EJM_
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 3,836
- 2,119
Niliambiwa, ulikuwa ni usiku kama huu wa leo wakati watu wakiwa wameenda kwenye misa ya mkesha wa kuamkia sikukuu ya x-mas marehemu mama yangu ndio alikuwa anahangaika kunileta mimi duniani. Naam usiku kama huu ndipo nilipozaliwa miaka kadhaa iliyopita na hivyo kufanya leo tarehe 25 kuwa sio tu siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Masiha, bali pia kuzaliwa kwangu na mwaka mwingine mpya kwangu.
Nawashukuru sana wana JF, hasa wa chumba hiki cha MMU, Siasa, Great Thinkers, Chit Chat, kule kwenye teknolojia nk. Kwani mmekuwa na mimi mpaka ninapoingia mwaka wangu mpya leo.
Nawatakia sherehe za kufana kwenye sikukuu hizi za mwisho wa mwaka lakini kikubwa zaidi, nawaombea sana Mwenyezi Mungu awape baraka na kuwazidishia kwa kila mtakalolifanya.

"HAPPY X-MAS & MERRY NEW YEAR TO YOU ALL"