Leo Yanga kabebwa kesho zamu ya Simba

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,798
Swala la Simba na Yanga kubebwa na marefa ni kitu endelevu na haitatokea siku itaisha. Leo Simba wanawazomea Yanga kwa kupewa penati isiyo ya halali kesho hao hao Simba watafunga goli la offside ya wazi dhidi ya kitimu fulani.

Anayepinga aingie YouTube atapata majibu. Kuna ile mechi ya Yanga na Azam mpira ulitoka refa akaacha baadae likawa goli, vile vile mechi ya Prison na Simba Mbeya Kibu Denis akiwa offside aliurudisha ndani mpira uliokuwa umetoka na Mkude akafunga.Huu ndio ukweli wasiopenda kuusikia mashabiki wa hizi timu kongwe.

Kila mtu anaezaliwa nchi hii, eitha ni Simba au Yanga. Hata kama hafuatilii mpira ila kimoyomoyo kuna moja kati ya hizi timu itamvutia. Ndivyo ilivyo hata kwa marefa wetu nao wamechagua upande toka walipozaliwa.

Kama Rais wa TFF mwenyewe anashutumiwa kuipendelea moja ya hizi timu sembuse marefa? Thubutu! Simba na Yanga kubebwa na marefa ni mwendo wa kupokezana leo Doto, kesho Kulwa sema atakayekuwa vibaya kwenye hicho kipindi ndo atahisi mwenzake anahonga marefa.

Subirini kituko kingine kesho.
 
Tatizo ni marefa wa huko nje watabeba? Unless mipango ni kufanikiwa ndani tu.
 
wee mbona hayo makundi ya CAF hugusi, au wee makundi kwako n tsup na telegram tyuuuh.

Byuti byuti.
Yanga FC huwa hawataki kabisa kuwa wasindikizaji bora ila one day yes ni 1 kwa 1 makundi, robo fainali, nusu fainali, fainali yenyewe na kuchukua kombe la CAF mazima
 
Hebu weka hapa tuone redio
Unataka lipi, Goli la Mkude, au la Geita dhidi ya Simba ambalo nalo lilikataliwa bila Sababu, Au Penalty ya Simba dhidi ya Yanga ambayo kagele alichezewa faul nje ya 18 na Yondani Refa aka amulu mkwaju wa Penalty. Au tukio la Kibu Denis ku udaka mpira akiwa katika lango lake akigomea sipigwe kanzu dhidi ya Azam?
 
Unataka lipo, Goli la Mkude, au la Geita dhidi ya Simba ambalo nalo lilikataliwa bila Sababu, Au Penalty ya Simba dhidi ya Yanga ambayo kagele alichezewa faul nje ya 18 na Yondani Refa aka amulu mkwaju wa Penalty. Au tukio la Kibu Denis ku udaka mpira akiwa katika lango lake akigomea sipigwe kanzu dhidi ya Azam?
Achana nayo hayo Makolokolo FC, kwanza laiti yangejua jinsi mwaka jana Mayele alivyonyimwa magoli halali ya kutosha hadi alikosa kiatu cha dhahabu wala yasingenung'unika.

Tatizo ni Makolokolo/mbumbumbu/Malalamiko/Makelele FC ndiyomaana hayana jinsi
 
Unataka lipi, Goli la Mkude, au la Geita dhidi ya Simba ambalo nalo lilikataliwa bila Sababu, Au Penalty ya Simba dhidi ya Yanga ambayo kagele alichezewa faul nje ya 18 na Yondani Refa aka amulu mkwaju wa Penalty. Au tukio la Kibu Denis ku udaka mpira akiwa katika lango lake akigomea sipigwe kanzu dhidi ya Azam?
Kajitia upofu. Hawezi kukujibu hata kidogo. Na hakuna kolo wa kusogeza pua hapa. Akisahau hiyo, mpe ile dhid ya Prisons mbeya kwanza last season.

Mayele alivyonyimwa magoli: vs geita, vs mbeya city, vs mtibwa n.k walishangilia sana.
 
IMG-20221029-WA0205.jpg
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu pole sana
Kajitia upofu. Hawezi kukujibu hata kidogo. Na hakuna kolo wa kusogeza pua hapa. Akisahau hiyo, mpe ile dhid ya Prisons mbeya kwanza last season.

Mayele alivyonyimwa magoli: vs geita, vs mbeya city, vs mtibwa n.k walishangilia sana.
 
SIMBA inajiweza kujibeba haihitaji mbeleko ndio maana iko kimataifa zaidi

Mzee umeandika kama shabiki na sio mpenzi wa mpira...

Marefa wa kibongo wanazingua sana kwenye kutafsiri sheria, kupeta zinapocheza timu kubwa hizo n.k
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom