivyofanya kenya,mungu ameshatulaani
 
Ni upuuzi usiomithilika kunakiri katiba ya wenzenu bila kujali mazingira yaliyosababisha wao kuwa na katiba hiyo. Watanzania tuna mambo yetu, mazingira yetu na vipaumbele vyetu. Kunakiri katiba ya kenya ni ujinga tena aibu ya karne.
 
Ingelikuwa ni vyema kama tungeliweza kupata nakala ya Ghana ili tulinganishe ....lakini so far ya Katiba ya kenya ipo vizuri.
 

Sikubaliani na hili. Inabidi na sisi tudraft ya kwetu. Circumstances za Kenya na Tanzania are not necessarily the same. And by the way, the link you provided is for the the Proposed CONSTITUTION OF KENYA, not the actual Constitution.
 
Mimi sioni shida kuiga mambo mazuri ila tatizo letu ni kuwa tunajifanya wajuaji sana na ndipo wachakachuaji watakapoingia na kujikuta kwenye yaleyale ya mwaka 1977 halafu tukose pa kukimbilia katiba ya Kenya iko kisasa zaidi hasa kwa mazingira ya East Africa na mbali na hayo wakenya walishatutanguli na wamejifunza kwa mazingira magumu sana hadi wakapata akili za kuwafanya wale matunda waliyo nayo leo.
 
.
acha upuuzi. kila jamii ina matakwa, hulka, silka, malengo, mitazamo na matarajio yake.........
inaelekea mzee hata mitihani darasani ulikuwa una copy na ku paste, ndio ninyi mliokuwa macopy hadi majina.PLEASE.. think as greatly as great thinkers
 
Kwanini tusi copy ya iran au vatican?

Siamini as home of great thinkers alafu watu wanashindwa kuonyesha ugreat thinker wao kwa kufikiri kucopy na kuphest katiba za watu.
shame on you!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kila Nchi hapa duniani iko katika level fulani katika mahitaji ya wananchi wake, demokrasia na mengineo.

Mahitaji ya Kenya yako tofauti na yakwetu, haswa kwenye mambo ya msingi ya kijamii. Sisi tunahitaji kujenga KATIBA yetu kulingana na mahitaji yetu sisi kama watanzania. Iwe inaguza kila sector kulingana na tulipo sasa hivi kisiasa na tunapo hitaji kwenda huko mbele...
 
Tanzania We are looking forward in the coming 10 years to be exceptional among the East African Community
So we need our own constitution to prosper on that.
We can use it to add value but NOT copy and paste.
 
Thread zingine zinatia kinyaa. kwani siku zote tunadai katiba ya kigeni au katiba mpya? Haya mambo ya kuiga ndo yanayotugarimu, kumbuka hii tuliyonayo ni ya kucopy. Think twice man/woman
 
Wewe jamaa inaonekana ni mzee wa kudesa. Kila kitu unadesa tu. Hii ni aibu. Utadesa mpaka sumu, shauri yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…