Leo ni kumbukumbu ya Entebe raid 4-7-2011!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leo ni kumbukumbu ya Entebe raid 4-7-2011!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tango73, Jul 4, 2011.

 1. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  NI vizuri leo kuwakumbuka mashujaa wa ki israel walikwenda kuwakomboa ndugu zao pale entebe nchini Uganda, mwaka 1976 usiku wa saa 12.32. Ni miaka thereathini na tano imepita lakini lile tendo la kishujaa ni kama vile limetokea jana asubuhi. Magaidi ya kipalestina yasiojua haki za binadamu yalitaka kuwachinja waisraeli 126 wakiwemo wazee, watoto na vijana kadhaa. Waliiteka nyara ndege ya kifaransa na kutua Uganda huku wakipata msaada mkubwa kutoka kwa Raisi wa uganda muda huyo hayati Nduli Idd amin dadaa. Israeli ili kuhakikisha inawakomboa raia zake wasiyo na hatia ilichagua makomandoo ambao kila mmoja wa makomandoo hayo alikuwa na ujuzi wa kuponea kifo chupuchupu vitani. Kijana Jonathan Netanyahu akiwa na miaka 28 aliongoza kikosi kilichowachinja magaidi wote wa kipalestina kwa muda wa dakika 45 tuu. Kwa kitendo hicho Israel ilikomesha magaidi wote duniani kutowanyanyasa raia wake wasio na hatia wakiwa safarini na kutoa onyo kwa nchi za kiafrica ambazo zilikuwa zinanunuliwa kusaidia kuwatesa wa Israeli kama vile Uganda.Tanzania tunajifunza nini na mafanikio haya ya israeli? Tujifunze kuwa ili kufanikiwa katika mazingira magumu ni jambo la maana sana kuchagua watu wenye sifa katika vitendo na elimu. Kuwa na elimu hakutoshi bali pia hiyo elimu lazima uifanyie matendo yanayoonekana kwa umma. Tusingekuwa na mgao wa umeme kama serikali ingefanya mateuzi kama yale ya liyofanywa na Israel kuwaokoa ndugu zao. Mungu libaliki taifa la Israel na sharon Ariel augue vema. amen!
   
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu asante kwa kutukumbusha tarehe hii muhimu ingawaje mimi binafsi haikuwa kwenye kumbukumbu zangu. Nina imani wengi wa members hapa hii itakuwa ni story mpya kbisa kuisikia lakini ukweli unabaki pale pale kwamba kitendo kile kilikuwa cha kishujaa mno. Labda kwa kuongezea ni kwamba Israel walimpoteza askari mmoja kwenye hiyo raid na huyo si mwingine bali ni Jonathan Netanyau aliyekuwa akikiongoza hicho kikosi cha makomandoo. Walitengeneza filamu ya hii kitu na nayejua jina la hiyo film atwambie kwa faida ya wale ambao hawaijui hii habari wanaweza kuangalia hiyo film. Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi hiyo filamu inaitwa 90 minutes at Entebbe!!!

  Tiba
   
 3. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Swadakta,
  Ngojea aamke Malaria Sugu na mausingizi yake, na hasira za kunyimwa unyumba na mumewe, atamwaga upupu wa al madrasat, ndo uone akili za makalion. Pia jana Malaria Sugu alikalisha ****** kutwa nzima hata hakuhudhuria hitma kupiga pilau.
  !
   
 4. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kweli Israel ilitoa fundisho kubwa kwa magaidi wote duniani! Mungu Ibariki Israel, atakaekubariki abarikiwe na atakayekulaani alaaniwe!
   
 5. Elizaa

  Elizaa Senior Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 160
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Umenikumbusha ushujaa wa hawa jamaa, kuwalinda raia wao kwa gharama yoyote. Viongozi wetu wana la kujifunza kutoka kwa Waisrael
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  safi sana then ni siku ya uhuru wa marekani USA. 04/July!
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Jul 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa siijui tarehe hii...
   
 8. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Viongozi wetu ni kuua raia zake kwa gharama yoyote!
   
 9. E=mcsquared

  E=mcsquared JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  RIP Yoni Netanyahu (was shot dead) and Dora Bloch (killed in Hispotal by "Joka Kuu, Fashist Nduli Idd Amin Dadaa").
   
 10. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Filamu hii ni nzuri sana, kwa wanaoweza kuitafuta you tube inapatikana, search kwa kuandika "Entebbe raid" itakuletea. Ni filamu ya kishujaa kweli kweli.
   
 11. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #11
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  asante kwa kutukumbusha mkuu.
   
