Let me adress the unadressable: Jesuits & mapadri

una point lakini...pengine mshana anazungumzia maisha aliyoishi seminari kipindi hicho baadae akagundua hana wito wa kuwa pandre....
Kuna seminary ndogo na kubwa. Malezi pamoja na masomo yote toka uingie seminary kubwa si chini ya miaka saba ndio ufikie ushemasi. Na utakaa mwaka tena kama mchungaji ndio ifikie hiyo hatua mshana anaita ordination. Na hicho kiwango kuna wananaojifunza hadi miaka kumi na moja. Mpaka hapo mshana katudanganya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uliisha wahi kusikia au kuona au hata kusoma kwenye maandishi ya Dr. Wilbrod Slaa akijitambulisha kama Padree/askofu etc?
Dr. Wilbroad Slaa ni Padri wa Kanisa Katoliki, hajawahi kuwa Askofu ila amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Wakatoliki Tanzania (TEC).

Haijalishi kama anajitambulisha au la, lakini Sakramenti ya upadre aliyoipokea haifutwi kwa kuwa aliomba kuacha kutoa huduma. Yule bado ni Padri, ambaye anaweza kutoa huduma kama padri katika mazingira fulani fulani.

Unapopewa Sakramenti za Kanisa (Ubatizo, upadre, ndoa, n.k.) haziondolewi na kitu chochote.

Ndio maana, kwa mfano, kama John amemuoa Anna kwa ndoa ya Kikatoliki, halafu akamuacha (kwa sababu yoyote ile) akampenda Elizabeth na akataka kufunga naye ndoa, Anna anaruhusiwa kuwawekea kipingamizi, na hiyo ndoa ya John na Elizabeth haitafungwa.

Kwanini hiyo ndoa isifungwe? Kwa sababu Kanisa linatambua Sakramenti ya ndoa Kati ya John na Anna ambayo ni ya milele. John bado yupo kwenye ndoa na Anna ambaye aliapa kumpenda mpaka kifo.

Kwahiyo Mkuu, hili suala halipo kwa mapadre tu, lipo kwa Sakramenti zote.
 
Tupe uthibitishoau ushahidi kuwa kuna point of no return.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Foundation course miaka 2
Samanera 3 years
Full monk 2 years... Jumla 7
Kwenye utawa point of no return hufikiwa kwa kuweka nadhiri za milele.

Hatua hii unaifikia miaka kadhaa (kwa mashirika mengi huwa 10 japo kila shirika na Jimbo lina utaratibu wake) baada ya kuwa mtawa.

Unataka kutuambia na wewe ni mtawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Point sana hii. Nakuunga mikono yote.
 
Hahahaaa mchana umenifurahisha kweli.
Foundation course miaka 2
Samanera 3 years
Full monk 2 years... Jumla 7

Sent using Jamii Forums mobile app
Ili tujue unaelewa unachosema tutajie hiyo foundation coarse inaitwaje?

Kabla ya kutoka ulikuwa umeweka nadhiri yoyote na ni mara ngapi?

Ulikuwa shirika gani (which congrigation)

Hiyo hatua ya mwisho uliyotoka inaitwaje?

Na ni wapi?

Hii nakuruhusu ugugo kabisa maana najua hutapata majibu sahihi na ndio uthibitisho unatuingiza chaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kumbe Budha du haya basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Understood
 
Waislam tumekatazwa kuupokea ushahidi wowote unaoletwa na mwanamke mmoja, mbona husikii lakini wewe?
Au unataka kusema hizo ni hadithi tu na Quaran haijaandika hivyo ndio maana unaendelea kushupaza shingo.
Cha ajabu kujibu hoja zake hamuwezi. Halafu anaweka ushahidi wa vyanzo vyake vya habari.
Kumbe Hilo Guardian la Uingereza ni gazeti la mwanamke? Una ushahidi kwa Hilo?
 
Nimejifunza na kuishi utawa kwa miaka 5 na kukamilisha hatua mbili muhimu... Hatua ya tatu ndio ingekuwa a point of no return! Ningeifanya ile sijui leo hii ningekuwa wapi[emoji848][emoji144]

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungekua mtumishi wa Mungu tena mwenye wafuasi wengi sana. Ila hata sasa hapa jf wito wako bado upo na unatambulika mkuu Mshana Jr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…