ng'ombo
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 418
- 619
Leo ni Kumbukumbu ya kifo cha Tx Moshi William wa msondo ngoma Machi 29, 2017.
Marehamu Moshi William alifariki tarehe 29 Machi mwaka 2006 siku ya jumatano majira ya saa 3 asubuhi na kuzikwa siku hiyo hiyo katika makaburi ya Keko Machungwa.
Tarehe na siku ya kifo chake vimejirudia mwaka huu. Alitunga nyimbo nyingi lakini baadhi ya nyimbo zilizotia fora sana ni kilio cha mtu mzima, ndoa ndoana, kaza moyo na ajali.
Tx Moshi William ameacha pengo na kumbukumbu isiyosahaulika kwa wapenzi wa msondo na muziki wa dansi kwa ujumla hapa Tanzania na Duniani kwa ujumla.