Leo Yanga kabebwa kesho zamu ya Simba

Mzee umeandika kama shabiki na sio mpenzi wa mpira...

Marefa wa kibongo wanazingua sana kwenye kutafsiri sheria, kupeta zinapocheza timu kubwa hizo n.k
IMG-20221029-WA0178.jpg
 
Mwisho wa kituo chenu Makolokolo FC ni makundi, sana sana mkijiita IDI ni robo fainali.

Endeleeni kuwa wasindikizaji bora wa CAF
alafu ujue wewe kima kuingia tuu makundi unavuna almost 1.5 bilioni, kuingia robo almost 2.4 bilioni sasa huoni kama huna akili jamaa yangu???
 
Swala la Simba na Yanga kubebwa na marefa ni kitu endelevu na haitatokea siku itaisha. Leo Simba wanawazomea Yanga kwa kupewa penati isiyo ya halali kesho hao hao Simba watafunga goli la offside ya wazi dhidi ya kitimu fulani.

Anayepinga aingie YouTube atapata majibu. Kuna ile mechi ya Yanga na Azam mpira ulitoka refa akaacha baadae likawa goli, vile vile mechi ya Prison na Simba Mbeya Kibu Denis akiwa offside aliurudisha ndani mpira uliokuwa umetoka na Mkude akafunga.Huu ndio ukweli wasiopenda kuusikia mashabiki wa hizi timu kongwe.

Kila mtu anaezaliwa nchi hii, eitha ni Simba au Yanga. Hata kama hafuatilii mpira ila kimoyomoyo kuna moja kati ya hizi timu itamvutia. Ndivyo ilivyo hata kwa marefa wetu nao wamechagua upande toka walipozaliwa.

Kama Rais wa TFF mwenyewe anashutumiwa kuipendelea moja ya hizi timu sembuse marefa? Thubutu! Simba na Yanga kubebwa na marefa ni mwendo wa kupokezana leo Doto, kesho Kulwa sema atakayekuwa vibaya kwenye hicho kipindi ndo atahisi mwenzake anahonga marefa.

Subirini kituko kingine kesho.
usijizime data,zamu ya Simba ilishapita tena ilikuwa ni zamu kuu kuliko hata hii ya Yanga. mikia inajifanya misahaulifu sana ila sisi tuna-deal na maktaba za kidigitali.
 

Attachments

  • VID-20221030-WA0005.mp4
    1.6 MB
Back
Top Bottom