Let me adress the unadressable: Jesuits & mapadri

Let me adress the unadressable: Jesuits & mapadri

nilijua utaanza Kwa kuuliza padri anakuwaje shehe?
unaweza kukuta hata Imani unayojitutumia humu umepewa na imam padri Kwa Mujibu wa Mada.
Aliyebariki UTUME wa Muhamadi ni padre, abishe Faiza ili tulete ushahidi. RC ni noumer, they are the one running this world
 
Hii ni moja ya conspiracy theories ambazo tumezoea kuzisikia kwa msiolijua Kanisa Katoliki. Unasimuliwa vihadithi huko mtaani halafu ndio unavibeba kama vilivyo unatuletea hapa.

Upadri ukiusomea kuna stage inafika inaitwa no return stage, in that stage unaambiwa kabisa...wait kwanza.
Kama unajua, kuna Sakramenti tatu za Kanisa Katoliki ukishazipokea, tunasema haziondoki. Zinaacha alama ya milele, isiyofutika. Mfano: ukipewa Kipaimara, hauwezi kukiondoa kokote; ukishabatizwa, wewe ni Mkristu wa milele hivyohivyo kwa Sakramenti nyingine ikiwemo upadre. Na kwa upadre, ni mapdre wote, sio kwa Jesuits pekee. Huu ulioandika ni upotoshaji.

Ukienda kusoma unapopanda madegree mpaka Vatican huwa kuna stage. Sasa inafika unaambiwa the true face of Catholicism na unaambiwa kabisa who is our god, our plans for this world, who are our enemies na mambo mengine kedekede. At that stage inakuwa too late huwezi tena kuacha.
Haya ni mambo ambayo kila mtu anayajua. Hizo hatua wanazozipitia Jesuits ndio almost wanazozipitia mapadre wa majimbo na mashirika yote duniani kote. Kila Jimbo na shirika lina utaratibu wake, lakini mapadre wote ni lazima wapitie malezi, wasome falsafa (diploma au shahada), wasome theolojia (diploma au shahada), wapitie mwaka wa uchungaji, wapewe ushemasi ndio wawe mapadri. Shida haujui na unaandika mambo usiyoyajua. Unapotosha.

ipo true na ni fact kuwa huwezi kuacha upadri, hata uzini, uue, uibe unaweza ukafukuzwa kazi lakini utaendelea kukaa sehemu malumu ukichungwa na kuendelea kulipwa, lakini siyo kurudi mtaani na kuanza mishe za boda boda, hata ukirudi mtaani watakua wanakuchunga sana
Dhambi haiondoi Sakramenti. Kwahiyo hata ukiua au kuzini, au kuiba bado utaendelea kuwa Padri (kupitia Sakramenti ya Upadre), utaendelea kuwa mwanandoa (kupitia Sakramenti ya Ndoa) utaendelea kuwa Mkristu (kupitia Sakramenti ya Ubatizo), n.k. Acha upotoshaji.

Mapdre wote huwa hawalipwi. Na ikitokea ukaacha kutoa huduma za Kipadre, maana yake unajitegemea kwa kila kitu. Ndio maana akina Padri Slaa unawaona wanapambana na hali zao.

JESUITS: Hii organization ipo ndani ya dini
Ndio. Majimbo yote na mashirika, ambayo kimsingi ndiyo hulea na kutoa mapadre, yapo ndani na chini ya Kanisa Katoliki.

maana kazi ya padri ni kuhakikisha anashika raia wengi kanisani
Uongo mwingine ambao kila siku tunaupinga humu. Nani ameshaona mtu ameshikwa eti kisa ameungama kwa Padri, huyo mtu, atoe ushuhuda na uthibitisho humu. Acheni uongo.

hawa CIA kazi yao ni kudeal na affairs za kikanisa nje ya kanisa. Hawa ndo wanakuwa marais, mashehe, wachungaji, wanasiasa, wanamziki, wafanyabiashara wakubwa n.k n.k
Kwanza CIA ni shirika la ujasusi la Marekani linalohusika na mambo ya intelijensia na ujasusi nje ya ardhi ya Marekani. Halina uhusiano wa aina na namna yoyote ile na Kanisa Katoliki.

Ukishakuwa mchungaji, au sheikh, n.k. maana yake unapingana na mafundisho walau ya Mama Kanisa. Hiyo inapelekea excommunication. Ukiwa excommunicated maana yake umejitenga na Kanisa. Wewe inahesabika kuwa sawa na mpagani. Kwahiyo hii hoja yako inakosa mashiko automatically. Unachotaka kutuambia wewe, kwa hoja hii, ni kuwa Jesuits sio Wakatoliki, kitu ambacho sio kweli.

Ninaomba mleta uzi uwe unafanya utafiti kabla ya kuanzisha uzi, tena kwenye jukwaa hili tunaloliheshimu. Mambo uliyoyaleta, hata kwa Mkatoliki wa kawaida tu ambaye anajua taratibu hizi ndogondogo za Kanisa, atakushangaa sana.

Umeleta upotoshaji tu. Inaonekana umeandika kitu usichokijua. Shame on you!
 
Nimejifunza na kuishi utawa kwa miaka 5 na kukamilisha hatua mbili muhimu... Hatua ya tatu ndio ingekuwa a point of no return! Ningeifanya ile sijui leo hii ningekuwa wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye utawa point of no return hufikiwa kwa kuweka nadhiri za milele.

Hatua hii unaifikia miaka kadhaa (kwa mashirika mengi huwa 10 japo kila shirika na Jimbo lina utaratibu wake) baada ya kuwa mtawa.

Unataka kutuambia na wewe ni mtawa?
 
Nimekaa kwa zaidi ya miaka saba kwa ukaribu sana na hawa Mapadre, mabruda na masister wa kikatholic....
Aisee hawa jamaa wote wana character flan moja ambapo huwa najiuliza sana!!! Ni coincidence tu wote kua na tabia hiyo moja au ni mafundisho!!??

Ni hivi, hawa watu bhana, wanapenda sana kujifanya wakarimu, wana huruma sana kwa binadamu na wanapenda kusmile na kucheka na watu........lakin ukikaa kuwachunguza kwa umakini wa jicho na upembuzi thabiti, utagundua hawa jamaa ni wana roho mbaya mbaya na ya kikatili sijapata kuona.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una uhakika watu wa kawaida, wasiokuwa mapadre au watawa, hawana hii tabia?
 
Ukiwa close sana na padri then maybe then anaweza kukupa siri hizi...but hauwezi kiacha upadri kama vile ambavyo hauwezi kuacha usalama wa taifa uende kuuza nyanya.
Lakini pia hauwezi kuacha upadre, kama ambavyo hauwezi kuacha ndoa ya Kikatoliki ukishafunga.

Hii hata sio siri, kila Mkatoliki anaijua.
 
Nimejifunza na kuishi utawa kwa miaka 5 na kukamilisha hatua mbili muhimu... Hatua ya tatu ndio ingekuwa a point of no return! Ningeifanya ile sijui leo hii ningekuwa wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilibakiza ordination tuu... Nimeishi maisha ya upadri kwa miaka 5+ shida ni kwamba haikuwa upadri wa kumwamini Mungu mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeanza ukasomea utawa na ukawa mtawa kwa muda wa miaka mitano. Hii maana yake ulitumia zaidi ya miaka kumi huko kwenye utawa.

Then ukasomea upadre, ukaupata na ukauishi kwa miaka mingine mitano. Maana yake ukatumia miaka zaidi ya kumi na mbili (walau) huko kwenye upadre.

Kama ulifanya kwa shirika lenye vyote utawa na upadre, utakuwa umetumia si chini ya miaka kumi na mitano kwa utawa na upadre.

Una umri gani Mkuu? Maana hapo bado sijaunganisha miaka mingine uliyodai ulikaa Afrika Kusini kwenye Ubudha.
 
Mshana Jr; kumbe aliyasema mleta UZI ni kweli kuwahusu mapadri? Aise???? Ndio maana Padree Kalugendo alichukua Zaidi ya miaka 20 kuoa since aachane na day to day activities za kanisa ingawa pamoja na kuachana na hizo activities, stil mitaani na maandiko yake alikua akijitambulisha kama padre. Noma sana RC
Upadre ni alama isiyofutika. Ukishakuwa Padre, wewe ni Padre milele. Hivyohivyo kwa Sakramenti nyingine zote ikiwemo ndoa na upadre.

Alichokifanya Kalugendo ni kuondolewa mamlaka ya kutoa huduma za Kipadre. Kuna utaratibu lazima uufuate, lakini sio lazima utumie miaka ishirini. Mbona Padre Wilbroad Slaa ilimchukua chini ya miaka mitano?

Hiyo haipo kwa upadre tu; ni kwa Sakramenti zote za Kanisa Katoliki. Shida mnajadili mambo msiyoyajua. Na nimeshangaaa kugundua kuwa Mshana Jr naye huwa anatudanganya tu kumbe.
 
Upadre ni alama isiyofutika. Ukishakuwa Padre, wewe ni Padre milele. Hivyohivyo kwa Sakramenti nyingine zote ikiwemo ndoa na upadre.