 12. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Vilevile kuna novel kwa jina hilo hilo la "90 minutes at Entebbe" na kingine " the Entebbe Raid". Tukio zima limetawaliwa na episodes kama za sinema za James Bond lakini kwa wale waliokuwa hai na utambuzi ile ndiyo hali halisi wakati Iddi Amin Dada akiwa amewekwa kwenye mazungumzo na wakali wa MOSSAD huku kwenye kiwanja cha Entebbe mapambano yakiendelea bila yeye kujua.

  Jonathan Netanyahu ni kaka damu wa Waziri Mkuu sasa wa nchi ya Israel ambao wote kwa pamoja ni wana wa Israel waliozaliwa baada ya kuanzishwa kwa Taifa la Israel mwaka 1947 na Umoja Wa Mataifa
   
 13. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kinda Idd Amini hakuwa mtu makini sana..alikuwa mtu wa kuwezwa kupotezwa kirahisi rahisi....
   
 14. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 80
  Na kwa walle wanaofuatilia sana habari za kisiasa na kijeshi za huko mashariki ya kati watakuwa wanafahamu kwamba israeli ni miongoni au niseme ni nchi bora kabisa katika ulimwengu katika kulinda raia wake. Ni nchi yenye raia kama milioni sita hivi (na wayahudi ulimewenguni kote hawazidi milion 15) huku wakiwa wamezungukwa na mabilioni ya magaidi wa kiarabu na kipersia wanaotamani kila sekunde kuona lile taifa linapotea kwenye ramani ya dunia. Pamoja na Opersheni entebbe, hizi operesheni za kishujaa za kuokoa raia wake "behind enemy lines" israeli inazifanya almost on daily basis.

  Mfano, kamanda Ehud Barak (waziri wa sasa wa ulinzi) mwaka 1972 wakati ule akiwa kijana wa miaka 30 mwaka aliweza kuongoza kikosi cha makomandoo kuokoa mateka wa ndege ya israeli iliyokuwa imetekwa na magaidi wa kiarabu na kuwaokoa wote "operesheni isotope". Mwaka 1986, makomandoo wa israeli walifanikiwa kuruka kwa ndege za kivita 15 kutoka israel kwenda iraki (umbali mrefu sana) enzi za dikteta saddamu hussein, huku wakivuka vikwazo vya rada za saudi arabia na jordan na kulipua kinu cha nuclear cha sadamu na kukipotezea kabisa. Hakuna ndege yeyote ya israel iliyolipuliwa.

  Hata kama wewe ni mpenzi wa israel au adui yake, hata kama wewe unakubaliana au hukubaliani na siasa zake kwa majirani zake, matukio haya ya ujasiri, ushujaa, ufundi pamoja na umakini wa israel katika kulinda raia wake preemptively, defensively na offensively unaodhihirisha uwajibikaji usio na mfano wa israeli kwa wanachi wake. Ni kweli vyombo vya usalama vya Tanzania vinapaswa kujifunza jambo moja au viwili kutoka kwa hawa wezetu.
   
 15. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Please join CUFI (american for the moment but soon I will start one here for Tanzania -cursed enough!), For those who does not belive in replacement. Christians United for Israel: Welcome
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  crap from crapist!
   
 17. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  RIP hero Jonathan Netanyau brother of the current Israel PM Benjamin Netanyau and a former close friend to Ehud barak serving defence minister of Israel.
   
 18. k

  kiloni JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu
  Mwema asome hii kabla ya kutuma askari kuua ndugu zake shameeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,988
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kutujuza,waisrael huwa wanamaanisha kwa kila jambo.
   
 20. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu kuna matukio mengi yanayoonyesha ni jinsi gani waisrael walivyo makini when it comes kwenye masuala ya kulinda usalama wao. Usisahau ndege 100 za kivita walizozilipua pale Cairo ambazo zilikuwa zinasubiri amri kuruka na kwenda kufuta kabisa taifa linaloitwa Israel lakini kwa mshangao ndege zote 100 zililipuliwa hapo hapo uwanjani hata kabla hazijaruka na Rais Nasser alipata ugonjwa wa moyo aliposikia hii habari, ugonjwa ambao haukumuacha mpaka ALIPOFARIKI. Usisahau pia ile Radar iliyokuwa imewekwa karibu na Suez canal kwa ajili ya kumonitor ndege za Israel na makomandoo waliokuwa wametumwa kwenda kuilipua walirudi na kutoa taarifa kwamba hakuna haja ya kuilipua, ile ni ya kwenda kuchukua tu kwani hapakuwa na ulinzi makini. Na kweli walikwenda wakawaua walinzi, wakaifungua na kuibeba kwa helikopter mpaka kwao.

  Hawa jamaa ni mwisho wa maneno na ndio maana dunia inawaogopa including nchi za europe na marekani yenyewe. Huwezi kusikia marekani ikilaani kilichofanywa na muisrael.

  Tiba
   
Loading...