leo tarehe 5 March 2014 ni Jumatano ya majivu

Tubuni,na kuiamini injili!Unapofunga,husijionyeshe onyeshe barabarani kwamba umefunga!Paka mafuta yako vizuri usoni,na kile ambacho ungekula (lakini umeamua kufunga) kitoe kwa wahitaji naye baba aliye mbinguni aonaye sirini atakujaza baraka zake!
 
Kwanini YESU alifunga? Kwa nini sisi tunafunga? Kuna uhusiano gani katika kufunga kwa YESU siku 40 na majilio ya pasaka? Je Pasaka ililetwa na YESU au ilikuwepo kabla?
 
Hawajui kitu hao mkuu. Hawafati maandiko wanafata wanadamu
 
Kina nani sasa wasiojua kitu? Angalia usije ukakurupuka kujidhania ndio una akili saaaaaana halafu baada ya muda ukathibitika pasipo shaka kuwa kichwani hamna kitu.

Hebu tuanzie na 'wasiojua kitu', nani hao?
 
wote wanaofunga ndo hawaelewi wanachofanya! Yesu hakwenda jangwani kufunga! sijuwi hawaelewi hata wanachoabudu! au ni kutojuwa kusoma! sijuwi wanaongozwa na pepo ktik kusoma maandiko! eti majivu! mnaakili kweli!!
ah acha magugu yakue pamoja na ngano mwisho wa siku itajulikana!!
 
Afadhali kusali kwa kufunga kuliko kusali dini ya mashetani na kufanya kuwa halali kabisa
wote wanaofunga ndo hawaelewi wanachofanya! Yesu hakwenda jangwani kufunga! sijuwi hawaelewi hata wanachoabudu! au ni kutojuwa kusoma! sijuwi wanaongozwa na pepo ktik kusoma maandiko! eti majivu! mnaakili kweli!!
ah acha magugu yakue pamoja na ngano mwisho wa siku itajulikana!!
 
Yoel 2:12,lakin hata sasa,asema Bwana Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote,na kufunga,na kulia,na kwa kuomboleza. Marko 1:15 Ufalme wa Mungu umekaribia tubuni na kuiamini Injili, Ufunuo 2:5 kumbuka ni wapi ulikoanguka ukatubu.
kila la kheri wote mnaofunga...
 
wana JF leo ni jumatano ya majivu ,ndiyo siku tunaanza mfungo wa kwaresma kwa wakritu wote hasa wakatoliki ni siku 40 za toba asanteni karibuni kwenye mfungo

Jamani wana jamvi;
Nisaidieni,
ktk biblia yetu takatifu,
Imeandikwa wapi habari ya kwaresma?
hasa hasa kuhusu kupakana majivu kwenye vipandauso?
 
Mambo ya wanadamu. Wakalia kusoma MITHALE ya WAUMINI badala ya kusoma Biblia. Wajinga sana hawa wajamaa
 
...“Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza. Rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana…”(Yoe 2:12)
Leo Kanisa limeanza kipindi cha Kwaresima. Hizi ni siku arobaini za sala, mafungo, kujinyima, kutubu na kuwasaidia wahitaji. Ni kipindi cha maandalizi ya sikukuu ya Ufufuko wa Yesu. Neno linalotuongoza niwongofu. Kwaresima ni safari inayomrudisha mkristo kwenye njia ya wongofu:nirudieni mimi!Hivyo ndivyo Bwana anavyotuhimiza. Anataka tumrudie, si kwa matendo ya nje, balikwa mioyo yetu yotekwakurarua mioyo na si mavazi.
Mafungo ya Kwaresima si ya kujikatalia kula tu, bali pia kuacha kabisa mawazo, maneno na matendo yanayopunguza mwendo wetu wa safari ya kiroho. Ni kipindi cha ibada ya moyo na cha kutenda matendo ya huruma yanayoonesha mshikamano wa kibinadamu na upendo wa kikristo unaookoa. Kama anavyosema Mt. Petro Krisologo; “Matendo ya huruma na ibada ndiyo mabawa ya mfungo… mfungo bila matendo ya huruma ni sanamu ya njaa, ni muonekano wa nje usio na thamani ya utakatifu. Bila ibada mfungo ni fursa ya ubinafsi… tunapofunga, ndugu zangu, tuweke chakula chetu mikononi mwa maskini” (Petro Krisologo,Omelia VIII, Sul digiuno della Quinquagesima)
Kipindi hiki kinapaswa kuwa kipindi kinachotusaidia kuanza tukio la kinabii, tukio linalosaidia kuyabadili maisha yetu na ya wenzetu. Katika Biblia Musa anafunga siku arobaini usiku na mchana kabla ya kupokea Amri Kumi za Mungu (Rej. Kut 34:28), anafanya hivyo pia Elia kabla hajakutana na Mungu juu yam lima Horebu (1Fal 19:8), hali kadhalika Yesu kabla hajaanza utume wake.
Majivu na maji
Kipindi cha Kwaresima kinaanza siku ya Jumatano ya Majivu. Don Tonino Bello, aliyekuwa Askofu wa Molfetta, Italia anaandika kuwa safari yote ya mkristo ni kuanzia kichwani hadi miguuni. Ni safari inayoelezwa vizuri kwa ishara ya majivu tunayopakwa kichwani na maji anayotumia Yesu kuwaosha mitume wake miguu. Ni safari inayoanzia kwenye toba na kuishia kwenye utumishi. “Toba na utumishi”, anasema Don Tonino Bello, “ni mahubiri makuu ambayo kanisa linayakabidhi kwa majivu na maji, kuliko kwa maneno”. Kwa maneno mengine ndiyo kusema kuwa mahubiri yetu hayawezi kuielezea vizuri zaidi safari ya uongofu kama jinsi ambavyo ishara ya majivu na maji inavyoweza kufanya. Tumrudie Mungu kwa moyo wa toba na katika utumishi tuzidi kuiona ile sura ya Mungu katika mahujaji wote walio katika safari ya maisha.
 
...! Hakika jambo usilolijua ni kama usiku wa giza!

"Misale ya Waumini (Kitabu cha kuwaongoza Waamini / Wakristu kushiriki kwa ushirikiano kuadhimisha Ibada Ya Misa Takatifu)" ni muhimu sana. Sababu kuu: ni kwamba ibada za Kiliturjia si ibada za mtu binafsi, bali ni maadhimisho ya Kanisa lote Ulimwenguni.

"Misale inamsaidia mwamini / mkristu kushirikiana kirahisi zaidi zote zinazoendeshwa chini ya Kanisa kwa kushirikiana na Waumini wenzako"
 
Kwanini YESU alifunga? Kwa nini sisi tunafunga? Kuna uhusiano gani katika kufunga kwa YESU siku 40 na majilio ya pasaka? Je Pasaka ililetwa na YESU au ilikuwepo kabla?

...somo: Kumbukumbu 26:4-10; Warumi 10:8-13; Luka 4:1-13
tunaanza rasmi ni wakati wa Kwaresima ambapo tunapata nafasi kumtolea Mungu zile siku arobaini kama njia ya kumshukuru kwa ajili ya huruma na ukombozi wake katika Mwanae Yesu Kristo. Pia wakati huu Kanisa latupatia nafasi ya kufanya toba, na hivyo kabla ya Jumapili hii tunapakwa majivu usoni ili kuungama adharani udhaifu wetu, na kukubali mwaliko wa Kanisa kufanya kitubio, tukiwa tayari kwa neema ya Mungu kumshinda Shetani.
Basi wakati huu wa Kwaresima tunaitwa kumuiga Kristo aliyemshinda Shetani kwa kifo na ufufuko wake.
Kwenye Injili, tunasikiliza habari ya Yesu akiongozwa na Roho njangwani ambapo anajaribiwa mara tatu na Shetani.
Majaribio yenyewe na msimamo wa Yesu ni mfano mkubwa kwetu sisi. Lengo la majaribio hayo ni kutusaidia kuelewa jinsi Yesu anapinga kila jaribio.
Yesu anakataa kutawaliwa na njaa na hivyo anaepuka kishawishi cha kutumia uwezo wa Ki-Mungu ili ageuze jiwe liwe mkate.
Anakataa pia kutumia njia ya mkato ya kuwaakikisha watu kwamba yeye kweli ni Mwana wa Mungu.
Majaribio ya Yesu jangwani yatusaidia kuona kwamba Yesu aliyashinda kwa kukubali kuishi chini ya matakwa ya Baba, badala ya kukubali kushindwa na tamaa zake binafsi.
Yesu alishinda majaribio hayo kwa sababu aliishi kikamilifu maisha ya ki-roho, na hivyo akaweza kuzuia tamaa za ki-mwili kutomtawala. Ingekuwa rahisi sana kuruka kutoka kwa mnara wa Hekalu. Kitendo hicho kingewaakikisha watu kwamba yeye ni Mwana wa Mungu, lakini Yesu alishinda jaribio hilo.
Tunapoanza wakati huu wa Kwaresima, majaribio ya Yesu na jinsi aliyashinda yawe kwetu mfano tungefuata. Ikiwa tungetaka kumfuata Yesu kwa uaminifu na utiifu, lazima tuweke kando wakati ambao tungeweza kuwa peke jangwani ili tutafakari umaana wa wito wetu kama wafuasi wake; wakati tungeomba Mungu msaada wake na nguvu za neema yake.

Kwaresima ni wakati tunapogudua huruma na msamaha wa Mungu katika Mwanae Yesu;

Kama Yesu tuwe tayari kupambana na majaribio.

Tukimwamini Yesu na kuishi katika Roho wake, hata sisi pia tutashinda vishawishi hata ingawa ni vikali.

Kwaresima ni wakati tunapoitika wito wa Mungu kujuta dhambi zetu na kugeuka kabisa na kuwa wapya maishani mwetu.
 
...“Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza. Rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana…”(Yoe 2:12)
Leo Kanisa limeanza kipindi cha Kwaresima. Hizi ni siku arobaini za sala, mafungo, kujinyima, kutubu na kuwasaidia wahitaji. Ni kipindi cha maandalizi ya sikukuu ya Ufufuko wa Yesu. Neno linalotuongoza niwongofu. Kwaresima ni safari inayomrudisha mkristo kwenye njia ya wongofu:nirudieni mimi!Hivyo ndivyo Bwana anavyotuhimiza. Anataka tumrudie, si kwa matendo ya nje, balikwa mioyo yetu yotekwakurarua mioyo na si mavazi.
Mafungo ya Kwaresima si ya kujikatalia kula tu, bali pia kuacha kabisa mawazo, maneno na matendo yanayopunguza mwendo wetu wa safari ya kiroho. Ni kipindi cha ibada ya moyo na cha kutenda matendo ya huruma yanayoonesha mshikamano wa kibinadamu na upendo wa kikristo unaookoa. Kama anavyosema Mt. Petro Krisologo; “Matendo ya huruma na ibada ndiyo mabawa ya mfungo… mfungo bila matendo ya huruma ni sanamu ya njaa, ni muonekano wa nje usio na thamani ya utakatifu. Bila ibada mfungo ni fursa ya ubinafsi… tunapofunga, ndugu zangu, tuweke chakula chetu mikononi mwa maskini” (Petro Krisologo,Omelia VIII, Sul digiuno della Quinquagesima)
Kipindi hiki kinapaswa kuwa kipindi kinachotusaidia kuanza tukio la kinabii, tukio linalosaidia kuyabadili maisha yetu na ya wenzetu. Katika Biblia Musa anafunga siku arobaini usiku na mchana kabla ya kupokea Amri Kumi za Mungu (Rej. Kut 34:28), anafanya hivyo pia Elia kabla hajakutana na Mungu juu yam lima Horebu (1Fal 19:8), hali kadhalika Yesu kabla hajaanza utume wake.
Majivu na maji
Kipindi cha Kwaresima kinaanza siku ya Jumatano ya Majivu. Don Tonino Bello, aliyekuwa Askofu wa Molfetta, Italia anaandika kuwa safari yote ya mkristo ni kuanzia kichwani hadi miguuni. Ni safari inayoelezwa vizuri kwa ishara ya majivu tunayopakwa kichwani na maji anayotumia Yesu kuwaosha mitume wake miguu. Ni safari inayoanzia kwenye toba na kuishia kwenye utumishi. “Toba na utumishi”, anasema Don Tonino Bello, “ni mahubiri makuu ambayo kanisa linayakabidhi kwa majivu na maji, kuliko kwa maneno”. Kwa maneno mengine ndiyo kusema kuwa mahubiri yetu hayawezi kuielezea vizuri zaidi safari ya uongofu kama jinsi ambavyo ishara ya majivu na maji inavyoweza kufanya. Tumrudie Mungu kwa moyo wa toba na katika utumishi tuzidi kuiona ile sura ya Mungu katika mahujaji wote walio katika safari ya maisha.

mkuu kbm;
ninukulie andiko lililoongelea KWARESMA.
Na agizo linalotuagiza kupaka majivu.
Na ndo swali langu wakuu.
 
Back
Top Bottom