Alichokifanya Kalugendo ni kuondolewa mamlaka ya kutoa huduma za Kipadre. Kuna utaratibu lazima uufuate, lakini sio lazima utumie miaka ishirini. Mbona Padre Wilbroad Slaa ilimchukua chini ya miaka mitano?

Hiyo haipo kwa upadre tu; ni kwa Sakramenti zote za Kanisa Katoliki. Shida mnajadili mambo msiyoyajua. Na nimeshangaaa kugundua kuwa Mshana Jr naye huwa anatudanganya tu kumbe.

una point lakini...pengine mshana anazungumzia maisha aliyoishi seminari kipindi hicho baadae akagundua hana wito wa kuwa pandre....
 
Kama unajua, Sakramenti zote za Kanisa Katoliki ukishazipokea, tunasema haziondoki. Zinaacha alama ya milele, isiyofutika. Mfano: ukishafunga ndoa, hauwezi kuifungua kokote; ukishabatizwa, wewe ni Mkristu wa milele hivyohivyo kwa Sakramenti nyingine ikiwemo upadre. Na kwa upadre, ni mapdre wote, sio kwa Jesuits pekee. Huu ulioandika ni upotoshaji.
Sema wewe nimekupendea kitu kimoja..wewe ni muungwana lakini usiejua vingi hivyo points zako hazinipingi direct kwasababu haujajaribu kupotosha.
Points zote umebase maelezo ya sakramenti n.k n.k
Sasa nakujibu hivi,vipi mke wako akifa? Hauruhusiwi kuoa mwingine??
Vipi sasa imani yako katika kanisa ikifa?? Hauruhusiwi kubadili dini wewe kama padri?
Point is hao mapadri wana siri nyingi na zinalindwa by all costs including death threats.

Ukishakuwa mchungaji, au sheikh, n.k. maana yake unapingana na mafundisho walau ya Mama Kanisa. Hiyo inapelekea excommunication. Ukiwa excommunicated maana yake umejitenga na Kanisa. Wewe inahesabika kuwa sawa na mpagani. Kwahiyo hii hoja yako inakosa mashiko automatically. Unachotaka kutuambia wewe, kwa hoja hii, ni kuwa Jesuits sio Wakatoliki, kitu ambacho sio kweli.
!

Hii ndo the only point iliyojaribu kupinga sasa kuhusu jesuits; hao wanaoperate in shadows,a secret society if i may,
Sasa hao wanaweza kufanya chochote na wasiwe excommunicated.... Hivyo hio sio point kwasababu hawa jamaa hawafanyi kazi zao openly kila mtu ajue kuwa sheikh flan ni jesuit au ni mroma, but wanaoperate undercover ndiyo maana katiba yao inakataza mtu yeyote mwenye background ya kiislam (hata kama babu yake na babu yake alikuwa muislam) kuja kuwa jesuit
Unahisi kwanini?? Na lengo kuu la hii society ni nini?
 
una point lakini...pengine mshana anazungumzia maisha aliyoishi seminari kipindi hicho baadae akagundua hana wito wa kuwa pandre....
Amesema "ameishi utawa"; maana yake aliufikia utawa. Otherwise angesema "alisomea utawa."

Baada ya hapo akasema tena kuwa "ameishi upadre". Maana yake alisomea hadi akawa Padri. Tofauti na hapo angesema "amesomea upadre".

Mshana Jr ni muelewa, anajua tofauti ya kusomea kitu fulani kwa muda fulani na kuishi kitu fulani kwa muda fulani. Angekuwa mtu mwingine sawa.

Ila kwa huyu jamaa, hapana. Anajua anachokiongea.
 
Inawezekana ni conspiracy theories tu.lakini shida inakuja ni kwanini kuwe na 'point of no return' kwanini kuwe na tahadhari kubwa kiasi hicho wakati wanajua fika hata Hugo anayetaka kuwa padri ni binadamu tu kama wanadamu wengine na huenda siku moja akakosea na akakengeuka miiko ya imani hiyo!?
Nadhani ingekuwa tu onyo la kawaida kwamba ukifanya hili na hili unatoka katika imani hii,nadhani pengine kuna madhara makubwa humfika mtu endapo atatoka katika imani zao,na hapo ndo nnapoamini hili andiko.
 
Amesema "ameishi utawa"; maana yake aliufikia utawa. Otherwise angesema "alisomea utawa."

Baada ya hapo akasema tena kuwa "ameishi upadre". Maana yake alisomea hadi akawa Padri. Tofauti na hapo angesema "amesomea upadre".

Mshana Jr ni muelewa, anajua tofauti ya kusomea kitu fulani kwa muda fulani na kuishi kitu fulani kwa muda fulani. Angekuwa mtu mwingine sawa.

Ila kwa huyu jamaa, hapana. Anajua anachokiongea.
We jamaa complicator sana...mbona kila mtu kamuelewa kuwa alimaanisha alisomea...
Hizi lugha sometimes tunaandika kwa mazoea tu mkuu
 
Sasa nakujibu hivi,vipi mke wako akifa? Hauruhusiwi kuoa mwingine??
Mwenzi mmoja akifariki, Mama Kanisa anamruhusu mwenzi aliyebaki kuoa, au kuwa Padre au kuwa mtawa. Hii haina athari hasi kwenye uhusiano wa mtu husika na Kanisa. Bado ataendelea kuwa Mwanakanisa.

Vipi sasa imani yako katika kanisa ikifa?? Hauruhusiwi kubadili dini wewe kama padri?
Kanisa Katoliki haliruhusu kubadili imani. Ukiibadili ni kwa matashi yako, lakini Kanisa halitakuunga mkono. Ndio maana akina Martin Luther walijitenga na Kanisa Katoliki japo Kanisa halikuwaunga mkono. Na hii huwaletea excommunication wale wote wanaojitenga na kuhama dini. Wanavunja Ushirika na Mama Kanisa.

Point is hao mapadri wana siri nyingi na zinalindwa by all costs including death threats.
Hakuna death threats wanazozipata mapadre. Mbona wanajitenga mara kwa mara na wanaendelea na maisha yao tu ya kawaida? Kanisa Katoliki ni takatifu, linapinga kifo. Haliwezi kumlazimisha mtu kuwa Padri au kuwa Mkatoliki.

sasa kuhusu jesuits; hao wanaoperate in shadows,a secret society if i may,
Si kweli. Wapo mbona na wanafanya kazi kama mapadre wengine? Sisi tunawaona huku kila siku na wanatupa huduma za kiroho. Wapo huko Dar (wanajulikana), wapo huku Mwanza (wanajulikana), wapo pale Dodoma (wanajulikana), na kwingineko.

Sasa hao wanaweza kufanya chochote na wasiwe excommunicated...
Excommunication inakuwa automatic, sio kwamba unaletewa barua. Mtu binafsi unajipima tu. Kwa mfano; ukitoa au kushiriki kutoa mimba unakuwa excommunicated. Je, ulishaona mtu amepelekewa barua kuwa amekuwa excommunicated kwa kuwa ametoa mimba? Unajiongeza tu wewe mwenyewe. Kwahiyo hata mapadre, sheria ni zilezile.

Hivyo hio sio point kwasababu hawa jamaa hawafanyi kazi zao openly kila mtu ajue kuwa sheikh flan ni jesuit au ni mroma, but wanaoperate undercover
Akishakuwa sheikh tu, huyo sio Padre tena na anakuwa Hana Ushirika na Mama Kanisa.

ndiyo maana katiba yao inakataza mtu yeyote mwenye background ya kiislam (hata kama babu yake na babu yake alikuwa muislam) kuja kuwa jesuit
Unahisi kwanini?? Na lengo kuu la hii society ni nini?
Sasa kama mnadai Uislam ulianzishwa na Kanisa Katoliki, kwa nini tena Kanisa likatae kuwatumia watu wa imani ileile lililoianzisha?
 
Sijui msukumo wako wa kuandika haya, kama kuwakosoa wakatoliki, subiri kwanza.

Kwanza hutakiwi kusimuliwa na watu huko ukaja kwenye umma na ujasiri wakukosemea yasadikiwayo kuwa siri za taasisi namba moja duniani.

Huo umuhimu ulojipa wa kuwa hatarini baada ya kuandika haya, unajidanganya. Hakuna mtu atakufuata wewe wakati umeandika hadithi za vijiweni. Kama wewe ni kijana mdogo ujue kuna wazee wamesikia hizi hadithi wakiwa vijana vijiweni.

Pia, kama ungependa kuelewa wakatoliki fanya bidii ujifunze kutoka kwao na si kumezeshwa hadithi mahali.

Vipo vitabu vya hizi conspiracy pia ambao wao wameenda deep kuliko ulichokiandika wewe. Kama umejikita huko bora ukajisomea zaidi.

Mwisho, 'laiti ungelijua ya kuyafanya yapaso amani na heri' ungeukomboa wakati. Kama ni mkristo hebu tafakari umepungua kiasi gani kabla ya kuanza kurekebisha mifumo ya makanisa mengine. Kama muislam hivyo hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom