Ndani ya muda huu rafiki yangu ameniletea taarifa kwamba mke wangu mama Neema ananisaliti ndani ya gesti moja mjini Mwanza.Rafiki yangu ameniambia kamuana akiingia gesti na jamaa mmoja ambaye ni jirani yetu anayefanya kazi TANESCO.
Nimejalibu kumpigia simu mke wangu mama Neema anasema yupo Mabatini kwa dada yake anaumwa.Rafiki yangu ananilazimisha twende kwenye hiyo gesti tukafumanie.Kwakweli nimechanganyikiwa sana mapigo ya moyo yamebadilika.
Wadau busara ni nini hapa niende gesti au nisiende? Maana hata sielewi kabisa.
Bora ununue bia baridi......kaa kwenye TV......mtizame Magufuli na Majaliwa wakishiriki usafi.......msubiri mama Neema arudi nyumbani mlale.......kwanza kushakua usiku saa hizi..........
Dah pole sana mkuu, ila cha zaidi action ya kufanya lolote iko mikononi mwako ,but ukikuta kwel Ana chepuka wee usiongee chochote rudi hom , tafuta bongo movie "Oprah my wife "
Kamanda kauka, uende guest kufanya nini? Jamaa anaweza akakuzulu bure katika kujihami. Wewe kesho asbhi sana anzia kwa huyo ndugu yake. halafu mmsubiri anapokuja. Akifika tu unamsalimia na kuondoka zako kurudi kwako. Yeye ndoo atachagua kuja kwako au kuhamia kwa TAnesco