Leo nikijibiwa haya maswali yangu muhimu mawili tu nitakuwa ni mwenye furaha na nitazidi kuipenda JF

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,926
Swali # 1.

Je, ni kweli kwamba wale Watu ambao huwa wanakuwa ni Waajiriwa wa Idara Nyeti hasa za CIA au KGB au MOSSAD ( sijajua wa Tanzania ) huwa wakipewa Jukumu la ama Kumuua au Kumjeruhi Mtu iwe ama kwa Chuki zao tu Kwake au kwa Maslahi mapana ya Marekani, Urusi na Israel baadae na Wao huuliwa ili Kupoteza Ushahidi?

Swali # 2.

Je, ni kweli kwamba Makomandoo hasa wa Marekani au Urusi au Israel ( sijajua wa Tanzania ) huwa wakifikisha Umri wa Miaka 50 huwa Wanauliwa ili baadae wasije wakawa wanatumika na ama Maadui wa ndani au wa nje wa nchi?

Kwa mfano kuna Mtu yupo Urusi ameniambia ( japo najilazimisha Kumuamini ) kwamba ana Rafiki yake Mmoja hivi wa Kirusi ila ni Mwanasiasa huko na ni Mpinzani mkubwa tu wa Rais Putin kuna Watu wa Idara Nyeti ya Urusi walitumwa kwenda Kumuua lakini labda kwa Mapenzi yake Mwenyezi Mungu pamoja na kwamba walimjeruhi vibaya kiasi cha Kumsikitisha kila Mrusi ila hakufa na hadi hivi leo yupo Hai japo anaeendelea kupatiwa Matibabu.

Ameniambia kuwa wale Watu wote wa Idara Nyeti ya nchini Urusi waliopewa hilo Jukumu la Kumuua baada ya Kushindwa Kulitekeleza hivi sasa wote wameuliwa kiasi kwamba hata Maiti zao hazijulikani zimezikwa wapi huko nchini Urusi.

Najua JF kuna Wataalam zaidi hivyo hapa mtanisaidia nami pia kuweza kupata Maarifa zaidi japo nashukuru mno Mungu kuwa haya Matukio sijawahi kabisa kuyasikia hapa Tanzania au Uganda au Rwanda achilia mbali Kenya na Burundi na siombei pia haya ya huko Marekani, Urusi na Israel yafanyike au yatokee huku Kwetu.

Karibuni.
 
Swali # 1.

Je ni kweli kwamba wale Watu ambao huwa wanakuwa ni Waajiriwa wa Idara Nyeti hasa za CIA au KGB au MOSSAD huwa wakipewa Jukumu la ama Kumuua au Kumjeruhi Mtu iwe ama kwa Chuki zao tu Kwake au kwa Maslahi mapana ya USA, RUSSIA na Israel baadae na Wao huuliwa ili Kupoteza Ushahidi?

Nasubiri swali la pili kwanza ili nijibu yote kwa pamoja
 
Kadri unavyojua na kufaham mambo mengi kuhusu jambo flani, ndivyo unavyozidi kuwa tishio kwa wahusika.

Leo hii nikikwambia jambo ambalo nisingependa lijulikane, kesho ikitokea hali inayonihatarishia usalama au maslahi yangu huku nikiamini wewe unafahamu hilo jambo, suluhu ya kwanza ni kukuua tu.

Ndio maana wengi wanatumia makundi au watu binafsi kutekeleza mauaji.
 
Rafiki aya yako ya mwisho imenifikirisha mno tu. Kwahiyo kumbe wale Watu ambao watakuja Kukuua baadae huwa hawatokei katika hizo Idara Nyeti za Marekani, Urusi na Israel? Na ni kwanini sasa huwa hawatekelezi hayo Mauwaji wao kama wao ( Watu wa Idara hizo tajwa hapa ) na badala yake wanawatumia Watu binafsi au Makundi?

Kwahiyo Rafiki kumbe na Mimi kama Mtanzania nikiwa na Adui yangu hapa hapa Tanzania naweza Kukodi Makundi ya Wauwaji ili Wamuue nikiwatoa labda katika nchi za Rwanda au Uganda kama siyo Afrika Kusini au Burundi na ikiwezekana hata naweza kuwatoa nchini Somalia?
 
Sio kweli labda kutokee ugomvi, hilo jibu linajitosheleza kwa maswali yote mawili

Kwahiyo kumbe wale wote wanaouwawa na Mashirika ya Kijajusi ya Marekani, Urusi na Israel huwa wanakuwa na Ugomvi binafsi nao? Ndiyo maana naipenda nchi yangu ya Tanzania kwani yenyewe haina huu Ukatili kwani Watanzania Siku zote tunapendana, hatugombani na ni Watu wa Amani daima.
 
maswali yako yote mawili ni NO mkuu hakuna anayeuliwa kutokana na hayo uliyoyaongea,kuuliwa kutatokea kama kuna sababu nyingine .elewa PM wa sasa wa ISRAEL alikuwa commando mzuri sana na ameshiriki kwenye deadly operations nyingi tu zinazoihusu nchi yake,President Putin ametokea KGB ,na hata hapa tuna wengi ambao wangali hai na wengine wamejiingiza kwenye politics za nchi.elewa TISS muundo wake na watumishi wake wengi ni wanajeshi,na baada ya utumishi wao wengi wanaishi maisha ya kawaida kama sisi na hakuna kuuliwa,elewa Mr.Kitine alikuwa mkuu wa usalama wa Taifa na sasa tunapishana naye mitaani!na anatoa comments zake kama mimi na wewe!
 
Ngoja nione michango, japo kila yule atasema kwa mtazamo, sidhan km kuna atakayekuja na fact, maana ni siri
 
Kwanini unataka kujua hayo mkuu ?
Umeshindwa kumuamini huyo rafiki yako anayeishi urusi utatuamini sisi wa tandahimba tukujibu majibu ya urusi !!!

Umesema utafurahi ukijibiwa maswali yako
Utafurahi kwa lipi kusikia kwamba wanauliwa baada ya kazi maalumu au umri maalumu?.
Kwa akili ya kawaida unazani kama wangekua wanauliwa pangekalika hapa duniani ?
Ukifuga mbwa akibadilika na kuwa tishio kwa watu huwa anapewa sumu au kupigwa nondo/risas lakini kama hana tatizo na watu huwa anafugwa mpaka kuzeeka.
 
Kwahiyo kumbe wale wote wanaouwawa na Mashirika ya Kijajusi ya Marekani, Urusi na Israel huwa wanakuwa na Ugomvi binafsi nao? Ndiyo maana naipenda nchi yangu ya Tanzania kwani yenyewe haina huu Ukatili kwani Watanzania Siku zote tunapendana, hatugombani na ni Watu wa Amani daima.
Nani atakubali kufanya kazi ambayo ukiikamilisha na wewe unauawa?
 
maswali yako yote mawili ni NO mkuu hakuna anayeuliwa kutokana na hayo uliyoyaongea,kuuliwa kutatokea kama kuna sababu nyingine .elewa PM wa sasa wa ISRAEL alikuwa commando mzuri sana na ameshiriki kwenye deadly operations nyingi tu zinazoihusu nchi yake,President Putin ametokea KGB ,na hata hapa tuna wengi ambao wangali hai na wengine wamejiingiza kwenye politics za nchi.elewa TISS muundo wake na watumishi wake wengi ni wanajeshi,na baada ya utumishi wao wengi wanaishi maisha ya kawaida kama sisi na hakuna kuuliwa,elewa Mr.Kitine alikuwa mkuu wa usalama wa Taifa na sasa tunapishana naye mitaani!na anatoa comments zake kama mimi na wewe!

TISS ndiyo nini Mkuu?
 
Rafiki aya yako ya mwisho imenifikirisha mno tu. Kwahiyo kumbe wale Watu ambao watakuja Kukuua baadae huwa hawatokei katika hizo Idara Nyeti za Marekani, Urusi na Israel? Na ni kwanini sasa huwa hawatekelezi hayo Mauwaji wao kama wao ( Watu wa Idara hizo tajwa hapa ) na badala yake wanawatumia Watu binafsi au Makundi?

Kwahiyo Rafiki kumbe na Mimi kama Mtanzania nikiwa na Adui yangu hapa hapa Tanzania naweza Kukodi Makundi ya Wauwaji ili Wamuue nikiwatoa labda katika nchi za Rwanda au Uganda kama siyo Afrika Kusini au Burundi na ikiwezekana hata naweza kuwatoa nchini Somalia?

Naomba nisiandike mambo mengi sana ila itoshe tu kusema, jitahidi kujikita kwenye mambo machache ya msingi yatakayokuletea manufaa.

Kwa ufupi hivyo vyombo na mashirika uliyoyataja, hataki kuhusishwa moja kwa moja na matukio hasa pale mambo yanapoenda tofauti na mipango. Hawataki kuacha ushahidi.
 
Back
Top Bottom