leo tarehe 5 March 2014 ni Jumatano ya majivu

leo tarehe 5 March 2014 ni Jumatano ya majivu

...! Hakika jambo usilolijua ni kama usiku wa giza!

"Misale ya Waumini (Kitabu cha kuwaongoza Waamini / Wakristu kushiriki kwa ushirikiano kuadhimisha Ibada Ya Misa Takatifu)" ni muhimu sana. Sababu kuu: ni kwamba ibada za Kiliturjia si ibada za mtu binafsi, bali ni maadhimisho ya Kanisa lote Ulimwenguni.

"Misale inamsaidia mwamini / mkristu kushirikiana kirahisi zaidi zote zinazoendeshwa chini ya Kanisa kwa kushirikiana na Waumini wenzako"

Vile vile yote yaliyo katika Misale ya Waamini msingi wake ni katika Biblia Takatifu na masomo yanayosomwa yamechaguliwa mahususi kulingana na mwaka wa kanisa na utaratibu pamoja na mfululizo wa vipindi na mutukio ya ya kiimani na haya hayapangwi na mtu mmoja.
 
...somo: Kumbukumbu 26:4-10; Warumi 10:8-13; Luka 4:1-13
tunaanza rasmi ni wakati wa Kwaresima ambapo tunapata nafasi kumtolea Mungu zile siku arobaini kama njia ya kumshukuru kwa ajili ya huruma na ukombozi wake katika Mwanae Yesu Kristo. Pia wakati huu Kanisa latupatia nafasi ya kufanya toba, na hivyo kabla ya Jumapili hii tunapakwa majivu usoni ili kuungama adharani udhaifu wetu, na kukubali mwaliko wa Kanisa kufanya kitubio, tukiwa tayari kwa neema ya Mungu kumshinda Shetani.
Basi wakati huu wa Kwaresima tunaitwa kumuiga Kristo aliyemshinda Shetani kwa kifo na ufufuko wake.
Kwenye Injili, tunasikiliza habari ya Yesu akiongozwa na Roho njangwani ambapo anajaribiwa mara tatu na Shetani.
Majaribio yenyewe na msimamo wa Yesu ni mfano mkubwa kwetu sisi. Lengo la majaribio hayo ni kutusaidia kuelewa jinsi Yesu anapinga kila jaribio.
Yesu anakataa kutawaliwa na njaa na hivyo anaepuka kishawishi cha kutumia uwezo wa Ki-Mungu ili ageuze jiwe liwe mkate.
Anakataa pia kutumia njia ya mkato ya kuwaakikisha watu kwamba yeye kweli ni Mwana wa Mungu.
Majaribio ya Yesu jangwani yatusaidia kuona kwamba Yesu aliyashinda kwa kukubali kuishi chini ya matakwa ya Baba, badala ya kukubali kushindwa na tamaa zake binafsi.
Yesu alishinda majaribio hayo kwa sababu aliishi kikamilifu maisha ya ki-roho, na hivyo akaweza kuzuia tamaa za ki-mwili kutomtawala. Ingekuwa rahisi sana kuruka kutoka kwa mnara wa Hekalu. Kitendo hicho kingewaakikisha watu kwamba yeye ni Mwana wa Mungu, lakini Yesu alishinda jaribio hilo.
Tunapoanza wakati huu wa Kwaresima, majaribio ya Yesu na jinsi aliyashinda yawe kwetu mfano tungefuata. Ikiwa tungetaka kumfuata Yesu kwa uaminifu na utiifu, lazima tuweke kando wakati ambao tungeweza kuwa peke jangwani ili tutafakari umaana wa wito wetu kama wafuasi wake; wakati tungeomba Mungu msaada wake na nguvu za neema yake.


Kwaresima ni wakati tunapogudua huruma na msamaha wa Mungu katika Mwanae Yesu;

Kama Yesu tuwe tayari kupambana na majaribio.

Tukimwamini Yesu na kuishi katika Roho wake, hata sisi pia tutashinda vishawishi hata ingawa ni vikali.


Kwaresima ni wakati tunapoitika wito wa Mungu kujuta dhambi zetu na kugeuka kabisa na kuwa wapya maishani mwetu.
umetoa maelezo lakini hujajibu swali hata moja.
 
[h=5]Jumatano ya Majivu[/h]Maadhimisho haya ya Jumatano ya Majivu yanayofanywa na makanisa kale makongwe, kunakuwa na majivu ambayo waumini wake wanapakwa kwenye vipaji vya nyuso zao na makasisi wao au wahudumu waliochaguliwa kufanya kazi hiyo. Wanavyos3ema wenyewe ni kwamba ibada na tendo hili vinalenga kuwawakumbusha waumini wao kuwa maisha yao hapa duniani ni mafupi na umuhimu wa wao kujindaa kwa kifo kinachokwenda kuwafuatia.

Lakini ibada hii haitokani na mapokeo wala imani ya Kanisa la kwanza bali chanzo chake kinatokana na imani za kipagani iliyochukuliwa na kuingizwa pamoja na maadhimisho ya Easter katika karne ya pili. Maadhimisho au ibada hii ya Jumatano ya Majivu haina uhusiano wowote na maagizo ya kwenye Biblia. Mwanzoni kabisa Jumatano hii ya Majivu ilikuwa ni siku ya kumuombolezea mungu aliyekufa na kifo cha kuteswa kipindi hiki cha pilikapilika za sikukuu. Ni wakati walipokuwa wanachoma matawi ya mitende ndipo hapo ndipo majivu haya yalipotokea.
 
Vile vile yote yaliyo katika Misale ya Waamini msingi wake ni katika Biblia Takatifu na masomo yanayosomwa yamechaguliwa mahususi kulingana na mwaka wa kanisa na utaratibu pamoja na mfululizo wa vipindi na mutukio ya ya kiimani na haya hayapangwi na mtu mmoja.
kunamengine yamebadilishwa kutoka katika bibilia ili kuendana na imani ya katoliki.
 
Yote mtasema ila imani ya mtu si ya kuchezea tukianza kutafuta vifungu vya kwaresma au majivu hakika tutaishia kukufuru tu cha muhimu kila mtu adumu katika imani yake......Hivyo Wakristu wenzangu tufunge kipindi hichi ili kujuta na kutubu dhambi zetu kama imani yetu inavyoelekeza,,,,,,bsi tukifunga
Mathayo 6:16-18 yasema, "Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamna; maana hujiimbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
 
Tutubu dhambi zetu,kwa kupigwa kwake msalabani sisi sote tumepona,mfungo mwema wapendwa.
 
Jamani wana jamvi;
Nisaidieni,
ktk biblia yetu takatifu,
Imeandikwa wapi habari ya kwaresma?
hasa hasa kuhusu kupakana majivu kwenye vipandauso?

unajua kwanini unaabudu jumapili sikuya jua wapi kwenye bibilia imeandikwa uabudu siku ya jumapili?
 
unajua kwanini unaabudu jumapili sikuya jua wapi kwenye bibilia imeandikwa uabudu siku ya jumapili?

Biblia inasema "Ingekuwa heri LEO msikie sauti yake, msiifanye migumu mioyo yenu."
Nifahamishe neno leo katika Biblia maana yake nini?
 
wana JF leo ni jumatano ya majivu ,ndiyo siku tunaanza mfungo wa kwaresma kwa wakritu wote hasa wakatoliki ni siku 40 za toba asanteni karibuni kwenye mfungo

.......kume na nyie mnafunga !?............saumu inaanza saa ngai na kuisha saa ngapi ?
 
wote wanaofunga ndo hawaelewi wanachofanya! Yesu hakwenda jangwani kufunga! sijuwi hawaelewi hata wanachoabudu! au ni kutojuwa kusoma! sijuwi wanaongozwa na pepo ktik kusoma maandiko! eti majivu! mnaakili kweli!!
ah acha magugu yakue pamoja na ngano mwisho wa siku itajulikana!!

kama unataka kujua habari za kufunga soma agano la kale kitabu cha nabii yoeli, pia zaburi ktk kisa cha nabii daudi alipoozaa na mke wa mtu. Na kisa cha nabii yona mjini ninawi. Kufunga ni kuomba msamaha kwa makosa tuliyotenda na pia kujiandaa kwa ajili ya pasaka. Kwa habari ya pasaka imekuwapo toka agano la kale. Tafadhali soma vizuri maandiko ili uelewe.
 
Huu uzi umevamiwa na majini ya Kisabato na ya Mwamedi......Ngoja niwahi chap kanisani nikayaombee yatoke.....
 
Hawajui kitu hao mkuu. Hawafati maandiko wanafata wanadamu

Mambo ya dini ni ya kuvumiliana tu. Utakuta dini nyingi zina kitu wanachokifuata. Nyingine zinafuata wanadamu, nyingine zinaabudu mawe, n.k.
 
.......kume na nyie mnafunga !?............saumu inaanza saa ngai na kuisha saa ngapi ?

saumu maana yake nini. Mi naamini tuna imani tofauti na wewe. Sisi tunafunga kuomba msamaha kwa makosa tuliyotenda na kujinyima kwa ajili ya kusaidia wahitaji na pia kujiandaa kumpokea kristu mfufuka. Sisi hatubadili masaa ya kula kutoka mchana kwenda usiku.
 
Mkifungua mnafungua kwa chakula gani?

Na mtu akiwa anaumwa inakuwaje?.

Na ukiwa umefunga ukatapika inakuaje?

Vp unaruhusiwa mumeza mate ufungapo?

hayo maswali uliyouliza majibu yake utayakuta islamic. Kwetu hayo hayapo.
 
Tubuni,na kuiamini injili!Unapofunga,husijionyeshe onyeshe barabarani kwamba umefunga!Paka mafuta yako vizuri usoni,na kile ambacho ungekula (lakini umeamua kufunga) kitoe kwa wahitaji naye baba aliye mbinguni aonaye sirini atakujaza baraka zake!

Asante Sungura
 
Mkifungua mnafungua kwa chakula gani?

Na mtu akiwa anaumwa inakuwaje?.

Na ukiwa umefunga ukatapika inakuaje?
Vp unaruhusiwa mumeza mate ufungapo?

“Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike, Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu lakini kwa upole na kwa hofu” (1Petro 3:14-15)
Ingawa kufunga katika maandiko karibu kila mara ni kufunga kutoka chakula, kunazo njia nyingine za kufunga. Kitu chochote kimeachwa kwa muda ili kuweka mawazo yetu kwa Mungu chaweza chukuliwa kufunga (1 Wakorintho 7:1-5). Kufunga lazima kuwe na mipaka muda uwekwe hasa wakati tunafunga kutoka kwa chakula. Muda ulioongezwa bila kukula unaweza kuwa wa madhara kwa mwili. Kufunga hakuko kwa madhumuni ya kuuteza mwili, bali kuyaelekeza mawazo yetu kwa Mungu. Kufunga kusichukuliwe kuwa “ratiba ya chakula.” Lengo la kibibilia la kufunga sio kupunguza uzito, bali kupata ushirika wa ndani na Mungu. Mtu yeyote anaweza kufunga, lakini wengine huenda hawataweza kufunga kutoka kwa chakula (Wenye ugonjwa wa sukari). Kila mtu anaweza anaweza kuacha kitu chochote kwa muda na kuleta mawazo yake karibu na Mungu.
 
Back
Top Bottom