Mapengo 17
R I P
- Mar 28, 2014
- 1,228
- 618
Nimepata taarifa kutoka kwa mmoja wa rafiki zangu aliyepo Dar es Salaam, ameniambia kwamba Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Leticia Nyerere, amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tangu awali mbunge huyo alisakamwa na maneno mengi kutoka kwa viongozi wa Chadema akiwemo kwamba aachane na ubunge ndani ya Chadema ili ajiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuliko kuendelea kukipigia debe chama hicho akiwa upinzani.
Hata hivyo, mbunge huyo anadaiwa kufanya matendo ya kujipendekeza kwa CCM kabla ya kujiengua na chama chake cha awali.

![]()
Mbunge wa Viti maalumu Chadema mkoani Mara, Leticia Nyerere, (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam jana kuhusu kuhama kutoka chama chake cha chadema na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kulia ni mtoto wake,Helena Nyerere na Julia Nyerere.