Leo nimekutana na Sikujua akilia kwenye busi kisa mapenzi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Sikujua ni wale golden girls katika familia, amesoma elimu yake yote kwa msaada kidogo wa wazazi na msaada mkubwa shukran kwa serikali. Alipomaliza shule alibahatika kupata kazi katika taasisi ya umma. Ana kazi yenye heshima na kipato kizuri tu.

Miaka 13 iliyopita alikutana na Raymond, kijana nadhifu na walianza mapenzi, miezi sita baada ya kujuana walifanya babe come and we stay. Hii ilikua ni nyumba aliyopangisha Sikujua yenye chumba kimoja cha kulala.

Sikujua anasafiri sana kikazi, kuna wakati hela za posho na per diem zilikubali alipata pesa ya kutosha na kuamua kumshirikisha Raymond na walinunua kiwanja sehemu ambayo ni Prime. Kiwanja cha nusu eka walijenga nyumba ndogo kwa kuanzia, a Shima ni kuwa oké iwe guest wing siku za usoni, ilikua na vyumba viwili na cha kwao ni self contained.

Raymond ni mfanya bishara, na mara nyingi Sikujua ana mboost, sasa hivi ameamua kuweka nguvu kwenye stationery na kuwa na Wholesale ya kalamu, madaftar, printing paper nk. Bidhaa zake anazitoa China. Anahakikisha mzigo wake ni quality hivyo si rahisi kupata mshindani.

Sikuju anasema matatizo alianza kuyaona ndani ya miaka mitano ya kwanza, Raymond anaweza kumtumia text akimkumbusha asisahau kurudi na mkate na maziwa ya NIDO kwani yamekwisha. Sikujua alianza kujiuliza, nyumba kwa 80% amejenga yeye, sasa huyu mwanaume anaekumbusha nisisahau mkate yeye anachangia nini?

Ukiona matatizo kwenye mapenzi ni mwanzo wa ufa, msipoyajadili na kuyamaliza mtakuja kujenga ukuta. Mwaka jana mfanyakazi mwenzao wakina Sikujua alifariki na madaktari walithibitisha ni Covid 19 ndiyo sababu cha kifo. Wafanyakazi wote walipimwa na Sikujua alikutwa na Covid. Alipewa wiki tatu za kujiuguza na asichanganyike na watu mbali na wale anaoishi nao. Raymond kusikia hii habari na yeye aliji isolate hotelini. Alimuacha Sikujua na dada wa kazi. Homa aliyokuwa nayo Sijukua ilikua kali, dada yake aliamua kuwapeleka watoto wake kijijini kwa mama yao ili amuuguze Sikujua.

Baada ya kupona sikujua anafundishwa kuwa Raymond aliji isolate na mrembo mmoja ndani ya hoteli na hii ilikua ni kumhudumia binti ambae walitarajia mtoto pamoja na mimba ya miezi mitatu iliharibika. Raymond alimpeleka hospitali na kulipa gharama zote na baada ya kuruhusiwa kutoka amemuweka hotelini ili apate full bed rest, hakuna kutandika kitanda wala kupika chai.

Mwaka huu uvumilivu umemshinda, Raymond amemwambia Sikujua wapeane nafasi na kufikiria kama kuna mwanga huko mbele ya safari yao ya mapenzi. Raymond amehama nyumbani na anadai nyumba iuzwe wagawane nusu kwa nusu kwani katika miaka 13 aliyoishi na Sikujua na yeye kuna mchango wake.

Sikujua haamini, kiwanja alichonunua kwa pesa yake na nyumba aliyoijenga single handed kwa kujibana, leo kuna anaetaka iuzwe wagawane pesa. Sikujua mwenyewe aliniambia, kiwanja kilipo kwa sasa hatamudu kukinunua.

Hawakufanikiwa kupata mtoto katika mahusiano yao na Sikujua anasema alitumia pesa, nguvu na akili yake kumlea Raymond na leo analipwa haya. Anatumia anti depressants kwa sasa ambazo zinamfanya anenepe. Nilikutana na Sikujua kwenye basi akielekea kwetu Kwamtogole. Alinionyesha picha ya Raymond kwakweli ni handsome.
 
Sikujua ni wale golden girls katika familia, amesoma elimu yake yote kwa msaada kidogo wa wazazi na msaada mkubwa shukran kwa serikali. Alipomaliza shule alibahatika kupata kazi katika taasisi ya umma. Ana kazi yenye heshima na kipato kizuri tu.

Miaka 13 iliyopita alikutana na Raymond, kijana nadhifu na walianza mapenzi, miezi sita baada ya kujuana walifanya babe come and we stay. Hii ilikua
Picha iko wapi
 
Simple and clear, kama Raymond anataka kuondoka basi aondoke kimya kimya! Mambo ya tugawane asikubali maana kanunua yeye na kajenga yeye! Huo ndo uwe msimamo wake period! Au hicho kiwanja kina majina ya Raymond?
 
Simple and clear, kama Raymond anataka kuondoka basi aondoke kimya kimya! Mambo ya tugawane asikubali maana kanunua yeye na kajenga yeye! Huo ndo uwe msimamo wake period! Au hicho kiwanja kina majina ya Raymond?
Aliweka majina yao wote kumshawishi Raymond kuwa wako safari moja. Pia sisi wanawake kuna wengine wanapenda kuonekans ni wapenda maendeleo mwanaume ashawishike.
 
Aliweka majina yao wote kumshawishi Raymond kuwa wako safari moja. Pia sisi wanawake kuna wengine wanapenda kuonekans ni wapenda maendeleo mwanaume ashawishike.
Huyo Raymond anahitaj kufunzwa akili. Swali moja zaid mkuu, biashara za Raymond zina thaman ya kutosha? Pia afanye uchunguzi zaid kwenye mali za Raymond alizozificha au za hadharani ili kama ilibidi yeye ndo afungue kesi ya kudai mgao
 
Hiki ulichokiandika ni minority case kwa wanawake ila ni majority kwa wanaume. Mfano raymond angekua mwanamke na huyo sikujua awe mwanaume ktk same situation raymond angepata watetezi wa kumsemea lkn kinyume chake basi tutamshangaa na kumlaumu raymond.
 
Back
Top Bottom