Leo tena Yesu amenitendea muujiza mkubwa!

Leo tena Yesu amenitendea muujiza mkubwa!

Kwa zaidi ya wiki moja nimekuwa nikihisi kana kwamba kuna mdudu anatambaa tambaa kwenye bega langu la kushoto. Nikipapasa sehemu hiyo sioni kitu. Leo nikasema "enough is enough"(yatosha sasa). Nikaweka mkono sehemu hiyo na kuikemea hali hiyo kwa Jina la Yesu. Hivi sasa hali ya mdudu kutambaa tambaa imetoweka kabisa katika eneo hilo! Hakika Yesu hajabadilika. Miujiza aliyoitenda miaka 2000+ iliyopita bado anaitenda hata leo kwa kila aaminiye.

Kisayansi, wenye dalili kama hizo, huambiwa kwamba wana "paresthesia." Wanapoenda hospitali, madaktari huwauliza maswali mengi ili kujua chanzo cha hali hiyo na kupima nguvu za misuli (muscle strength), kupima hisia (sensation testing), au kufanya Nerve Conduction Study (NCS) kwa kutumia vifaa kama Electromyography (EMG), MRI (Magnetic Resonance Imaging), au CT Scan na Ultrasound (USG). Baada ya hapo, wagonjwa hufanyiwa fisiotherapi, au kupewa dawa za kupunguza mgandamizo wa mishipa, au wakati mwingine kufanyiwa upasuaji.

Namshukuru Mungu nimepona bure kwa Jina la Yesu, bila kuingia gharama ya kulipia vipimo hivyo na madawa!

Miujiza kama hii ni vigumu kuiona maishani mwako kama huamini kuwa Yesu ni Mungu, Mtenda miujiza.
Umekutana na Yesu wapi? Put aside faith, use reason.
 
Gunner11
Huu uzi nafikiri ulikupita. Mungu akusaidie uokoke uanze kuona miujiza ya Mungu maishani mwako
Tuna amini je kuwa Ulicho kisema kwenye maandishi yako ni kweli??

Ni sawa kuna vitu vinatokea maishani mwetu ila tunajuaje kuwa ni Mungu na sio imetokea tu kwa sababu kuna other causation?
 
Umekutana na Yesu wapi? Put aside faith, use reason.
My learned friend, “put aside faith and use reason” does not mean “believe only what you can physically see.” Reason itself allows us to infer the existence of realities we cannot see directly. So the real question is not merely, “Where did you physically meet Jesus?” but, “What does the evidence reasonably justify us to conclude about Him?” Reason should examine the evidence, not arbitrarily exclude the possibility of the unseen.
 
Back
Top Bottom