Leo nimekuja kivingine..................... ........! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leo nimekuja kivingine..................... ........!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mtambuzi, Apr 28, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya dini zinasema, jisaidie na ndipo Mungu atakusaidia. Nyingine zinasema, bisha hodi utafunguliwa. Kubisha hodi ni hadi utembee na kufika mlangoni, bila kufika mlangoni hutafunguliwa. Hii inaonesha kwamba ni sisi tunaoanza kufanya ili jambo liwe.Kama tunataka kupata tunacholenga kwenye maisha yetu, hatuna budi kujua pia tunachopanda kila siku kupitia mawazo, vitendo na kauli zetu.

  Kama unawapenda baadhi ya watu na kuwachukia wengine, utavuna kutoka pande zote, chuki na upendo.
  Kufikiri, mitazamo, imani, hisia,vitendo na kauli, ni mbegu ambazo zinapokuja kuzaa baada ya kupandwa hutuletea mazao tuliyoyapanda. Inawezekana tulisahau au kutojua kwamba, tunapanda mbegu fulani. Hili la kutojua halizuii mbegu hiyo kuzaliwa na kukua, hadi kuvunwa, ikiwa ni ya mmea huo huo.Kwa kadiri tunavyotilia nguvu mawazo, hisia, vitendo, kauli, mitazamo na imani fulani tulizonazo, ndivyo ambavyo tunanyweshea na kutilia mbolea mbegu hizo na matokeo yake yatakuwa mazuri sana kwa ubaya au uzuri, kutegemea tulipanda nini.

  Jambo la msingi hapa ni kuchagua kupanda kile ambacho mtu anakipenda. Ruhusu kwenye mawazo yako, imani zako, hisia zako, mitazamo yako, vitendo na kauli zako, yale tu ambayo yatakupa furaha, amani na utulivu. Pia ambavyo vitakupa ridhiko, upendo na uelewa. Usiruhusu hofu, ukosefu, chuki, kijicho,na chochote chenye kuumiza au kumuumiza mwingine, maana hicho ndicho kitakachokujia hata kama hukitaki.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Well said Mtambuzi, ukinuia wengine mabaya utavuna mabaya, ukinuia wengine mema utavuna mema.

  Mie huamini hata ukimtendea mtoto wa mtu mwingine mazuri, mazuri hayo yatalipwa kwa watoto wako.

  Na ni mwiko kula kilicho cha yatima.
   
 3. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Bonge la comment yaaani la ukweli hili Konnie.. I think it is the Best JF Comment/Post of April!

  Niruhusu nikufagilie..
   
Loading...